Dada mimi nimekaa Amerika kwa jumla ya miaka minne hivi. Na Zuri zaidi nilikuwa nakaa hapo hapo Orlando, Florida kwa kipindi fulani.
Ubaguzi wa rangi bado upo sana kule, ingawa umejificha katika tabasamu nyingi unazoweza kukutana nazo usijue. Wanazo preconceived notion kuwa mtu mweusi yupo hivi, na huwa hawataki kuamini kuwa mtu mweusi anaweza kuwa tofauti na notion walizo nazo: Ukuwa kule wewe ni mjinga tu, hata kama unapata A na B darasani, wewe ni ombaomba tu, hata kama una kazi, wewe ni mshamba tu, hata kama umekaa huko miaka mingi. Na sababu ya hayo yote huwa ni rangi ya ngozi yako. Mkitoka leo na mtoto wa kizungu kutafuta kazi, hata kama wote ni wageni pale, mzungu atapata kazi kwanza. Na wewe utakapopata hiyo kazi, mshahara wako utakuwa chini kuliko wa yule mgeni mwenzako mzungu.
Siku moja mzungu aliniletea makombo ya chakula kwa kuamini kuwa sikuwa na chakula pale niliishi nikatupa. Na usiombe vijana wanaume wa kizungu wakakuona unapendwa na binti mzungu mwenzao. Hasira na chuki huwa inapanda zaidi kuliko kabla ya hilo kujilikana. Namejiuliza sana kama huyo kijana aliyeuawa hakuwa na girlfriend mzungu. Huchukui muda ukijifanya kupendwapendwa na wasichana wazungu--hasa katika majimbo ya Deep South, yaani Florida, South Carolina, Texas, na majimbo mengine ya kusini.
Ubaguzi upo sana America. Nimeona mwenyewe. Sijasimuliwa.