navin-govind
Member
- Apr 10, 2015
- 72
- 112
Wadau nawasalimu,
Kuna mgogoro wa kifamilia unafukuta nyumbani kwangu,
Ni kwamba kuna kaka yangu ambae alipata matatizo na yupo jela sasa takribani mwaka wa pili akitumikia kifungo cha miaka saba.
Huku nje familia yake ilishindwa kumudu kodi ya nyumba baada ya kodi aliyolipa jamaa kuisha, mkewe alikuja kuniona kwa ajili ya hilo, nami nikaliwasilisha kwa wazee ambapo walishauri niichukue hiyo familia tukae pamoja kwangu kwa kujibanabana hivyo hivyo.
Kwa kuwa kumlipia kodi kwa kweli kwa majukumu niliyonayo nisingeweza, maana ada za shule za watoto wake ni mimi pia ndio nalipa kwa sasa, tuliwatoa shule za gharama na kuwaleta za kawaida.
Wakahamia kwangu yeye na watoto wake, tunaamini kuwa miaka mitano iliyobaki katika kifungo si mingi sana, tukimwacha mwanamke aende njia yake si ajabu jamaa akatoka huku familia imepotea au kuchukuliwa na jitu lingine ukizingatia mwanamke hakua na kazi, ni house wife na wote tunajua jinsi hawa wenzetu walivyo dhaifu, nadhani wengi mmeshasikia simulizi nyingi za watu waliofungwa waliwakuta wake zao wako wapi pindi walipotoka huko.
Nyumbani amani imetoweka sasa, kati ya mke wangu na huyo shemeji yangu, huyu shemeji kiukweli ni mchapa kazi na mwenye heshima ya hali ya juu, nikirudi kutoka kazini huja mlangoni kunifungulia geti, baada ya hapo huja kwenye gari hunipa shikamoo huku amepiga magoti na kupokea kwa unyenyekevu mzigo wowote ninaokua nao.
Nikitoka kwenda bar nikirudi saa tano saa sita usiku huja kunifungulia geti anamzuia housegirl asiamke anakuja yeye, kisha hunipakulia chakula na kunikaribisha, ananisubiria anatoa vyombo na kuni wish good night.
Sasa hii treatment ambayo huyu shemeji ananipa imemkasirisha sana mke wangu ambae kwa kweli nimeshasahau mara ya mwisho ni lini alinikirimu hivi, mimi uhudumiwa na hg na wengi wao huwa viburi sio kama anavyofanya shemeji, Sasa umezuka ugomvi mkubwa ndani kati ya mke wangu na shemeji.
Usiku silali naambiwa nichague nimfukuze shemeji au yeye aondoke eti kama nimeona shemeji ni bora, mke wangu sasa haendi kulala mapema anakaa sitting room na shemeji hadi saa sita hadi nifike ili aone kama kuna kitu kinafanyika, ameshatangazia wanaukoo kuwa mimi na shemeji kuna kitu kinaendelea jambo ambalo sio la kweli.
Pia shemeji anapenda kuniita kwa jina la "" mume"" juzi mke wangu alimsikia akiniita hivyo na kumuuliza mume wako na nani ukazuka ugomvi mkubwa sana, wakati mwingine naporudi usiku mwingi shemeji anakua yupo ukumbini na mavazi ya kulalia akitazama series, mke wangu nae anatoka kuja kunisubiria hapo hapo akidhani kuna kitu labda tutafanya hapo na shemeji, hawazungumzishani kitu hadi mimi napofika, yule shemeji anawahi mezani kunipakulia chakula.
Juzi juzi tulikua tunakunywa bia mimi na shemeji yangu mahala fulani, huwa namtoa out mara moja moja ili walau apoteze mawazo ya matatizo yaliyowapata, nikatumia Muda huo kuongea ili ajishushe kuepusha ugomvi usiokua wa lazima pale home lakini akanijibu kuwa wife ndio anapaswa kujishusha kwa kuwa ni mdogo kwake.
La hasha nikampangie kwake yeye na wanawe niwe namhudumia huko, nikamjibu sina uwezo huo wa kuhudumia familia mbili, ukizingatia kuwa ndugu ni kama wamenitelekezea mimi huu mzigo kila mtu anajifanya yupo busy na wengine wakilia ugumu wa maisha.
Wadau mnanishauri nini kuhusu tatizo hili, maana hali sasa ni tete, mke wangu amenipa ultimatum kwamba nimuondoe shemeji or else aondoke yeye, mimi tatizo langu kubwa ni wale watoto, hatima yao, inafikia hatua sasa mke wangu anawazuia watoto wetu wasicheze pamoja na wale wa kaka kutokana na ugomvi na mama yao.
Msaada wa haraka unahitajika