Mauzauza ya mke wangu

Mkuu hujasema kwamba tatizo hilo lina muda gani ?
Ndoa yenu ina muda gani ?
Mkuu unataka u solve tatizo la mkeo au umkomoe mkeo?
 
Nataka ndoa yangu iwe na amani na furaha kama mwanzo maelewano ndani hamna.
 
Dawa ya moto ni moto jaribu utasema ndio
 
dah,ndoa hizi...wakati yako inafuka moshi,ya mwenzio inawaka moto....pole
 
Mrudishe kwao na waambie wazazi wake kuwa atarudi nyumbani
pale tu utapoenda kumchukua wewe mwenyewe.
 
Mtwange yellow card, asipojirekebisha piga pyepyeeeeee then mtwange Red Card atoke ndani na wewe usifanya substation si unajua red card haina substation
Aisee.......substation!
Kipaumbele i. Elimu, 2. Elimu, 3. Elimu tarehe 25 oct.
 
Subiri mpaka jpili ukishampigia kura yako Lowassa, mbunge wa UKAWA na diwani wa UKAWA unaweza kusepa.
 
Binafsi nataka niondoke nyumbani walau nikapumzike mbali na jiji hili for 6months.ushauri tafadhari.

You are damn wrong.
Usikimbie kadhia, tatua ukiwa humo humo ndani. Wewe ni kichwa cha familia, onesha uanaume wako. Na yeye akisepa kwa miezi hiyo sita unadhani patakua na nyumba tena hapo? Solve kadhia hizo ukiwa humo humo
 
Mkuu jamaa anaomba ushauri wala haja lalamika.
Mkuu hivi huelewi nini maana ya mwanaume kuwa kichwa? Ni kuweza kusimamia nyumba yako ipasavyo, Kama unaweza kumwachia mke wako akafanya maamuzi yake bila wewe kuhusika huoni kama ni kushindwa kuisimamia nyumba yako!!! Unawezaje sema unataka kuondoka nyumbani kwako Simama sema kuanzia leo sitaki moja,mbili, tatu mwambie mwanamke kama hawezi kuacha ni vigumu kuwa pamoja basi na iwe hivyo sio kukimbia nyumba!!
 
70% my wife!hata mie nilitaka kukimbia nyumba lkn nikaghairi nikajifunza kutokumuongelesha, "mzigo?? Nikaanza kuchepuka" tena sina mpango hata yeye akitaka akechepuke tu!3 month kanyooka, yeye ndio anabembeleza!
 
Natoa ushauri huu kwa unyenyekevu sana tafadhali kabla ujaamua kutengana au kuachana na mkeo au mumeo onana na mwanasheria na wala sio padre au mchungaji au sheikh, utapata ushauri mzuri sana kuhusu usalama wako wewe na wa mali zako

Khaaa jamaniii yamekua hayo tena,mali kwanza???
 
Dah huyu sasa kazidi, mpeleke Kwa Gwajima atarudi amenyooka
 
Ondoka nyumbani.........
Maisha mafupi haya mkuu....
usipoteze muda na wapumbavu.....
 
70% my wife!hata mie nilitaka kukimbia nyumba lkn nikaghairi nikajifunza kutokumuongelesha, "mzigo?? Nikaanza kuchepuka" tena sina mpango hata yeye akitaka akechepuke tu!3 month kanyooka, yeye ndio anabembeleza!

Duuh mkuu, ntakutafuta nione jinsi hii strategy yako inavyofanya kazi
 
Nitarudi kwenye jukwaa hili kwa mrejesho .
Ushauri wenu ni muhimu sana kwangu.

Naheshimu mawazo yakila mwana jukwaa.

Mbarikiwe sana.
 

kama aliyesema "the way a person writes reflects his personality then kweli kuna tatizo...no one should be quick kujudge kam we ndio una tatizo au mkeo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…