Matumizi ya simu katika Mahusiano

dr. mume na mke siri za nini?
kwa nini kuwe na siri kati yenu?

hata mie nashangaa hizi siri za kutotaka mke/mume azijue...
kama anaona "sehemu zako za siri"
password ya atm, mpesa, tigo pesa, mnashare, hakuna ambacho mnafichana..... then simu inakuwa na siri...mmmmmmmh nashangaaa mie

Kwa mfano...I am a Dr...kama we ni mke wangu, ukishika simu yangu utapata kichaa! Kuna lots texts/emails/chats ambazo clients/ndugu/rafiki wananitumia kwa ajili ya ushauri...na ni issues mbali mbali very personal watu wananitumia na nashauriana nao. Mfano - unafungua simu yangu unakuta chat history na 'mdada' anayenuiuliza madhara ya 'anal sex' sababu she enjoyed it (huu ni mfano wa kweli)...tell me, ungereact vipi??

Hiyo yaweza tokea kwa mwanaume/mwanamke yeyote wa fani nyingine yeyote, haimaanishi ana 'affair', lakini mziki wake waweza vunja penzi.

Wiki iliyopita tu kuna mtu amemuua mwanaume mwenzake huko Mara kisa amakuta ujumbe wa simu kwa mkewe akimuuliza 'mbona hatukuonana nikupe unipe ule mzigo'...yeye na mkewe wote ni wafanyabiashara...sasa bila ya kujua mzigo gani unaua, unafungwa maisha...hasingeshika simu ya mkewe yangetokea wapi hayo?
 
Mimi Bf wangu huwa sigusi kabisa simu yake na wakati mwingne husema simpendi et kisa simfuatilii, lakini yy ya kwangu tukionana tu anasoma msg zote mpka call, ukitaka mahusiano yadumu usiguse simu ya mwenzio, utajikuta msg inaingia mara unaisoma, "oooh dia jana niliinjoi sana kwa penzi lako tamu naomba turudie tena" bora upotezee kabisaa kama una presha unazimia warahii.
 
kama ni m2 mwaminifu huna haja ya kuficha simu,just try to be smart.home yetu simu yoyote itakayo ita mtu aliopo ataibokea na sijawahi kuona m2 analalamika eti fani kapokea cmu ake .Ukiwa mwaminifu utakuwa huru huwezi kuwa na wasiwasi na simu ako!
 
kuwa na mwenza au mke/mume sio kigezo tosha cha mmoja wenu kupoteza kabisaaa privacy yake..

simu pia ni kati ya vitu vinavyotunza privacy za watu wengi sana kwa sasa na kwa technolojia tuliyonayo duniani... kwa mantiki hiyo naomba nishauri kuwa ni vema kila mtu aka-handle privacy yake kwa upande wake na mwenza wake pia ajitahidi kuheshimu hiyo privacy ya mwenzake..so ni vizuri simu zikamilikiwa na mmiliki husika regardless mahusiano yenu yako vipi...

siri ni zaidi ya kuwa na extra girlfriends or friends with benefit amabao unawasiliana nao behind ur partner's back...zipo some family related issues ambazo usingependa kwa wakati huo mwenzako azijue...bado ni copyrighted material ya first family members/citizens then raia muamiaji/mwenzawako anaruhusiwa kujuwa after the family decission to tell others.
 
Aisee mtu kama sio mwaminifu sio mwaminifu tu hata kama asipoweka password kwenye simu haitasaidia,mimi mume wangu hajaweka password na hanikatazi kutumia simu yake ila kuna siku nikiangalia kwenye inbox hukuti received msg na wala hukuti sent msg!kadelete kila kitu.Nilichoka siku moja nilikua natumia laptop yake nikaona yahoo messenger chat zake nusu nife kwa kihoro,usiombe kabisa kukutwa!!!!nimekoma siku hizi siangalii chochote
 
Kusoma au kugusa simu ya mwenza wako sio tatizo bali shida inakuja ni kitu gani utakikuta kwenye simu ya mwenza wako na hapo ndipo shida inapoanzia so in order to be safe majority huwa wanajaribu kuepukana na hizo shida huwa hawapendi kugusa kabisa na ndiyo maana waswahili wanasema ukimchunguza bata kamwe hauto mlaa.
 
unajua nini amegundua kwamba unampenda sana, ndo maana ana kiburi

usimuache kwa sasa ila tafuta hobby zingine zitakazo kupa faraja, jichanganye sana na marafiki, yeye mpotezee kiaina, punguza kumpigia simu au acha kabisa,message zake chelewa kujibu akituma leo jibu kesho yake jioni, akitaka kuja kwako jifanye haupo ni ngumu ila itakusaidia sana, ndani ya mwezi utagundua kama kweli na yeye anakuhitaji, na hata ukiamua kumuacha hautapata shida kwani utakuwa umezoea staili mpya ya maisha yako bila ya yeye kuwepo. Pole sana inaitaji nguvu ya ziada kuona visivyoonekana

Huyu msichana nampenda sana tena sana na yeye ananipenda ..huwa sipendagi kushika simu yake ila kuna siku nilishika simu yake akaichukua ghafla akafuta meseji nikamuuliza kwa nini amefuta akasema kuwa imetoka kwa ex wake na hakutaka niione..sasa nimwache aendelee kuwasiliana na ex wake ama nifanyeje?
updates!
Jamani huyu msichana kweli anayo nia njema na mimi kweli? tar 26 nilimkataza asiwasiliane na ex wake huyo bila ya kunihusha akanielewa sasa tar 29 akambeep huyo ex wake wakawa wanachati kwenye yahoo.. ..
na wameahidiana kutumiana meseji ili wawe wanachati huko yahoomessenger
kweli huyu mdada ana nia njema na mimi kweli?halafu kial saa ananinunia nikimuuliza kuhusu huyo ex wake anakuwa kama mbogo ananuna mpaka basi..eti wadau hapa kuna maisha kweli hapa??
naomba kama una matusi uachane na thread yangu nahitaji ushauri na wala sio kebehi. najua sio vizuri kukagau vitu vya mpenzi wako ila ukiona kuna kitu kimebadiliak naona ni vema kukagua .. nafanya hivi kwani natyaka nioe na huu ndio umri wangu wa kuoa so sitaki niingie mkenge .
Regards!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

updates!!

huyu mrembo nimekutana naye leo tukakaa sehemu nikamuuliza

hence nimeshapewa jibu ..i m supposed to read between lines
 
Nadhani kwa upande mmoja au mwingine simu ni privacy ya mtu,sio kipimo cha uaminifu. kwani wapo watu ambao hata hawahitaji kutumia simu kuonyesha uaminifu wao.

Simu pia zaweza kukuharibia maisha,a friend of mine alinipa stori mke wake alishamtukana mama mkwe wake ,ilitokea kwamba mama alipiga simu kwa kutumia simu ya mtoto wake mwingine na bahati mbaya number ilikua mpya so mke akapokea ,sasa mama mkwe aliposema haloo na msichana tu kusikia ni sauti ya kike ,kabla hata alyepiga hajajitambulisha si msichana akaanza matusi,yaani matusi hayo mara we mal..a unmpigia mume wangu simu ya nini mara,na mengine hata hayafai kusema huku.

Maskini mama wa watu akawa mpole, akakatiwa na simu,baadae sasa ndio jamaa aje,kwani wakati simu inaita alikua bafuni kurudi si ndio akaanza kumwakia mumewe,ohh we mhuni sana mara sijui nini,mara hata hawajamaliza si ile simi ikaita tena,ikabidi jamaa apokee ,mke akaanza tena weka loud spika nimskie huyo ms....@@### anataka nini,yaani baada tu ya jamaa kuweka loud spika na kuskia ni sauti ya mamake na kumsalimia shikamoo mama,mke alitamani aingie chini ya uvungu.well tatizo likawa solved lakini hiyo aibu msichana aliipata sidhani hata kama anatamani kumwona mama mkwe wake na yeye na simu tangu siku hiyo basi,Sasa fikiria suala kama hilo,yapo na mengine nadhani zaidi ya haya.
 
Mi nimemwambia asiguse kabisaaa simu yangu. Na yake sigusi. Na huu ndo usawa.
 
Umeona eeh.
Mimi wala sishangai na sina muda wa kubishana na wanaotetea usiri wa simu kwa kuwa nijuavyo mimi 99% ya wanaume ni cheaters ...kwa hiyo usitegemee watakubali simu zao ziguswe na wake zao.

Ila mimi mume wangu atafute simu ya siri kani simu yake naigusa whenever I feel like...na analijua hilo. Privacy my foot!

Eti simu ni diary...mara ngapi zinakwapuliwa na vibaka??? Kazi gani unayofanya ambayo mke hapaswi kuijua??? Unauza madawa ya kulevya???

Ivi siri na aibu kubwa ya binadamu si utupu/uchi? Lakini kwa nini unakuwa huru kuvua nguo zako mbele ya mkeo/mumeo? Mi nadhani huyo ni mtu ambaye unaweza kushare nae siri yako kubwa, so kwenye simu kuna siri gani ambayo hutaki mwenza wako aijue?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nijuavyo mimi watu wote wanaofanya kazi nyeti hawaruhusiwi hata kutumia private PC kwa shughuli za kikazi... Afu watu wanakuja na cheap explanation eti siri za kazini...Kazi zenye usiri uwa zinaishia ofisini. Acha kuwadanganya wake zenu.
 
Umeamua kuishi kwa matumaini au? Sijakupata?
Hata kama huangalii deep inside unajua mumeo anakucheat...hata uki pretend kuwa everything is okay.

Kwa wasio na maamuzi yeyote...wanaoshindwa hata kuwakemea waume zao...hakuna haja ya kugusa simu za wenza wenu kwani hata ukijua haita make difference.


Aisee mtu kama sio mwaminifu sio mwaminifu tu hata kama asipoweka password kwenye simu haitasaidia,mimi mume wangu hajaweka password na hanikatazi kutumia simu yake ila kuna siku nikiangalia kwenye inbox hukuti received msg na wala hukuti sent msg!kadelete kila kitu.Nilichoka siku moja nilikua natumia laptop yake nikaona yahoo messenger chat zake nusu nife kwa kihoro,usiombe kabisa kukutwa!!!!nimekoma siku hizi siangalii chochote
 
Umeona eeh.
Mimi wala sishangai na sina muda wa kubishana na wanaotetea usiri wa simu kwa kuwa nijuavyo mimi 99% ya wanaume ni cheaters ...kwa hiyo usitegemee watakubali simu zao ziguswe na wake zao.

Ila mimi mume wangu atafute simu ya siri kani simu yake naigusa whenever I feel like...na analijua hilo. Privacy my foot!

Eti simu ni diary...mara ngapi zinakwapuliwa na vibaka??? Kazi gani unayofanya ambayo mke hapaswi kuijua??? Unauza madawa ya kulevya???

99% ya wanaume wanaoleta usiri siri na simu zao ni CHEATERS tu, kwa issue ya madawa ya kulevya sidhani kama ipo
 
Kwenye mahusiano kuna mambo mng km kuaminiana kuheshimiana nk! Lkn zaid na zaid ni ukwel so me naona ni vyema kuwa mkwel 2! Mn za mwiz 40! Haha

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Nijuavyo mimi watu wote wanaofanya kazi nyeti hawaruhusiwi hata kutumia private PC kwa shughuli za kikazi... Afu watu wanakuja na cheap explanation eti siri za kazini...Kazi zenye usiri uwa zinaishia ofisini. Acha kuwadanganya wake zenu.
nyumba kubwa ndio maana nilisema pale mwanzo kuwa hapa tutazunguka mbuyu bure..
Sisi wanaume na hao wanawake wanaotetea USIRI we are all cheaters..kwisha habari yake..
Hakuna sababu utakayoieleza kwenye NDOA ikakubalika kuhusu kuweka password kwenye simu..
Kinachofanyika ni watu kukubali tu matokeo kwamba hata nikijua haita-make difference..
Then wacha tuishi kwa matumaini..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom