Matusi Redioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matusi Redioni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Preta, May 24, 2011.

 1. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 23,993
  Likes Received: 2,715
  Trophy Points: 280
  Leo nilikuwa nasikiliza kipindi cha jahazi Clouds Fm, Kibonde, Kayanda na Wasiwasi walikuwa wanajadili kuhusu kufa kwa ATC, mjadala umeenda vizuri japo Kibonde alikuwa anaonekana mwenye jazba sana.......kilichonishangaza ni pale alipojidai kuwa ana machungu sana na kufikia hatua ya kutoa tusi la nguoni (k****m***m**k**)nadhani watu wazima mmenielewa, Hata wenzie aliokuwa nao niliwasikia wakicheka kichinichini kwa mshtuko walioupata na simu zikipigwa mfululizo,sasa linakuja swala la je....Clouds FM imekuwa ya kihuni namna hii kiasi ambacho imeanza kutoa matusi ya nguoni?
  Nadhani kuna mliokuwa mnasikiliza pia,mtakubaliana na mimi. Kwa kweli ni fedheha.
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,292
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Hii radio bana...haya ngoja tusikie TCRA watasema hawakusikia
   
 3. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 23,097
  Likes Received: 10,415
  Trophy Points: 280
  hiyo redio huwa sisikilizi nowadayz huyo kibonde nilishauliza anapitiaga bar kwanza
  coz ana mambo ya hovyohovyo allah ndo ajuaye na ndo sisikilizi tena :smash::A S thumbs_down:
   
 4. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 23,993
  Likes Received: 2,715
  Trophy Points: 280
  Ni aibu sana, Kusaga asipokuwa makini na huyu mtu redio yake itakosa wasikilizaji, sio sehemu zote ni wabaya lakini ajitahidi kurekebisha pia na kule kwenye kasoro. Kila siku lawama kwa Kibonde haziishi, mimi nilikuwa nasikiliza na nilikuwa namuona ana mapungufu lakini sikuwa nachukulia kihivyo....but leo nimegundua Kibonde ana walakini....nilidhani anasingiziwa
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 36,337
  Likes Received: 14,605
  Trophy Points: 280
  hi ndio clouda fm
   
 6. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,434
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Nilisikiliza lakini bahati mbaya au nzuri nilihama kabla ya hiyo scene, lakini kibonde si kati ya presenters ninaowakubali, akili yangu inaniambia ni mtu wa kujipendekeza kwa watu fulani, mimi husikiliza power breakfast angalau namwona hando anajua anachofanya, akiwa na co wake barbara, namkubali pia PJ wakati wa kuperuzi na kudadis. Bonge naye namuona yuko decent. Huyo kibonde kaeni naye wenyewe.
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  May 24, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 70,387
  Likes Received: 28,171
  Trophy Points: 280
  Mpende msipende, mkubali msikubali Kibonde yuko juu. Nina uhakika kabisa kama Tanzania tungekuwa na mfumo mzuri wa listener ratings basi kipindi cha Jahazi kingekuwa kiko juu sana katika muda wake kinapokuwa hewani (saa kumi mpaka saa moja jioni).

  Kama kweli Kibonde angekuwa mbovu kama ambavyo wachache wenu mnavyotaka watu waamini basi nina uhakika kabisa wasikilizaji wa kipindi hicho wangekuwa wameshapungua tokea zamani.

  Lakini inavyoelekea ni kinyume chake. Ili mtu uweze kujua na kumkasirikia kuwa leo kasema nini ni lazima u tune in kwenye kipindi cha Jahazi. Bila kumsikiliza utajuaje na (kujifanya) kukasirikia kile alichosema?

  Kibonde kaza buti mwana. Uko juu. Simamia kile unachokiamini na usichoke wala kutishika kutoa maoni yako kwani wewe siyo reporter wala news anchor. Wewe ni commentator. Fani ya utangazaji kama commentator inakupa uhuru wa kutoa maoni yako kinyume na ilivyo wasomaji na waandishi wa habari ambao wanatakiwa kuandika na ku report facts.

  Just remember this my brother. Don't let the haters faze you. Make your haters your motivators by becoming the number one hater aggravator in the whole wide world. I got your back son. Keep up the good work.
   
 8. Bollo Yang

  Bollo Yang JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 440
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Acha uongo, hata mimi pia nimesikiliza, hakuna sehem aliyotukana kama unavosema, hata kama angelikua ni mjinga kiasi gani asingeweza kutukana hilo tusi on air, punguza chuki.
   
 9. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 23,993
  Likes Received: 2,715
  Trophy Points: 280
  no no no.....Kibonde simchukii kwa sababu hata nikimchukia simjui, na isitoshe mimi ni mpenzi sana wa kusikiliza Clouds, na inakuwaje leo kwa sababu nimemchukia nije niseme kuwa Kibonde ametukana wakati ni uongo?........
   
 10. Kwamex

  Kwamex JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama kweli katoa hilo tusi, basi hoja kama hii itatokea pia kwenye media nyinginezo, nakuwa mzito kuamini moja kwa moja kama kweli katukana live.
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,221
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Wabongo ndio zetu....mtu akikosolewa/semwa basi HAPENDWI!Yani kila kitu watasema ni chuki....ndo maana hatuendelei!
   
 12. d

  dropingcoco Senior Member

  #12
  May 24, 2011
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  amekutuma uje kumtetea? au ndio wewe mwenyewe kibonde unataka kujisafisha?tumesikiliza jahazi na tumemsikia akitoa tusi, jamaa la hovyo sana lile
   
 13. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2011
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  kwa mujibu wa baadhi ya wachangiaji wa uzi huu, hata humu ndani mna Vibonde kibao ama wapambe wake. poor We!
   
 14. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,106
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ni kweli katukana nimesikia,na wenzake wakacheka sana.
  Naona Preta kanizidi spidi,nilikuwa nataka niweke hii taarifa.
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,602
  Likes Received: 349
  Trophy Points: 180
  Shimo la taka ngumu.
   
 16. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,107
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Hata KIU na magazeti mengine ya udaku yanasomwa na watu wengi kuliko Financial Times. Lakini hiyo haina maana kuwa hayo ni magazeti makini au ni kwa watu makini (japo mtu makini anaweza kuyasoma kwa sababu zake binafsi) kuliko Financial Times. Mwambie Kibonde aandike "article" juu ya maada yeyote ya kijamii (amekuwa kwenye mambo ya habari muda mrefu kwa hiyo anatakiwa awe na uelewa wa kawaida wa mambo yanayoihisu jamii) na aiwakilishe mahali - kwa mfano mdahalo wa kitaifa (achilia mbali wa kimataifa) uone kama itapita awamu ya kwanza ya mchujo.
   
 17. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Radio mawinguuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 18. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,584
  Likes Received: 783
  Trophy Points: 280
  Kibonde nilimsikia kwa maskio yangu akishabikia kulipwa la deni Dowans, akidai sio ishu kwani watanzania mil. 40 tukichanga buku 2 kila kichwa inakaribia kulipa deni, akaja akadai tena madai ya wanaUDSM ya kuongezewa boom hayana msingi kwani wanafunzi wa pale ni walevi, wazinifu na wapenda xtarehe, kwa ujumla ana hulka ya kujipendekeza kwa watawala. Jumlisha na haya ya matusi... Mh?
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  May 24, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 70,387
  Likes Received: 28,171
  Trophy Points: 280
  Anza wewe kuandika hiyo atiko...
   
 20. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 23,993
  Likes Received: 2,715
  Trophy Points: 280
  Inaelekea redio tulizokuwa tunasikiliza ni za mbao na zinamchukia Kibonde
   
Loading...