Wadau naleta kwenu,mada hii :ni Lipi jema katika mahusiano kati uhuru wa kutogusa simu ya mwenza wako (msg ) na hata ikiita na kuwa mnaweza kusomeana au kuchulia msg??maana naona mahusiano mengi yanavunjika sababu ya simu za mkononi!!nawakilisha
ukiona mtu hataki cm yake iguswe na yake huyo, kama unajua haina sms mbaya kwa nini uikatalie. cm inapigwa utafikiri wewe ndo costumer care wa mitandao yote. afu eti cm yangu usiguse na mie yako sigusi, jiamin baba kuna lilojificha nyuma ya pazia ndo maana unakuwa mkali kwenye cm.
Kama ni mke au mume ni haki yake kuwa huru kwa simu yako ila kama uko mwaminifu.
Kama hujiamini kwa maswala mbalimbali ndiyo utakuwa mchungu mwenzio kushika simu yako.
Siku hizi simu ni zaidi ya 'mawasiliano'...mbona zamani kulikuwa na simu za landline, ambazo kila mwanafamilia (achialia mbali wapenzi) walikuwa wako huru kuzijibu na hazikuleta matatizo yote haya tuyaonayo sasa? Kwani mtu huwezi tumia simu yako ya mkononi kama landline? Inawezekana...ila tumeshapita enzi zile, tuko kwenye era ambayo simu ni zaidi ya mawasiliano tu...simu ni diary, ofisi, safe yako ya kutunza siri/information zako za siri etc. Kubali kataa, hata kwa wanandoa, kuna mambo/vitu/siri zako ambazo hutaki mkeo/mumeo ajue..na si lazima siri hizo ni kuhusu usaliti wa kimapenzi. na siri hizo zinaweza zikafumuka kupitia kuchungulia chungulia simu za mwenzio na zikaharibu 'uhusiano wa kimapenzi'! Sasa juu ya nini kila mtu hasiwe na privacy yake...
Mimi nimeona na kusikia sehemu nyingi sana wanaogombana wote sababu kubwa ni simu tu na kusomeana msg!ndio najiuliza kila siku ipi bora kati kutosomeana kabisa au kuwa wazi kwa simu ya mwenzako??(Wenye mahusiano au mke na mume)
Siku hizi simu ni zaidi ya 'mawasiliano'...mbona zamani kulikuwa na simu za landline, ambazo kila mwanafamilia (achialia mbali wapenzi) walikuwa wako huru kuzijibu na hazikuleta matatizo yote haya tuyaonayo sasa? Kwani mtu huwezi tumia simu yako ya mkononi kama landline? Inawezekana...ila tumeshapita enzi zile, tuko kwenye era ambayo simu ni zaidi ya mawasiliano tu...simu ni diary, ofisi, safe yako ya kutunza siri/information zako za siri etc. Kubali kataa, hata kwa wanandoa, kuna mambo/vitu/siri zako ambazo hutaki mkeo/mumeo ajue..na si lazima siri hizo ni kuhusu usaliti wa kimapenzi. na siri hizo zinaweza zikafumuka kupitia kuchungulia chungulia simu za mwenzio na zikaharibu 'uhusiano wa kimapenzi'! Sasa juu ya nini kila mtu hasiwe na privacy yake...
Ivi siri na aibu kubwa ya binadamu si utupu/uchi? Lakini kwa nini unakuwa huru kuvua nguo zako mbele ya mkeo/mumeo? Mi nadhani huyo ni mtu ambaye unaweza kushare nae siri yako kubwa, so kwenye simu kuna siri gani ambayo hutaki mwenza wako aijue?