Maumivu makali

Maumivu makali

Huyo mwanamume ni mzembe sana....

Utaendaje kwa wife na sms za namna hiyo? Alishindwa nini kusafisha uchafu wake na kwenda kwa mkewa akiwa msafi kama mtoto aliyeiba sukari au mboga jikoni anavyokuwa mtakatifu mbele ya mama?

He has to pay the price.. ingawa atashinda mchezo!
We acha tu, ukinogewa kaka ni hatari sana.
 
Mimi ni dada wa miaka 38 nina watoto 3 kwenye ndoa nina miaka 13, mume wangu ana umri miaka 52.

Mwaka huu mwanzoni nilifuma sms kwenye simu ya mume wangu akijibu sms ya mchepuko.

Ni hivi mchepuko alimwandikia kwamba ana mimba yake, yeye akajibu kwamba sio mimba yake siku ambayo walikutana yeye akumaliza (sijui alikuwa na mana gani). Hiki kitu kimeniumiza sana moyo.

Nilikuwa nina uhakika kwamba anachepuka lakini nikajipa moyo anatumia condom. Baada ya kufuma hiyo sms ndio nikaamini kwamba ana kwenda bila kinga. Hiki kitu kinaniumiza sana moyo sijui nifanye nini ili nisahau, ukizingatia magojwa yalivyo mengi! Inatisha kwelikweli.

Naomba ushauri nitumia njia gani ili nikifute kwenye mawazo yangu.

Mwathirika.
Hapa kazi ipo. Michepuko hii inaleta tabu sana ndani ya nyumba. Piga goti dada yangu kumuombea huyo mzee wako aponywe na hilo pepo..
 
Mtoa mada inaonekana huwa unachepuka kwa kutumia condom au mmekubariana mkichepuka mtumie kondom ndio maana unalalamika hapa
 
Hakuna kinachobadilika ila huwezi kumzuia mtu mzima mwenye akili zake kufanya atakacho.

I wish nikupe story yangu kidogo kuhusu simu ila inaumiza kwa upande wangu so sipendi kabisa kushika simu ya mwanaume
Huoni hapo kwa kushika simu imemsaidia kujua mme anaenda peku...
Bora kajua mapema ili ata akiambukizwa kuanzia sasa iwe ni kwa maamuzi yake na sio hakujua...
Kutoshika simu ya mmewe ni sawa na kutembea kwenye giza, kuna mambo unayoweza kuyaepusha endapo unashika simu yake,believe me bora kuumizwa na mambo mengine lakini sio kuambukizwa magonjwa na mmeo....
 
A 52yr old man cheating on his wife, so pathetic ekse! Nini anachohitaji huyu katika maisha ambacho hajakiona na kukiishi. Miaka 52 kweli...? Kweli kuna kukua mwili huku akili zikiwa changa..
 
Pole sana ,huwezi kumzuia amefikia critical age of cheating with surplus funds 50-65 yrs
 
Back
Top Bottom