Matumizi ya TEHAMA yawe Kipaumbele cha Utendaji ndani ya Shirika la Posta

Sep 13, 2016
49
23
IMG-20230726-WA0014.jpg


♦️ Akabidhi Vyeti na Tuzo za Pongezi kwa wafanyakazi wa Shirika la Posta walioshiriki kufanikisha Tanzania kupata nafasi ya Ujumbe kwenye Mabaraza ya Umoja wa Posta Duniani (CA &POC).

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ndugu Khadija Khamis Rajab wakati akifungua kikao kazi cha Mameneja wa Makao Makuu na Mikoa Extended Management Meeting pamoja na kikao cha 34 cha Kamati Tendaji ya Baraza Kuu la Wafanyakazi lilioanza vikao vyake vya siku tatu leo tarehe 25 Julai 2023, Jijiji Arusha.

IMG-20230726-WA0013.jpg


"Matumizi ya TEHAMA na masuala ya kidijitali ndani ya Shirika la Posta hayaepukiki kutokana na mabadiliko ya ulimwengu tulionao kwa sasa katika nyanja zote za uchumi, siasa na jamii. Kauli mbiu ya Mkakati wa nane wa Posta inavyosema 'Posta ya Kidijitali kwa Biashara Endelevu' ndiyo mkazo unatakiwa kuwekwa ili kulikuza Shirika hili na kulifanya kuwa bora barani Afrika" alisisitiza Ndg. Khadija.

Aidha, Ndg. Khadija aliwataka wafanyakazi wa Shirika la Posta kutilia mkazo mafunzo mbalimbali yanayotolewa ili yaongeze uwezo, ubunifu na tija katika utendaji kazi ndani ya Shirika huku akiwataka viongozi wa Shirika kujadiliana kwa uhuru na uwazi changamoto za mwaka uliopita wa 2022/2023 na kubaini mikakati ya maboresho ya changamoto hizo kwa mwaka ujao wa 2023/2024.

IMG-20230726-WA0017.jpg


Naye Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania Ndugu Ramadhan Omar Mohamed amelipongeza Shirika la Posta kwa juhudi za kupiga hatua za kidijitali kulingana na Mpango Mkakati wa Nane wa Shirika unaosema Posta ya Kidijitali kwa Biashara Endelevu, huku akimuomba Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ndugu Khadija Rajab kusaidia usimamizi wa ukamilishwaji wa zoezi la Anwani za Makazi Zanzibar ili Shirika la Posta liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Kwa upande wake, Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Macrice Mbodo, ameeleza kuwa kikao hicho kinachofanyika kwa siku tatu, kitatathimi na kujadili utendaji wa Shirika kwa mwaka 2022/2023, na kukubaliana malengo na kusaini mikataba ya utendaji kwa mwaka huu wa 2023/2024.

Aidha Postamasta Mkuu ameeleza kuwa Shirika hilo limedhamiria kuwa mfano wa kuigwa kwa posta zote barani Afrika kupitia huduma zake za kidijitali na Fedha Jumuishi ( Financial Inclusion).

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ndugu Khadija Khamis Rajab alipokea Tuzo yake na ya Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Khalid Mohamed ya kutambua jitihada za Wizara hiyo katika kutekeleza Sera kanuni na miongozo na mipango ya Wizara hiyo iliyochochea ukuaji, mageuzi na ustawi wa Posta ya kidijitali kwa mwaka 2022/2023.

Aidha Ndugu Khadija Khamis alipata nafasi ya kutoa vyeti vya Pongezi kwa niaba ya Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta akiwemo Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Ndugu Macrice Mbodo, Kaimu Mkurugenzi wa huduma za fedha Ndugu Constantine Kasese, Meneja Mawasiliano Ndugu Elia Madulesi na Mratibu wa Anwani za Makazi Ndugu Jasson Kalile.

Imetolewa na;
Ofisi ya Mawasiliano;
Shirika la Posta Tanzania.
25 Julai 2023
 
Back
Top Bottom