Preta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 24,320
- 18,875
Leo nilikuwa nasikiliza kipindi cha jahazi Clouds Fm, Kibonde, Kayanda na Wasiwasi walikuwa wanajadili kuhusu kufa kwa ATC, mjadala umeenda vizuri japo Kibonde alikuwa anaonekana mwenye jazba sana.......kilichonishangaza ni pale alipojidai kuwa ana machungu sana na kufikia hatua ya kutoa tusi la nguoni (k****m***m**k**)nadhani watu wazima mmenielewa, Hata wenzie aliokuwa nao niliwasikia wakicheka kichinichini kwa mshtuko walioupata na simu zikipigwa mfululizo,sasa linakuja swala la je....Clouds FM imekuwa ya kihuni namna hii kiasi ambacho imeanza kutoa matusi ya nguoni?
Nadhani kuna mliokuwa mnasikiliza pia,mtakubaliana na mimi. Kwa kweli ni fedheha.
Nadhani kuna mliokuwa mnasikiliza pia,mtakubaliana na mimi. Kwa kweli ni fedheha.