Selasini asema CHADEMA iliviua vyama vingine 2015, Zitto asema ACT Wazalendo haifanyi siasa za kuachiana Majimbo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,897
141,834
Baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mbowe kusema chama chake hakihitaji ushirikiano au muungano na vyama vingine vya upinzani baadhi ya viongozi wa upinzani wamemshukia kama mwewe.

Selasini wa NCCR mageuzi amesema 2015 CHADEMA kupitia UKAWA ulikuwa na mkakati wa kuviuwa vyama vingine vya upinzani na ilifanikiwa kuidhoofisha NCCR Mageuzi na CUF.

Selasini amesema kamwe hawatarudia makosa ya kushirikiana na CHADEMA katika jambo lolote.

Naye KC Zitto Kabwe wa ACT Wazalendo amesema chama chake kinafanya Siasa za nchi nzima na siyo Siasa nyepesi za kuachiana Majimbo.

Mengi utayakuta Mwananchi.

Ngoma inogile!
 
Katika kosa CDM walifanya mwaka 2015 ni kumpokea Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea urais, na juu ya kosa hilo ni kukubali kuungana na vyama vingine vya upinzani. Jambo lile ilikuwa ni kama kufaidisha vyama vingine vilivyokuwa kwenye ukawa, bila vyama hivyo kuwa vimefanya kazi ya kuvuta wapiga kura.

CDM isikosee tena kuungana na vyama vingine, ama kutoa nafasi za kigombea kutoka kwa mtu yoyote ambaye hakuwa mwanachama wa CDM, muda mfupi kabla ya uchaguzi. Kila chama kishinde mechi zake, maana hii miungano inatumika kuchafuana, kutengenezea usaliti na uhasama usio na tija.
 
Chadema imeshaungana na CCM vyama vingine itavikuta huko huko!
 
CHADEMA itaachiana majimbo na CCM hao wengine watulie kwa sasa!
 
Back
Top Bottom