Mauaji ya Kanisani, jina la Katekista latajwa, AKIMBIA, asakwa na Polisi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Kufuatia mauaji ya Nickson Myamba ambaye alikuwa ni Katibu wa Baraza la Walei Kigango cha Makambako, Jimbo la Njombe, Februari 7, 2022 kisha kudaiwa mwili wake kutenganishwa kichwa na kiwiliwili, bado kuna hali ya sintofahamu kuhusu tukio hilo.

Tayari Jeshi la Polisi la Njombe kupitia kwa RPC wa mkoa huo, Khamisi Issa limetoa tamko kuwa upelelezi unaendelea na tayari kuwa watu kadhaa wameshikiliwa.

Kuna ujumbe umesambaa kwenye baadhi ya magroup ya viongozi na waumini wa kanisa hilo (Njombe) juu ya kukimbia kwa Katekista ambaye alikuwepo eneo la tukio siku husika.

Kuna ujumbe huu umetumwa na muumini mmoja mtandaoni akiwasihi wenzake kuwa makini kisha picha ya huyo Katekista anayedaiwa kukimbia ikisambaa pia.

Ujumbe wenyewe ni huu chini na picha ya huyo Katekista ipo hapo imeambatanishwa na stori hii,,,,,,,:::

..................

JUU YA MAUAJI YALIYOTOKEA MISHENI YETU MAKAMBAKO

Tarehe 8 Februari nilikuwa safarini kuelekea Iringa ndipo nilipopitia makambako kuacha mzigi.

Kufika getini hakuna MTU anaruhusiwa kuingia ndani ya Parokia kwa sababu naambiwa yametokea mauaji parokiani, na paroko pamoja na viongozi walikuwa kituo cha polisi Kwa mahojiano...

Nikapewa taarifa za mauaji ya katibu kama mlivyosikia

Hadi sasa mshukiwa mkuu ambaye ni katekista ametoroka na hajapatikana.

Na polisi wanasema hâta hivyo wapo sehemu nzuri YA kumpata.

Watu hapa Makambako wameshtuka na kujawa butwaa na hofu na huzuni kubwa.

Kwa misheni zetu mauaji na ya kikatili Kama haya hatujapata kuna nayo. Huyu Katekista amekuwa ni kiongozi Wa miaka zaidi YA 20... point of reference YA watu wengi.

Mauaji haya YA kinyama si tuyamefanyika...yamefanyia kwenye eneo la kanisa, ofisi/duka la kanisa...mbaya Zaidi yamehusisha watu ambao ni viongozi.

Kwa maelezo YA paroko siku hiyo ilibidi katekista akabidhi mahesabu ili aweze hudumia duka hilo MTU mwingine full time.

Katibu ndo alikuwa anashughulikia huo mchakato Na siku hiyo ndo ilikuwa siku YA makabidhiano.

Jana jioni imefanyika misa nyumbani Kwa marehemu wakiwemo viongozi wote ngazi YA wilaya.

...............

Mwisho wa kunukuu andiko hilo.
 
Raia wema wakimbilie wapi sasa maana kila sehemu panatisha kanisani kwenyewe wanatenganisha kichwa na kiwiliwili
 
Pope - anaficha uharamia wa Mapadre!

Mapadre - wanalala na masister wa mission

Mapadre - wanalawiti watoto wadogo bila Aibu.

Ndoa - ya jinsia Moja karibu sasa inaruhusiwa

Makambako - wanachinjana sababu ya fedha!

"Wanaitwa watu wa Mungu"
Mkuu, sio kosa lako sababu hayo pekee ndiyo uliyojaaliwa kuyajua juu ya Kanisa Katoliki. Siku ukiijua imani yenyewe halisi na watu wake wanaoiishi hutokuja tena kupost hivi. Mungu ni mwema na humjalia imani thabiti kila amuombaye. Mungu atujalie imani na moyo wa kuwapenda wengine.
 
Back
Top Bottom