Maziko ya Sheikh Thabit Kombo Jecha 1986

Maziko ya Sheikh Thabit Kombo Jecha 1986

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
622
Reaction score
431
๐— ๐—”๐—ญ๐—œ๐—ž๐—ข ๐—ฌ๐—” ๐—ฆ๐—›๐—˜๐—œ๐—ž๐—› ๐—ง๐—›๐—”๐—•๐—œ๐—ง ๐—ž๐—ข๐— ๐—•๐—ข ๐—๐—˜๐—–๐—›๐—” ๐Ÿญ๐Ÿต๐Ÿด๐Ÿฒ

Na Mwandishi wetu wa Medani za Kihistoria na Siasa.

Waliosimama mbele ya Jeneza la Marehemu Mzee Kombo, Wakwanza kutoka kushoto walioko chini wakati huo na vyeo vyao kwa wakati huo ni :

Waziri Kiongozi wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, anayefuata ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Sheikh Idriss Abdulwakil, Aliyesimama ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wakti huo na Rais mstaafu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa mwenye huzuni na majonzi makubwa.

Wengine walioko chini ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi (anaonekana akifuta machozi kwa leso), Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mzee Rashid Mfaume Kawawa.

Waliokaa nyuma kulia ni Mzee Maarufu Zanzibar na Kiongozi wakti Jumuiya ya Ismailia wa Aga Khan wakti huo Mzee MohamedAli Jinnah (Baba yake Mwandishi Habari Nguli
Na TV Presenter wa ITV na IPP, Ndg. Farouk Karim) ambaye pia ni kiongozi wa Jumuiya ya Agha Khan Ismailia kwa Zanzibar na Kiongozi wa Jumuiya ya Ibbadhi Mzee Ahmed Salum Ruwehi (AlRuweihy ama AlRawahy).

Leo Miaka 40 kamili Tunapokumbuka tarehe Kama ya Leo ya kumbukizi hii ya siku ya maziko ya Al Marhuum Sheikh Thabit Kombo Jecha, tunavuta kumbukumbu ya kihisia ya muasisi huyu na hatua za mapambano ya Ukombozi wa Zanzibar pamoja Kiungo kikuu cha Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar na kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliopo hivi sasa Ambayo Ambayo imetimiza miaka 62 ya Muungano huo na kuufanya Muungano wa Muda mrefu zaidi duniani kuliko Miunganiko yote mengine Kihistoria Ambayo baadhi yake ilishavunjika.

Katika historia hiyo ya Muungano na Uwepo Taifa la Tanzanoa, Ni vigumu sana kumtenganisha Sheikh Thabit Kombo Jecha na historia ya Zanzibar ya wakati huo na sasa hata wakti wa kuunganisha Vyama Viwili Vikuu vya Ukombozi vya TANU na Afro Shirazi ASP na kuzaliwa kwa CCM hapo hapo Amani Zanzibar.

Mbali na kuwa Katibu Mkuu wa Kwanza hadi mwisho wa Chama cha Afro Shirazi, ASP yeye ndiye aliyechora ramani nzima ya Zanzibar kujitawala kupitia ASP kwa kushiriki na kuongoza mikakati yote ya kiintelijensia kuhakikisha Zanzibar inajitawala akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Watu 20 ya kuunda Katiba ya Kwanza ya Chama ikiwa na Wajumbe kumi kutoka kila Upande wa Muungano huo huku Katibu Mkuu wa Kamati yake hiyo akiwa Mzee Pius Msekwa.

Sheikh Kombo Jecha pia atakumbukwa kwa kujitambulisha Rasmi ASP Tanganyika kwa Mwalimu Nyerere ambaye alijijengea Heshima kubwa kwa Mwalimu na inasemekana hadi leo katika Tarikhi na Historia Kuwa ndiye mtu ambaye Mwalimu alikuwa akimheshimu kwa kiwango cha juu kabisa katika Medani zote za Kisiasa.

NYUMA kabisa ya picha kulia wawili wanaozungumza kwa ishara ni wa kwanza kushoto aliyevaa Kanzu ni Balozi Dkt Mahmoud Thabit Kombo ambaye sasa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye ni mtoto wa mwisho wa Sheikh Thabit Kombo Jecha.

IMG-20261026-WA0096.jpg
 
Back
Top Bottom