Mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA Arusha: Watuhumiwa watoroka mahakamani mbele ya polisi!

Suala la Msingi la kujiuliza hapa ni hawa Askari walikuwa wangapi?; kama alikuwa peke ake basi ni tatizo kwani ni vigumu sana kumlinda binadamu mwenzako tena mwenye akili timamu tena yawezekana hata kukuzidi wewe umlindaye.

Wafungwa wapo wa makosa mbalimbali hivyo yawezekana pia wafungwa hao nao wapo trained hivyo waliweza kumzidi ujanja huyu Askari, kwani tunajua kuwa Shari ya aina yoyote ili uishinde yahitaji timing tu.

Hivyo nachelea kusema kuwa ni uzembe au sio uzembe"
 
Daudi Balali ametoroshwa kwa style ya kufa akiwa hai so na hawa utasikia wame uwawa na policcm walivyokua wana rushiana risasi!Ila ukweli wapo hai na viroba wana kunywa!Tukisema hili ni jeshi la policcm wata kataa???Hivi wale wanajeshi walio mpa siku 100 dhaifu wako wapi mbina hatuwasomi au ilikua nguvu ya soda???Pambav kabisa policcm aaaah!!!

Mkuu, unaona mbali!
 
wametoroka chini ya mikononi mwa polisi? au wametoroshwa na polisi?

Intelijensia alikuwa wapi? Hawakuwa na kitu kizito cha kuwapiga nacho? au mke wa chagonja kawaingiza usalama wa Taifa?


Very intereting!
Kwa jinsi ninavyojua, watuhumiwa wa mauaji wanapelekwa au kurudishwa wanapaswa kuwa kwenye Pingu njiani kote wakisindikizwa na askari mwenye bunduki.
Maswali ya kujiuliza.
Hawakuwa na Pingu?
Pingu zilikatika wakapata mawazo ya kumnyang'anya askari Bunduki na kuondoka nayo?
Je,kwa nini ihusishe watuhumiwa wote wawili wa mauaji ya kiongozi wa Chadema? Na si zaidi wala pungufu ya hapo?
Je, tukio hilo ni la ngapi ndani ya miaka 10 iliyopita?
Sina imani na jeshi hilo.

 
Acha kutueleza mambo ya mwaka 47 uzembe wa polisi? kwani aliyekuwa na SMG ni askali mmoja tu? ebu tuambie kwa nini polisi wengine hawakuchukua hatua? na kwa nini watoroke hao watuhumiwa muhimu wa kesi kwa hiyo wasipopatikana si ndo kesi itakuwa imekwisha maana ushahidi umetoroka na kupotezwa[/QUOmTE]

kibogo mimi sikuletei mambo ya mwaka 47, najua ukweli polisi ni wazembe sana + wapenda rushwa. Kwa mantiki hiyo huyo Ramadhan Shaban na mwenzake kwa kuwa ni watuhumiwa wazoefu bila ya shaka wamehonga hao polisi au kama nilivyokuambia uzembe wao polisi tu.
 
Very intereting!
Kwa jinsi ninavyojua, watuhumiwa wa mauaji wanapelekwa au kurudishwa wanapaswa kuwa kwenye Pingu njiani kote wakisindikizwa na askari mwenye bunduki.
Maswali ya kujiuliza.
Hawakuwa na Pingu?
Pingu zilikatika wakapata mawazo ya kumnyang'anya askari Bunduki na kuondoka nayo?
Je,kwa nini ihusishe watuhumiwa wote wawili wa mauaji ya kiongozi wa Chadema? Na si zaidi wala pungufu ya hapo?
Je, tukio hilo ni la ngapi ndani ya miaka 10 iliyopita?
Sina imani na jeshi hilo.


Mkuu nikujuze kwa usahihi zaidi.

Siyo watuhumiwa wote wa mauaji wanapelekwa na pingu mkononi. Wengi wa watuhumiwa wanaopelekwa na pingu mkononi ni wale ambao walishahukumiwa na utakutawengi wapo na askari Magereza ambao kidogo wanaonyesha wapo makini kuliko hawa ndugu zetu wa polisi.

Kinachofanyika kwa mahabusu hao, ni kuwa siku ya kesi wanachukuliwa na mahabusu wengine kama kawaida hawafungwi pingu wala nini mpaka mahakamani kisha wanawekwa lock up mpaka muda wa kusikiliza kesi zao na baadae kurudishwa tena lock up tayari kurudi gerezani via karandinga.

Labda ikitokea mtuhumiwa arijaribu kutoroka kisha akashindwa ndiyo anaweza kufungwa hizo pingu na kuangaliwa kwa umakini sana.

Binafsi naamini kama polisi hawajavuta mkwanja ni uzembe uliopelekea hali ile.
 
Ki ukweli polisi tushawazoea. Hii kauli waliozoea kutumia ya kutii sheria bila shuruti wanafika mahali na kujisahau kuwa hata wakifanya tukio gani mwisho wa siku wa kulaumiwa ni raia!
 
hadi sasa RCO wa arusha bado yuko madarakani au keshastaafu?
kufumbiana macho katika masuala kama haya ni hatari
who knows mtuhumiwa akaenda kuiangamiza kabisa familia ya marehemu?
Mwema anafanya mchezo, cheo kimemshinda.
 
Binafsi naamini ni uzembe wa polisi waliokuwa mahakamani leo ndiyo imepelekea hali hii.

Kwa hili Sio uzembe... kwanini iwe wawili wale wale waliokubali kosa!!!!!! JMTi ya CCiM ina mambo khaaa!
Kesi mwishowe itakuwa hakuna ushahidi wa kutosha hivyo watuhumiwa waliobaki wanaachiwa huru....damu ya binadamu mwenzetu inatulilia, Mungu tupe hekima!
 
ngumu kumesa, kweli think tank ya serikali ya CCM iko empty, unakuja na upuuzi kama huu eti wamempiga kumbo askari wakala kona, ni mjinga gani unaweza kumuaminisha huu upuuzi. Igeni hata kwa illuminati walitengeneza tukio la 9 11, wakampakazia Osama mpaka leo wajinga wote duniani ambao ndo majority wanaamini hivyo.
 
Mahabusu wawili kati ya sita ambao ni watuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa CDM tawi la USA Arusha wametoroka leo mchana mahamani.

Mahabusu hao wawili ni watuhumiwa wakuu wa mauaji maana katika maelezo yao ya awali walikiri jinsi walivyojishirikisha na mauaji ya marehemu. Itakumbukwa kuna uzi ulishahi kuanzishwa juu ya watuhumiwa wa mauaji ya mwenyekiti CDM wa USA kukamatwa kwa mganga wa kienyeji Sindiga, sasa baadhi ya watuhumiwa hao ndiyo waliotoroka.

Taarifa za awali zinasema walifanikiwa kupora na bunduki moja ambayo baadae waliitelekeza.

MoDs usfute uzi huu, taarifa hizi hazina shaka kabisa kwa mujibu wa chanzo changu makini kilichopo huko Arusha.


Inaonekana mods kuna aina ya malalamiko ya threads kufutwa bila sababu za msingi. Kwa nini kila wakati tunasoma wana JF wanawasihi msifute threads? Inabidi mjiulize kama mna walakini katika ku-moderate
 
Inaonekana mods kuna aina ya malalamiko ya threads kufutwa bila sababu za msingi. Kwa nini kila wakati tunasoma wana JF wanawasihi msifute threads? Inabidi mjiulize kama mna walakini katika ku-moderate

Malalamiko hayo yapo, hasa kwa issue ambazo zinahitaji uthibitisho au kubwa kitaifa. Ikiwa hivyo inabidi mleta uzi uandike kitu ambacho una uhakika nacho kulingana na chanzo chako ili ueleweke na uzi wako ukae vinginevyo MoDs hawapendi majungu.
 
Back
Top Bottom