Maumivu makali

Maumivu makali

me bado kidogo sana babu
Na ww kwa umri huo umeshamaliza vibarua vyako vyote au unamsumbua bb dc

Mie ni mstaafu na kibogoyo bwana. Siwezi tena kufakamia nyama choma hata kama nazitamani.


Hahaa kweli aisee ila mimi ya mjukuu wako nachokonoa ili nisije nikauvaa mkenge

Sawa tu ila endelea kuandaa heading ya thread kwani probability ya kukutana na ujumbe tata ni kubwa tu
 
katika mahusiano yote niliyopitia nilikuwa nikiponzwa na Upole na Ile Hali ya kumuamini mtu kupita Uwezo. Kipindi nipo CBE niliingia katika Mahusiano na Binti mmoja ambaye nilikuwa nikimpenda na Kumthamini kuliko Hata Mama Yangu Mzazi..

Kila alichokuwa Akinieleza nilikuwa nikikubali na kuamini.. Nilimuonyesha kila aina Ya mapenzi, nilimuonyesha ni Jinsi gani Mwanamke Anatakiwa kupendwa... Alikuwa Huru kushika na Kuangalia Chochote.. Iwe Simu; lap top na Vingine vingine kibao. Na hata Yeye alinipa Uhuru Huo kitu Ambacho kiliongeza Upendo Wangu kwake.

Kumbe nilikuwa nikifanywa Mjinga, Mpumbavu na Limbukeni.. Kumbe wakati nikiamini nipo mimi kama mimi kumbe mwenzangu Alikuwa na Mtu wa Pembeni. Na ili mimi nisigundue Akanunua Simu ambayo Ilikuwa Akiificha na kuchati na watu wake akiwa kwao ama mbali na Wewe.

MUNGU hakutaka kumficha mnafiki, Mungu hakutaka niendelee kudanganywa. Ilikuwa Siku ambayo nilikuwa katika Maandalizi Ya Semister nikiwa Nimejiinamia Simu Yangu Ikaingia Sms Upande Wa WhatsAp... Sijui ni kitu gani kilinipata lakini Nilijikuta nikiogopa kuifungua Ile Sms.. Wakati Nikiendelea kujifikiria zikaanza kuingia sms Mfululizo nikaona Bora Nizisome....

Nikaifungua Sms Ya kwanza Ambayo Ilionekana kutumwa na Namba Ngeni.... Hapo nikakutana na Picha Ya mwanamke niliyempenda Akiwa Uchi tena Huku Amekumbatiwa kwa nyuma.. Sijawahi kuumia, kulia kama Nilivyoumia Siku Hiyo..

Bahati Mbaya Nikaharibu Masomo Yangu.. Ibrah Nikadisco na Hata niliporudia mwaka bado nikaangukia pua.. Ingawa ni Mtu Mwenye jina kwasasa Lakini Namchukia mpaka naingia kaburini
Mmh shem umepitia makubwa khaa, no wonder una negativities nyingi na mapenzi. Stay away from mahusiano, jiponeshe maumivu yako kwanza
 
Pole ibra87,

Dunia haiko fair na kila uande unahusika kwenye huu upuuzi!
 
Last edited by a moderator:
Heeeeeee..........

Pole ibra87
 
Last edited by a moderator:
Mmh shem umepitia makubwa khaa, no wonder una negativities nyingi na mapenzi. Stay away from mahusiano, jiponeshe maumivu yako kwanza
Ndiyo maana tunawambia kuwa ukiona nyani Mzee basi ujue keshakwepa mishale kibao.

Kwa wale wanaoweza, ni muhimu kupenda kwa akili badala ya moyo!
 
Aah babu kikombe hiki ni kichungu khaa

Kwa vile ni lazima kukinywea basi tujifunze kunywa kwa machale.

Hata hivyo zama zenu zimekuwa na changamoto nyingi. Sie kuwasiliana na mpenzi ilikuwa kwa barua ambayo inajibiwa siyo chini ya mwezi.
 
Mimi ni dada wa miaka 38 nina watoto 3 kwenye ndoa nina miaka 13, mume wangu ana umri miaka 52.

Mwaka huu mwanzoni nilifuma sms kwenye simu ya mume wangu akijibu sms ya mchepuko.

Ni hivi mchepuko alimwandikia kwamba ana mimba yake, yeye akajibu kwamba sio mimba yake siku ambayo walikutana yeye akumaliza (sijui alikuwa na mana gani). Hiki kitu kimeniumiza sana moyo.

Nilikuwa nina uhakika kwamba anachepuka lakini nikajipa moyo anatumia condom. Baada ya kufuma hiyo sms ndio nikaamini kwamba ana kwenda bila kinga. Hiki kitu kinaniumiza sana moyo sijui nifanye nini ili nisahau, ukizingatia magojwa yalivyo mengi! Inatisha kwelikweli.

Naomba ushauri nitumia njia gani ili nikifute kwenye mawazo yangu.

Mwathirika.

Ungeupigia simu mchepuko kwa uhakika zaidi,
 
Kwa vile ni lazima kukinywea basi tujifunze kunywa kwa machale.

Hata hivyo zama zenu zimekuwa na changamoto nyingi. Sie kuwasiliana na mpenzi ilikuwa kwa barua ambayo inajibiwa siyo chini ya mwezi.
Mmh babu teknolojia imetusaidia lakini pia madhara yake kwenye uhusiano Mmh. Bora enzi zenu kwa kweli
 
daah....condom huwa inanifanya nisifurahie tendo kabisa . haina tofaut na punyeto
 
Mmh shem umepitia makubwa khaa, no wonder una negativities nyingi na mapenzi. Stay away from mahusiano, jiponeshe maumivu yako kwanza

yeah shem kuna kipindi nilitamani kwenda hata kujitumbukiza baharini.. Lakini Mungu ni mwema na Ananipenda bado.. Japo kuwa nikisemaga mnaona kama nawachukia lakini sina jinsi..
 
Mmh babu teknolojia imetusaidia lakini pia madhara yake kwenye uhusiano Mmh. Bora enzi zenu kwa kweli

Kiranga cha kushika simu kiliniisha enzi za usichana wangu sithubutu ng'ooooo, na ni zaidi ya marufuku kushika simu yangu, utachokikuta marufuku kunihoji, jihoji na ujijibu mwenyewe.
 
yeah shem kuna kipindi nilitamani kwenda hata kujitumbukiza baharini.. Lakini Mungu ni mwema na Ananipenda bado.. Japo kuwa nikisemaga mnaona kama nawachukia lakini sina jinsi..
I can feel you. Shem tuseme tu, na Sisi tunawasema pia, maana pande zote tunaumizana. Pole kwa yote na Mshukuru Mungu kwa yote pia
 
Kiranga cha kushika simu kiliniisha enzi za usichana wangu sithubutu ng'ooooo, na ni zaidi ya marufuku kushika simu yangu, utachokikuta marufuku kunihoji, jihoji na ujijibu mwenyewe.
Hahaha me naona hadi siku nidondoke kwa presha ndo ntaacha. Sasa wewe ni mtata, muache mwenzio ashike yako, yake usishike coz umeamua teh teh. Nipe umbea kidogo ulikuta breaking news gani humo
 
Siku Zote Tambua kuwa Mwanaume Anapatikana Popote lakini Uhai haupatkani Hata Kwa Kiasi gani Cha Pesa... Kutokujali kwa mumeo hasa anapokuwa mbali na wewe inaonyesha ni Rahisi Kukuletea Magonjwa Ya Zinaa likiwemo la Ukimwi. Unadhani Ukipata Ukimwi nani Atakuwa Ameharibu Maisha Yake?

Machozi Hayawezi kukuondolea Hali hii wala hayataitibu Tabia Ya Mumeo bali Machozi Yako Yanaweza kuwa ni Silaha Ya Mwisho kukuua.

Wafikirie Watoto Wako Kisha Jifikirie Wewe, Waonee huruma Wao na Jionee Huruma Wewe. Kulia na kulalama Sio Suluhisho la Hilo tatizo...

Chakufanya Muweke Chini na Mueleze Ukweli Juu Ya kile Ulichokikuta kwenye simu. Usimuogope kwa kuwa ni Mumeo na usimuogope kwa kuwa Unaona Mtagombana unachotakiwa ni Kuipigania ndoa Yako na watoto wako..

Ukiona Hasikii muitie Wazee Au Viongozi wa DINI na iwapo Itashindikana Unaweza kutoa Msimamo wako katika suala hilo.

Mweeeh!! Ibra wewe kila ukisimulia ni majanga tu, pole mwaya, mahusiano ni kizungumkuti.
 
Back
Top Bottom