Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,501
- 9,280
TANGA: Mawakala wa CHADEMA, ACT-Wazalendo, CUF na NCCR-Mageuzi wakamatwa baada kuzuia wapiga kura kuingia kituoni kwa madai ya wao kutopewa barua
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Blasius Chatanda amesema baadhi ya mawakala wa vyama tofauti vya siasa wamekamatwa kwa madai ya kuzuia wananchi kupiga kura kwa kufunga milango.
Amesema walizuia wananchi kupiga kura kwa madai ya wao kutopewa barua za kuwatambulisha ili waruhusiwe kuingia kwenye vituo vya kupigia kura.
Kamanda Chatanda amesema mawakala hao ambao baadhi walizungumza na Mwananchi Digital kabla ya kukamatwa,walikuwa katika vituo vya Tongoni na Ofisi ya Mtendaji ya Kata ya Ngamiani Kusini .
"Ni kweli baadhi ya wafuasi wa vyama vya siasa tunawashikilia kwa mahoajino kwa sababu kulikuwa na kutoelewana kwenye vituo walivyokuwepo jambo ambalo lingeweza kuleta vurugu kama tungewaacha waendelee kuwepo kwenye maeneo hayo," amesema.
Hata hivyo amesema wapo ambao waliwaelewesha na kuwaachilia kutokana na kuonekana walikosa elimu na hivyo kushindwa kufuata utaratibu
Chanzo: Mwananchi