life is Short,
..kinachoendelea hapa Tanzania ni tofauti na USA.
..Latinos wanafanya kazi ambazo wazawa wa Kimarekani hawazitaki.
..Huwezi kumtumikisha mzawa Mmarekani ktk ujira na mazingira wanayotumikishwa Latinos.
..Latinos wangekuwa wanaingilia zile shughuli ambazo wazawa wanazitaka ungesikia kurupushani ambayo ingetokea.
..kwa hapa Tanzania wahamiaji haramu wanagombea resources na wazawa. kwa mfano kuna wanaoingiza mifugo yao na kuharibu mazao ya raia wa Tanzania. wengine wamevamia maeneo ya misitu na kuharibu mazingira. zaidi kuna tatizo la ujambazi wa kutumia silaha za kivita ambazo inatuhumiwa wanaingia nazo toka huko walikotoka.
..kwa kifupi ni kwamba wahamiaji haramu wanaishi kibabe huku wakikanyaga haki za raia. imefika mahali raia wa Tanzania wanaishi ktk mazingira magumu as if wao ndiyo wakimbizi.
..kwa kifupi ni kwamba wahamiaji haramu hapa bongo wanabomoa badala ya kujenga nchi.
..siyo kweli kwamba wabongo wote wanataka high life and free lunch. majority ya wa-Tanzania wako vijijini na wanachapa kazi kwelikweli. hujasikia wananchi wanalalamika jinsi wanavyopunjwa ktk bei za pamba, kahawa, korosho, etc etc.