Tuache ubaguzi,wengine tusijione watz zaidi kuliko wengine,kama ni mtanzania mwenzetu na anaonewa lazima tumtetee kwa nguvu zote.Tumewafukuza watutsi sasa tunaanza kubaguana wenyewe,mwishowe tutasema hata Wakwere walitokea burundi enzi za biashara ya utumwa na baada ya uhuru kufuata ndugu zao Bagamoyo
vizuri. Lakin mbona raia wa uganda.kenya na rwanda watimuliwe kama mbuzi na raia wa malawi waambiwe wakajiandikishe wapate vibali? Nijibu mkuu
Jipe moyo. Adha ya namna hii itampata kila mtu mahala popote. Ila zoezi lina nia njema, kwani uhamiaji haramu ni threat to the national security. Ugumu wake unatokana na kukosa national ID.
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
kwanza naomba ku-declare interest yangu hapa!
"i am not only a tanzanian or just a luo, but a citizen of the world...."
tarehe 16/09/2013 niliitwa uhamiaji makao makuu kwa kisingizio kuwa mimi si raia halali wa nchi ya tanzania...
Walifuatilia jina langu; wakaangalia na sura yangu eti waka-rule out kuwa mimi si raia wa tanzania! Wengi wamepata kashi kashi
hizi hapa mjini na maeneo mengine kama arusha, kigoma, kagera, musoma, mwanza, n.k
wakaniuliza maswali mengi likiwemo hili la kustaajabisha kidogo... Kuwa "babu mzaa baba yangu au bibi mzaa mama yangu aliingia
lini nchini tanzania...???" maswali ya kipuuzi nami niliwajibu kipuuzi "sijuhi kwa sababu sikuwepo kuthibitisha kama ni kweli walitoka
sehemu nyingine kuingia nchini tanzania ama la"
lakini nami nikawauliza sheria inasemaje kuhusu uraia? - maelezo niliyopewa hayakuridhisha na ni kiri tu kuwa wale jamaa
wanaoweka pale ni weupe sana kichwani!
Nikauliza tena swali: Nani ni mtanzania? Je kama tukianza kuwafuatilia watu kwa asili ya majina yao na maeneo tunayohisi historia
ndiko ilikoanzia kuna watu watakuwa watanzania kweli?
Jamani maudhi ya operesheni hii ni mengi sana usiombe yakufikie! Ni waase tu wale wenye majina yenye asili ya nchi kama kenya,
sudani kusini, congo drc, uganda, rwanda, burundi, n.k kamwe usitembee bila vitambulisho vyako - birth certificate, voter id, n.k.
Zoezi hili linaweza kuwa na nia njema kabisa lakini waliopewa kulisimamia na mbinu wazazotumia zitatuachia nyufa nyingi sana na
uhasama mkubwa sana na majirani zetu! Lakini pia unabaki unajiuliza maswali mengi bila majibu.
Ina maana hapa nchini usalama wa taifa hawajui majukumu yao?
Mbona zoezi hili ni kwa baadhi ya watu tu tena waafrika wenzetu?
Mbona zoezi linazingatia majina ya watu na muonekano wa sura zao tu?
Je, ni halali kwa waendesha operesheni kukamata/kugawana mali za watuhumiwa?
Je, taratibu za kidiplomasia zinaelekeza hivi au hizi ni hasira dhidi ya kenya, rwanda na uganda?
jidodo jaribu kutumia busara na kama hauna kakope tafadhari. Unatia aibu tu kwa JF pamoja na Taifa. Huyu jamaa ana issue!
jambo ninaloshangaa raia wa uganda,rwanda na kenya wakishikwa wanarudishwa kwao fasta,lakin raia wa malawi walioambiwa wakajiandikishe wapewe vibali vya kuishi.kwa nini raia wengine wasisingeambiwa hivo.
mimi naona kuna aina fulani ya kulipizana kisasi na jirani zetu wa afrika mashariki,pia walioshikwa wengi ni black wakat kuna wahindi,waarabu kibao,hawana vibali harafu kamanda anajidai kusema tumeshika na wahindi 2,ili ionekane kuna raia wengine pia.
na ata majirani zetu washausoma mchezo ndio maana wameanzisha umoja wao,na watatekeleza kwa vitendo waliyokubaliana ili watuache kwenye mataa.
sisi tutakalia na uchadema,uccm,unga etc
Zoezi hili ni zuri lakini jinsi linavyofanyika sivyo kabisa.Watu wanachukuliwa kwa kuhisiwa wahamiaji haramu(sijui haramu kwa nani), wakibainika kuwa siyo wahamiaji haramu wanageuziwa kibao kuwa wanahisiwa kufanya biashara haramu.. Wananchi wananyanyaswa, wanadhalilishwa katika nchi yao na hii inatokea Dar es salaam sijui mikoani itakuwaje.Hapo kuna issue gani wakati serikali inatimiza wajibu wake? au nawe mhamiaji haramu? kama mtu alichukuliwa kwa mahojiano akaonyesha vilelezo kisha akaachiwa kuna ubaya gani? kwanza huyo jamaa si ndiyo yule aliyeleta thread ya kuichafua Tanzania katika sakata la Immigration JNIA Airport?
Hapo kuna issue gani wakati serikali inatimiza wajibu wake? au nawe mhamiaji haramu? kama mtu alichukuliwa kwa mahojiano akaonyesha vilelezo kisha akaachiwa kuna ubaya gani? kwanza huyo jamaa si ndiyo yule aliyeleta thread ya kuichafua Tanzania katika sakata la Immigration JNIA Airport?
Kama kawaida Tunafukuza WAO natujue na WETU watafukuzwa !! WaTanzania wengi wapo nchi za nje na nchi jirani wakiendesha maisha yao ya kila siku kama kawaida. Sasa zoezi hili la kutimua uhamiaji haramu linapowakumba Wakenya au waGanda, nk; Basi na wa Tz. wetu hawatasalimika nasi tutafukuzwa hii ndo sheria ya kisiasa zisizo na nidhamu. Tujipangee na kutayarisha kambi za kupokea wananchi wetu kutoka nje !! Hayo nisemayo yasiwashtue lakini Ukweli tuige nchi zilizoendelea km: USA, CANDA,AUSTRALIA,EUROPE na nyingi hizi nchi hadi hii leo hupokea wageni wengi kila leo (walokuwa wahamiaji haramu au halali) na wote hao wanatosha kutokana na kuwajibika kikazi na kutoa huduma za aina tofauti....! Nchi hizo zinajengeka na kujengwa na watu wa VICHWA mbali mbali na ufumbuzi wenye maarifa katika zsekta nyingi. imedhirika kuwa maendeleo na uchumi Unakuja kwa njia ya mashindano na kuchuana kikazi kati ya wakazi....!
Sisi kama tumeshindwa kujua basi tungoje hadi tutakapoamka au kuzinduka.!!!!
God bless CLEAN HEARTs and OPEN minds.
Mkuu Muta', kila heshima juu yako, Ahsante mh. Mwenzangu unaupeo na busara aminika, Hawa wajamaa zetu Sijui niwaite jina gani la myama ( WANYAMA WETU ) hawanaga mpango na hawana UTU na wamefilisika damu na kutokuwa na MOYO wa kibinaadamu !! Na bado sijui niwaeke daraja gani humu duniani!! Hadi sasa ninaomba kwa mungu asituletee jangaa hilo na atuepushe na BALAA la aina yeyote katika nchi hii TANZANIA huwaga nina salii sana kuliombea Taifa letu liwe lenye amani na usalama.... hayo Kwa maana nyingi tunawjua VIONGOZI, WANASIASA na WAHUSIKA na WATETEZI, nk Wa nchi hii walivyo Bila kuambiwa, wawezaona Makovu yetu na Majeraha tulonayo !!'Wasiwasi wangu ni uwezo na utayari wa kuwapokea. Tuliwafukuza wahamiaji haramu' ktk hali ya ugafura sana:-tulisikia Rwnd wakilalamika kuwa hawakupewa taarifa...lakini wakaonesha mapokezi makubwa na ya kujari.. wakatoa na usafiri wakupeleka watu wao; walipoombwa magari 50 wakatoa mabasi 100..
Wakifukuzwa wakwetu, tutaweza?...rushwa, umaskini, upendeleo wakupeana tenda....refer matukio ya mabomu ya mbagara na mafuriko jangwani....nasubili comment za ' wazalendo' hapa.
Tanzania tunawahitaji sana walimu toka nje lakini wanatakiwa wawepo nchini kisheria, na hawawezi kufukuzwa iwapo wana vibali halali. Ila inawezekana aukwan wazaramo hawawez kuwa wahamiaj haram?.........sion sababu ya kuwafukuza walimu kutoka nje ya nchi maana wanawaelimisha vijana wetu tena wapo na vibali..
Zoezi ni zuri kama unavyosema lakini palipo na wengi hapakosi dosari na hasa ukizingatia linafanywa na vyombo mchanganyiko lakini mwisho wa yote faida yake ni kubwa kuliko hasara yake.Zoezi hili ni zuri lakini jinsi linavyofanyika sivyo kabisa.Watu wanachukuliwa kwa kuhisiwa wahamiaji haramu(sijui haramu kwa nani), wakibainika kuwa siyo wahamiaji haramu wanageuziwa kibao kuwa wanahisiwa kufanya biashara haramu.. Wananchi wananyanyaswa, wanadhalilishwa katika nchi yao na hii inatokea Dar es salaam sijui mikoani itakuwaje.
Inaonekana kama nia ya zoezi ni ukamataji zaidi kuliko kuonyesha vielelezo. Tunapoelekea sipo kabisa..
Usione rahisi kusema mtu anachukuliwa kwa mahojiano lakini maana yake ni nyingine kabisa.Watu wanalala lupango hadi siku mbili ili tu kuonyesha vielelezo wakati wana vielelezo vyote na ni raia halali..
With high RESPECT mkuu, umeongea kwa hekima na busara " yaonekana Serikali haykulisoma na kulitafakari jambo hili "Tatizo watu wame vamia operesheni kichwa kichwa bila kujiandaa,
Ni sawa na daktari kwenda kumfanyia operesheni mgonjwa bila kuandaa visu, taa wala dawa ya usingizi,
Matokeo yake anamweka mgonjwa kwa operating table na kumsafisha halafu anaanza kuhaha
Kwengine ukionyesha kitambulisho cha uraia au passport au hata driving licence tu mchezo kwisha..kama wewe ni permanent resident, raia au haramu itajulikana , lakini hapa sisi loop holes kila pahala, na pesa za vitambulisho vya uraia zimegugunwa na panya
Labda sasa tuweke historians na anthropologists etc pale immigration watusaidie