Mawakili wa utetezi wakwamisha uamuzi mdogo kesi ya Sabaya

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
5,079
8,219
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo Jumatano Desemba 29, 2021 imeshindwa kutoa uamuzi mdogo katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita baada ya mawakili wa utetezi kushindwa kufika mahakamani.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27 ya mwaka huu, mbali na Sabaya watuhumiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

"Mahakama inakuwa haipo katika nafasi ya kutoa uamuzi huo mdogo labda kama washitakiwa wataondoa uwakilishi. Tunaomba tupangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutoa uamuzi huo mdogo,"

Hakimu Kisinda aliwauliza watuhumiwa hao iwapo bado wanauwakilishwa na mawakili wao ambapo waliieleza mahakama bado wanawakilishwa.

Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 3, 2022 kwa ajili ya uamuzi huo mdogo ambapo pia aliutaka upande wa Jamhuri kuhakikisha shahidi aliyekuwa anaendelea kutoa ushahidi wake anakuwepo mahakamani hapo kwani baada ya uamuzi huo ataendelea.

Watuhumiwa hao wanatetewa na Mawakili Mosses Mahuna, Fauzia Mustafa, Edmund Ngemela, Sylvester Kahunduka na Fridolin Bwemelo.

1640772397652.png


Mwananchi
 
Back
Top Bottom