Mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA Arusha: Watuhumiwa watoroka mahakamani mbele ya polisi!

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,071
Vyanzo zaidi vimeweza kutupatia ukweli wa hasa kilichojiri leo mahakamani pale Arusha.

Watuhumiwa wawili wa mauaji ya Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Usa River, Msafiri Mbwambo, aliyechinjwa kwa kitu kikali mithili ya msumeno, wametoroka mahakamani leo Arusha, mbele ya askari polisi. Itakumbukwa hii kesi inahusisha viongozi aw CCM.

Kama kuonesha kuwa video ya mpango huo isingenoga sana, watuhumiwa hao inasemekana wamemnyang'anya bunduki mmoja wa askari kati ya wengi waliokuwa wakiwalinda. According to the source, Askari waliokuwepo wakishuhudia saga hiyo, wakanogesha zaidi picha kwa kutochukua hatua yoyote, achilia mbali kulinda mali ya jeshi na serikali, hawakumsaidia hata mwenzao wakati anashambuliwa, kunyang'anywa bunduki na kuchaniwa nguo zake, call them uniform.

If that not enough to end the show, bunduki hiyo, according to source, iliokotwa muda mfupi baade ikiwa imetelekezwa. Another game in the making. Wanafikiri wananchi wrote wamelewa banana.

MORE INFO

And the beat if not the show goes on...baadhi ya maaskari waliokuwa 'lindo' wanashikiliwa polisi. Kesho kuna mahafali/shughuli pale CCP, kwa hiyo wakubwa pia wa hawa jamaa wako kwenye mji wa utalii.
 
Mahabusu wawili kati ya sita ambao ni watuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa CDM tawi la USA Arusha wametoroka leo mchana mahamani.

Mahabusu hao wawili ni watuhumiwa wakuu wa mauaji maana katika maelezo yao ya awali walikiri jinsi walivyojishirikisha na mauaji ya marehemu. Itakumbukwa kuna uzi ulishahi kuanzishwa juu ya watuhumiwa wa mauaji ya mwenyekiti CDM wa USA kukamatwa kwa mganga wa kienyeji Sindiga, sasa baadhi ya watuhumiwa hao ndiyo waliotoroka.

Taarifa za awali zinasema walifanikiwa kupora na bunduki moja ambayo baadae waliitelekeza.

MoDs usfute uzi huu, taarifa hizi hazina shaka kabisa kwa mujibu wa chanzo changu makini kilichopo huko Arusha.
 
Huu ni mchezo hapa unachezwa bana

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Duh wamejipanga kweli aiseee so wamekubali then wanapotea

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hivi unafahamu kwamba wewe ni msemaji wa Chama? sasa haya mambo ya tetesi na nafasi yako wapi na wapi? Najuwa fika hili swala linaweza kuwa limetokea ila huoni kuwa kama mseamaji rasmi wa Chama unapaswa kuongea fact?

Hivi Salva Rweyemamu naye atuletee thread ya tetesi hapa JF unategemea tutamnyamazia kimya? No way thread zingine waache waanzishe watu wengine na siyo wewe, ninapoona jina lako nategemea fact tu na siyo tetesi.
 
Kama ni kweli hii habari, basi wategemee wananchi kujichukulia maamuzi yao kwa wahalifu baada ya kupoteza imani na vyombo vyetu vya usalama.
 
Hivi unafahamu kwamba wewe ni msemaji wa Chama? sasa haya mambo ya tetesi na nafasi yako wapi na wapi? Najuwa fika hili swala linaweza kuwa limetokea ila huoni kuwa kama mseamaji rasmi wa Chama unapaswa kuongea fact?

Hivi Salva Rweyemamu naye atuletee thread ya tetesi hapa JF unategemea tutamnyamazia kimya? No way thread zingine waache waanzishe watu wengine na siyo wewe, ninapoona jina lako nategemea fact tu na siyo tetesi.

Kweli mkuu Matola akiwa msemaji wa chama Tumaini Makene hastahili kuandika habari za tetesi, isipokuwa facts otherwise anakuwa anajiweka katika nafasi mbaya ya kuendelea kuwa reliable source of information/news.

Tafdhali makene jaribu kutumia njia zote unzoweza kuthibitisha habari hii.
 
Last edited by a moderator:
wametoroka chini ya mikononi mwa polisi? au wametoroshwa na polisi?

Intelijensia alikuwa wapi? Hawakuwa na kitu kizito cha kuwapiga nacho? au mke wa chagonja kawaingiza usalama wa Taifa?

Wametoroshwa na policcm,Na believe or not lazma kuna kigogo wa ccm anahusika kwenye mauaji hayo.
 
Hivi unafahamu kwamba wewe ni msemaji wa Chama? sasa haya mambo ya tetesi na nafasi yako wapi na wapi? Najuwa fika hili swala linaweza kuwa limetokea ila huoni kuwa kama mseamaji rasmi wa Chama unapaswa kuongea fact?

Hivi Salva Rweyemamu naye atuletee thread ya tetesi hapa JF unategemea tutamnyamazia kimya? No way thread zingine waache waanzishe watu wengine na siyo wewe, ninapoona jina lako nategemea fact tu na siyo tetesi.

Mkuu Matola unataka kumfundisha jamaa awe na id nyingine ya kuanzisha tetesi hahaaaaaaa!
anyway, nilikuwa pale central police nikawa nasikia stori za namna hiyo, ila sikutilia maanani sikujua imetokea wapi maana nilikuwa nimeconcentrate kwenye mambo yangu.
kama ni kweli huu ni unyama wa hali ya juu, na msishangae na muuaji wa Daudi Mwangosi naye akatoroka kwa staili hiyo hiyo kupoteza ushahidi!
 
Last edited by a moderator:
Huyo wememtorosha ili akaunganishwe kwenye ili deal ya kuwaua viongozi wakuu wa Chadema. kwa ule ukatili aliofanya lazima wampe kazi kwenye mtandao wao
 
Back
Top Bottom