Mauaji ya visasi

Mauaji ya visasi

20221004_050150.jpg
 
u
Mauaji ya visasi (kulipa kisasi) ni dhambi ya tatu kuzaliwa duniani
Dhambi ya kwanza ngono na usaliti pale Eden, lakini hii ina mazonge mengi kwakuwa uongo na kutotii maagizo vyote vinaingia hapo! Ni dhambi yenye vipengele A, B C na D

Dhambi ya tatu ni mauaji, ambayo asili yake ni choyo na wivu, pale Kaini alipofanya uchoyo wa kutoa sadaka iliyonona na matokeo yake ikakataliwa.. Ya mdogo wake Abel ilipokelewa na ndipo roho ya chuki ilipomuingia Kaini na kuamua kumuua mdogo wake kwa mama. Adam hakuwa babayake wa damu.

Tangu hapo mkeka wa mauaji ya visasi uliasisiwa ulimwenguni.. Tangia hapo maelfu kwa maelfu wameuawa kwa mauaji ya visasi. Nimekisoma kisa cha kijana wa Songwe aliyeuwawa mbele ya mkewe na mwanae na wauaji wakaondoka bila kuchukua chochote! Visa hivi ni vingi mno na nitasimulia baadhi kadiri ya kumbukumbu zangu, nakukaribisha nawe uungane nami kama kuna chako unakikumbuka!

Maisha haya hutukutanisha na wengi lakini pia na mengi, kuna watu kwa sababu zozote zile wanajiona ya kwamba wao ndio wao na wengine si kitu.

Wao ndio wanastahili kupata
Wao ndio wanastahili maisha mazuri
Wao ndio wanaijua pesa kuliko wengine
Wao ndio wanastahili maisha na vitu vizuri kuliko wengine

Visa hivi vya mauaji ya visasi vina asili moja! Wauaji hawachukui chochote! Visa hivi vyanzo vyake ni
Usaliti wa kibiashara/dili
Usaliti kwenye mapenzi/mahusiano
Harakati za kisiasa na madaraka
Wivu wa maendeleo/kupata kwa wengine
Dhuluma
Utemi
Ubabe nk nk
Kwenye hili kuna wauaji wa kukodi ama baadhi hutekeleza mauaji wenyewe tena kwa taarifa kabla ya kutekeleza mauaji.

Sometimes kwenye haya mambo ukishindwa kusamehe lipa kisasi! Haikuongezei kitu lakini inakupunguzia maumivu! Ila usiijaribu hii njia imejaa mabaya!

Mnamkumbuka yule traffic aliyeuliwa kwa risasi pale sayansi ? Jamaa alikuja na boda akamuuliza Afande unanikumbuka? Jamaa akajibu ndio.

Jibu hilo lilitosha kummininia risasi zilizoondoka na uhai wake
Nitakuja na visa vingine.
menichanganja mkuu,ebu nivavadulie kidogo hapo,si kwamba nakubishia hapana,kwani elimu ni bahari,kumbe abel hakua mtoto wa adam ya adam,imekaaje hapa,manake tunaambiwa MUNGU alimuumba adam na hawa pekee na watoto wao ndio hao,sasa huyo kidume aliyejifanya kumnanii mke wa adam kama yaliyomtokea masanja alitokea wapi?...nifafanule mkuu kwani natamnua kuna vitabu vimefichwa kama kitabu cha enock,,,,lete uzi mazee
 
u

menichanganja mkuu,ebu nivavadulie kidogo hapo,si kwamba nakubishia hapana,kwani elimu ni bahari,kumbe abel hakua mtoto wa adam ya adam,imekaaje hapa,manake tunaambiwa MUNGU alimuumba adam na hawa pekee na watoto wao ndio hao,sasa huyo kidume aliyejifanya kumnanii mke wa adam kama yaliyomtokea masanja alitokea wapi?...nifafanule mkuu kwani natamnua kuna vitabu vimefichwa kama kitabu cha enock,,,,lete uzi mazee
Ni simulizi nyinginezo kwamba siku bibi Eva anakula tunda kilinasia halafu baby Adam akaweka nakshi tuu
 
Mwanafunzi wa shule ya msingi Mtumba, Farida Makuya (16) aliyetarajia kuanza mtihani wa darasa la Saba leo, ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani nyumbani kwao Mtumba Jijini Dodoma na watu wasiojulikana huku watu hao wakitokomea bila kuchukua kitu chochote
 
Kuchapiwa ni siri ya ndani na ilianzia pale Eden.. Wewe unadhani baada ya Eva kuongopewa na ibilisi(nyoka) na kula 'tunda' la mti wa kati alitoka salama? Adam alikula makombo tuuu...
Kaini ni uzao wa ibilisi na ndio maana hakuona umuhimu wa kutoa sadaka nzuri..
Nimeongeza kitu hapa respect kwako mshana.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Nina visa viwili na kupitia visa hivi vimenifunza kuheshimu makubaliano na mtu/watu au kutokutoa ahadi bila kuitafakari!!!

Cha kwanza
ni 2004:jamaa alikuwa ni rafiki yake binamu yangu mkubwa sasa kutokana na mara nyingi kuwa naongozana na huyu binamu yangu (R.I.P) nikajikuta huyu jamaa nimekuwa nyoka wake,ilikuwa kawaida kupewa million mbili peleka kwa fulani nenda pale chukua hela kadhaa niletee so automatically nikajikuta nimeingia kwenye circle ya watu wake,imeenda hivyo sasa siku moja akanipa Tsh 700,000/=  akaniambia wapelekee fulani!

Jamaa walikuwa watu wa deal za sigara dk kama 17 baada ya kuachana nae nikiwa ndani ya Ki-Hiace akani-text rudi kufika pale nilipomuacha nikamkuta anaongea na simu kama wanatukanana na anayeongea upande wa pili siku tatu mbele wakamvamia jamaa kwake Mbezi Kibanda Cha Mkaa usiku wa saa mbili mbele ya mkewe,alivyotuhadithia mkewe jamaa alimtuma akachukue kwenye draw 3mill cash wamuache wakasema wao hawakutumwa pesa wakammaliza,alipigwa risasi moja makalioni nyengine shingoni kwa nyuma kwenye pingili za mgongo na shingo akafa on the spot na hawakuchukua chochote.

Kwa sababu nilishakuwa na muunganiko na jamaa zake kadiri siku zilivyoenda wakawa wananifungulia codes kwamba alipewa dili Canter imejaa sigara za mazabe akapatana bei kwanza kwa kufika hela ndogo kisha akawaambia wapeleke mzigo wakiwa njiani akawakamatisha jamaa kwa askari then akazunguka upande wa pili kwamba yeye atamalizana na hao askari so wao wachukue sikumbuki bei but haikufika 2mill jamaa wakakubali but still akaiona ni nyingi akawapunguza tena hata walipokubali akawa pesa hawapi na mzigo askari mwenye file hanyooshi maelezo wakaja kutonywa na askari mwengine kwamba mzigo jamaa alishachukua na hata haukufika hapo kituoni.

Cha pili:mwaka 2017,huyu nae tulikutana kimjini mjini alikuwa mtu wa kupokea bond za magari (wenyewe wanaita hela za moto) Ila yeye alikuwa mtu akiacha gari bond anachonga funguo ya ziada siku mwenye nayo akiigomboa hakai nayo mwezi inapotea akajichanganya akakopesha watu wanaojuana bila yeye kujua akawapiga tukio wakaunga dots walimmalizia bar kaenda msalani kukojoa jamaa wakamfata huko huko wakammaliza.

Muhimu sana kuzingatia makubaliano au ahadi tunazowapa wenzetu.
Kweli mkuu makubaliano yafatwe.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mtani soma hii

Siku moja Kaini na Abeli walimtolea Yehova dhabihu. Je, unajua dhabihu ni nini? Ni zawadi ya pekee. Yehova alifurahishwa na dhabihu ya Abeli, lakini alichukizwa na dhabihu ya Kaini. Jambo hilo lilimkasirisha sana Kaini. Yehova alimwonya Kaini kwamba hasira ingeweza kusababisha afanye jambo baya. Hata hivyo, Kaini hakusikiliza.

Badala yake Kaini alimwambia Abeli hivi: ‘Twende shambani.’ Walipokuwa peke yao shambani, Kaini alimshambulia ndugu yake na kumuua. Yehova alifanya nini? Yehova alimwadhibu Kaini kwa kumfukuza aende mbali na familia yao. Kaini hakuruhusiwa kurudi tena nyumbani.
Bado nasubiri kuona ni wapi pamesema dhabihu ni mwanamke Kaini na Abel walikuwa wanagombea sijapoana....
 
Kuchapiwa ni siri ya ndani na ilianzia pale Eden.. Wewe unadhani baada ya Eva kuongopewa na ibilisi(nyoka) na kula 'tunda' la mti wa kati alitoka salama? Adam alikula makombo tuuu...
Kaini ni uzao wa ibilisi na ndio maana hakuona umuhimu wa kutoa sadaka nzuri..
Uongo, uongo, uongo, uongooooo
 
Ila Kuna watu makatili Jamani..uondoe uhai wa mtu kisa Mali/mapenzi/sijui vitu gani gani...kuua hapana Jamani...ukizingua kisasi nitalipa kinamna nyingine lakini sio kuua Jamani..watuuu
Unamoyo kama wangu aisee
 
Mkuu; Tunda lilozungumzwa kwenye Bilblia sio "Tunda" tunaloshabikia kuliwa kimasihara.
Ingekuwa ni hilo, Mbona ilishatolewa ruhusa tangu awali kwa maneno: Nendeni mkazae (Adam; Me na Eva/Hawa;Ke )na kuitiisha/mkaijaze nchi(.Mw.1:28) Je, wangezaanaje kama sio kwa kujamiiana?
Tunda hapo ni Kukosa Utii i.e. Unaambia au unaAmriwa usifanye hiki we unapuuzia na unafanya(Umeasi maagizo) kwa hiyo wewe sio Mtiifu.
Umemjibu vema kabisa
 
Back
Top Bottom