Maudhi ya operesheni kimbunga!!

Maudhi ya operesheni kimbunga!!

Na walimu 10,000 wa Kenya walioambiwa wajiandikishe wanatoka Commoro?
KWa sababu Raia wa Rwanda na Burundi walishapewa option ya kuwa raia wakakataa na option ya ku legalize wakataa na ndio maana wakishikwa tu lazima warudishwe. Maana option zingine hazifanyi kazi zaidi ya hiyo ya kuwarudisha.

Msikilize huyu ndo aliwapa option hizo, sasa wewe unatagemea nini? msikilize huyu bwana mpaka mwisho.

PRESIDENT KIKWETE ON ILLEGAL IMMIGRANTS' REPATRIATION FROM TANZANIA - YouTube

mkuu apo kwenye red,wameambiwa walipie dollar 2000 sawa na 3,200,000 kwa mwaka kwa kila mwalimu na uwa inapanda kila mwaka,je wale wamalawi waliambiwa walipe ?
 
kwa hiyo wewe unataka kuishi tanzania kwa nguvu kwani huna kwenu?
 
mkuu apo kwenye red,wameambiwa walipie dollar 2000 sawa na 3,200,000 kwa mwaka kwa kila mwalimu na uwa inapanda kila mwaka,je wale wamalawi waliambiwa walipe ?

Wamalawi sio wafanyakazi hawahitaji working permit, watalipia bei ya residence card, pale watakapopewa hizo card. Tofautisha kati ya working permit na kadi ya makazi. Hiyo bei hapo juu ni ya working permit, kwa wamalawi wanaofanya kazi nao itabidi walipe hiyo dolla. Lakini umemsikiliza huyo bwana mpaka mwisho? link niliokuwekea hapo juu.
 
Hapo kuna issue gani wakati serikali inatimiza wajibu wake? au nawe mhamiaji haramu? kama mtu alichukuliwa kwa mahojiano akaonyesha vilelezo kisha akaachiwa kuna ubaya gani? kwanza huyo jamaa si ndiyo yule aliyeleta thread ya kuichafua Tanzania katika sakata la Immigration JNIA Airport?

Ninajua labda wewe ni employee katika baadhi ya vyombo hivi. hivyo sishangai ukitoa comments za namna hiyo. Lakini kumbuka kuwa hao jamaa wakti mwingine hawatumii hata akiri ndgu yangu!! Jaribu kufikiri hata kidogo! Hawatumii akiri you might think these People have never been to School! Pili wewe hili swala halijakugusa labda hata ndugu yako hajaguswa lkn kwa watu ambao wamesumbuliwa nafikiri wana haki ya kuwakemea hawa watu. Mawazo ya Rais yalikuwa mazuri lkn watendeja ni mbumbumbu labda kama WEWE!
 
Mi nashangaa jambo moja,hiyo operation inaangalia Raia wa mipakani tu mbona wanawaacha Wachina na Wahindi wamejazana kibao viwandani na mitaani???? Mfano mzuri waende Kiwanda cha Nguo 21st Century pale Morogoro mule ndani ya kiwanda wapo wengi na hawatoki mule ndani hata siku moja mwisho getini

Uthibitisho wa uraia
Je katika zoezi la kuwaondoa wahamiaji haramu.Naomba kuuliza,leo hii tukipita nyumba kwa nyumba Tanzania nzima,je ni watu wangapi wataweza kuthibitisha uraia wao?Inawezekana hata wewe unayesoma ujumbe huu sii raiya halali.kuwa tu na vitambulisho haitoshi kuwa Raiya.Kama ni uraiya wa kwa kuzaliwa je una nyaraka zinazoonesha we ulizaliwa Tanzania?Kama ni wa kuandikishwa una cheti za kuzaliwa au nyaraka yoyote ya uhamiaji?Kama vyote hivi huna inatosha kuthibitisha kuwa ni mhamiajia haramu.​
 
thatha ,
  • Acheni ubagauzi....Uthibitisho wa uraia
    Je katika zoezi la kuwaondoa wahamiaji haramu.Naomba kuuliza,leo hii tukipita nyumba kwa nyumba Tanzania nzima,je ni watu wangapi wataweza kuthibitisha uraia wao?Inawezekana hata wewe unayesoma ujumbe huu sii raiya halali.kuwa tu na vitambulisho haitoshi kuwa Raiya.Kama ni uraiya wa kwa kuzaliwa je una nyaraka zinazoonesha we ulizaliwa Tanzania?Kama ni wa kuandikishwa una cheti za kuzaliwa au nyaraka yoyote ya uhamiaji?Kama vyote hivi huna inatosha kuthibitisha kuwa ni mhamiajia haramu.​
 
Wamalawi sio wafanyakazi hawahitaji working permit, watalipia bei ya residence card, pale watakapopewa hizo card. Tofautisha kati ya working permit na kadi ya makazi. Hiyo bei hapo juu ni ya working permit, kwa wamalawi wanaofanya kazi nao itabidi walipe hiyo dolla. Lakini umemsikiliza huyo bwana mpaka mwisho? link niliokuwekea hapo juu.

vizuri. lakin mbona raia wa uganda.kenya na rwanda watimuliwe kama mbuzi na raia wa malawi waambiwe wakajiandikishe wapate vibali? nijibu mkuu
 
Watanzania asilia wapo. Ni wale waliokutwa na mkoloni, wakazaana na hadi leo hii tuko na vitukuu vyao. Fuvu la mtu wa kale sana duniani lilipatikana Ngorongoro, Tanzania. Hii yote inathibitisha kuwa Watanzania asilia wapo. Swali lako kwa maofisa wa uhamiaji halikuwa na mashiko.

Hacha kuipotosha dunia! Tanzania haipo kabla ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar! Mkoloni hakuwahi kuikuta Tanzania wala kuwakuta Watanzania!

Na tukiendelea na siasa hizi za maji taka na kwa fikra hizi za kichwa nazi kamwe hatutafika mbali!!!
 
jidodo jaribu kutumia busara na kama hauna kakope tafadhari. Unatia aibu tu kwa JF pamoja na Taifa. Huyu jamaa ana issue!

wabuyaga! usiangaike na jidodo. Ana mazoea ya kuiacha akili yake pembeni anapojaribu kuchangia mada !
 
Ninajua labda wewe ni employee katika baadhi ya vyombo hivi. hivyo sishangai ukitoa comments za namna hiyo. Lakini kumbuka kuwa hao jamaa wakti mwingine hawatumii hata akiri ndgu yangu!! Jaribu kufikiri hata kidogo! Hawatumii akiri you might think these People have never been to School! Pili wewe hili swala halijakugusa labda hata ndugu yako hajaguswa lkn kwa watu ambao wamesumbuliwa nafikiri wana haki ya kuwakemea hawa watu. Mawazo ya Rais yalikuwa mazuri lkn watendeja ni mbumbumbu labda kama WEWE!

Safi sana! Kama kuna mambo ya kijinga yanafanyika pale JNIA watu wasiseme? Acheni kufanya kazi kwa mazoea ya kijinga jinga enyi watu! Dunia inawaona na inawachukulia kama mazezeta fulani hivi!
 
Come sun come rain...wahamiaji haramu hawakubaliki tanzania ya sasa na hasa hawa wanaotumia kigezo cha eac.

Eac haifuti mipaka ya nchi husika na watu kuingia kwa jirani kama unaingia choo cha uswaz mlango gunia hodi ya nini.
 
umemjibu vizuri sana,ila hawwezi kukuelwa kwa sababu ni haramu.....
Watanzania asilia wapo. Ni wale waliokutwa na mkoloni, wakazaana na hadi leo hii tuko na vitukuu vyao. Fuvu la mtu wa kale sana duniani lilipatikana Ngorongoro, Tanzania. Hii yote inathibitisha kuwa Watanzania asilia wapo. Swali lako kwa maofisa wa uhamiaji halikuwa na mashiko.
 
tumia akili kufikiria,haikuwepo kweli lkn kunawatu tunaoitwa Watanzania,jiulize tumetokana na nini?...mnalazimisha mamabo,vp kwenu kuna njaaa....nendeni tutawaleteeni chakula,jifunzeni kulima....kwa nn ufuatwe wewe tu wakati kuna watu wa aina yako wengi tu...au mnataka mpaka muanze kupigwa na vitu vyenye ncha kali....tumewachoka....Kiswahili chako tu kinaonesha wewe si mwenzetu ona hapo kwenye nyekunduka
Hacha kuipotosha dunia! Tanzania haipo kabla ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar! Mkoloni hakuwahi kuikuta Tanzania wala kuwakuta Watanzania!

Na tukiendelea na siasa hizi za maji taka na kwa fikra hizi za kichwa nazi kamwe hatutafika mbali!!!
 
Hili zoezi ni zuri sana lakini linavyotekelezwa ndio issue...mtu anakushusha kwenye basi lets say Rorya mnz au kasulu Dar,kisa jina lako ni otieno au nkuruzinza,thats un acceptable..sisi waluo majina yetu yanatokana na muda au msimu uliozaliwa..kuna jirani yetu mmoja tena baba yake mwanajeshi hadi leo..aliulizwa mbona unaitwa odhiambo wewe ni mkenya? Akawajibu odhiambo sio jina la wakenya mbwa nyie,odhiambo ni jina la kijaluo,which means nilizaliwa jioni..kuna makabila kama masai ole sekun wa tanzania na ole sendeka wa kenya hawana tofauti...cha msingi mimi ningepewa nafasi ya kushauri,ningeshauri msako ufanyike mlango to mlango kwa kuwausisha mabalozi na wenyeviti wa mtaa,kitongoji,watendaji nk..hili zoezi haliitaji haraka as such,utawezaje kumtofautisha mwita wa tarime na mwita wa lsbania? Hapa kinachotakiwa ni kutatua tatizo hili kidiplomasia zaidi...juzi nikiwa safarini kutoka mnz-Dar iliniuma sana mama mmoja kashushwa pale igunga na basi likamuacha kisa anasura ya kitusi,kumbe wala sio mtusi baba mnyantuzu mama mtusi,je huyu ni raia wa wapi? Tusifanye kazi kwa kukariri sura na majina..wengine majina yetu yana maana sana as per our traditions..eti ukiwa na jina la kisungu mwanzo mwisho hata ukiwa mhamiaji haramu haulizwi hata kidogo ili mradi unaitwa peter peter,au clinton barrack,hillary kery nk..operation kimbunga oyeeee.
 
vizuri. lakin mbona raia wa uganda.kenya na rwanda watimuliwe kama mbuzi na raia wa malawi waambiwe wakajiandikishe wapate vibali? nijibu mkuu

Hao raia wa uganda,kenya na rwanda waende tuh kwao pamoja na E africa yao. Lakini wa malawi ndugu zetu kabisa wa sadec,watabaki hao.
 
Watanzania asilia wapo. Ni wale waliokutwa na mkoloni, wakazaana na hadi leo hii tuko na vitukuu vyao. Fuvu la mtu wa kale sana duniani lilipatikana Ngorongoro, Tanzania. Hii yote inathibitisha kuwa Watanzania asilia wapo. Swali lako kwa maofisa wa uhamiaji halikuwa na mashiko.

INASIKITISHA SANA!
Yaani tunabaguana kwa sababu ya mipaka aliyoacha MKOLONI?

Hatukumbuki kabisa kabla ya kuja wakoloni Afrika ilikuwa ni moja.Japokuwa kulikuwa na tofauti za kikabila za hapa na pale lkn bado tuliheshimiana na kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.
Leo hii kutokana na mipaka ambayo wakoloni waliiweka kutokana na mkutano wa Berlin miaka ya 1880,tunaitana WAKIMBIZI na WAHAMIAJI HARAMU!Hv hizi dini tunazoziamini zinatusaidiaje?Tunaamini kuwa Mungu yupo wakati huohuo tunafanya vitendo kama Mungu hayupo.

TUACHE UNAFIKI!
 
Kwanini hamtaki kurudi kwenu? hakuna cha berlin wala mkoloni, hapa ni kimbunga hadi rwanda.
 
Tuache ubaguzi,wengine tusijione watz zaidi kuliko wengine,kama ni mtanzania mwenzetu na anaonewa lazima tumtetee kwa nguvu zote.Tumewafukuza watutsi sasa tunaanza kubaguana wenyewe,mwishowe tutasema hata Wakwere walitokea burundi enzi za biashara ya utumwa na baada ya uhuru kufuata ndugu zao Bagamoyo
 
Back
Top Bottom