Pole sana mpendwa
Tina Buu kwa yaliyokufika. Hakuna kidonda kisichopona ila wakati mwingine kidonda hicho kinaweza kuchukua mda mrefu kupona kutegemea na ukubwa wa kidonda hicho na infections zilizomo kwenye kidonda hicho, hivyo hata wewe hayo maumivu na mawazo yataondoka tu kadiri muda inavyozidi kwenda endapo utajitahidi kusamehe na kusahau.
Pia nakushauri uende ukapime magonjwa ya zinaa hasa UKIMWI ili ujue kama umeathirika au la. Na kama hujaathirika basi ni vyema umshukuru Mungu na uchukue tahadhari ili usipate maambukizi. Na kama itatokea majibu yakasema kuwa umeathirika basi usikate tamaa kwani kuathirika sio mwisho wa maisha. Endelea kuishi maisha yako kama ulivyozoea huku ukiomba msaada wa Mungu ili kwa upendo na huruma yake kwako akuponye huo ugonjwa ambao umeupata pasipo kutarajia maana yeye ni muweza wa yote na hakuna kinachoshindikana kwake.