SoC02 Matumizi ya mitandao ya Kijamii

Stories of Change - 2022 Competition

Cbk

New Member
Sep 7, 2022
1
0
MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII.

Mada kuu; je ipi matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa vijana wa kitanzania (miaka 10 -45) hivi leo?

Maana halisi ya dhana kuu; mitandao ya kijamii ni nini? NI huduma ambapo watu huongea, au hujumuishwa pamoja na watu wengine aidha ndani ya nchi au ulimwenguni kote, huduma hizi huweza kuunganisha watu wenye shauku/ mapenzi ya aina moja mfano mpira wa miguu,shule,ndondi vyakula vya aina mbali mbali, filamu ,dini nakadhalika pamoja na urafiki.mifano mbalimbali ya mitandao ya kijamii ni facebook,instagram,twitter na mengineyo mingi ya aina tajwa hapo juu.

Tujikite katika matumizi ya hii mitandao ya kijamii tukirejeshaa fikra zetu kwenye maana hapo juu;
Kwa kutaja maudhui makuu tu;

Kuleta watu pamoja yaani kutujengea urafiki.
Kupokea na kutuma taarifa yaan kubadilishana taarifa.
Inasaidia kukuza kasi ya mawasiliano ndani ya muda mfupi kwa uwanda mkubwa.
Je, kwa mtazamo wangu tujikite kwenye mada na swali lenyewe je mimi na wewe tumezingatia matumizi gani muhimu kama kijana wa kitanzania hapo juu na ipi sababu kuu ya matumizi uloamua kuchagua na kutekeleza matumizi hayo kwa muda mwingi ?

Kwa mtazamo wangu, kwa idadi kubwa ya vijana wa kitanzania bado tunahitaji elimu sahihi ya matumizi ya mitandao ya kijamii sababu kubwa ikiwa bado hatuna katika matumizi sahihi yenye tija kwenye mitandao ya kijamii , asilimia kubwa tumeelekeza kutumia mitandao hiyo kwa jaili ya kuburudisha saikologia ya bongo zetu kuliko kuwa na mtazamo chanya ni kwa namna basi mitandao hiyo inaweza kutunufaisha zaidi kimaendeleo.

Inafikia kipindi nawaza kusema ” what if social network was inverted to exploit our mind set” kwa nini hivyo kwa sababu matumizi kwa asilimia kubwa hayajikita kubadili mfumo wa maisha ya kijana wa kitanzania.

NINI KIFANYIKE?(USHAURI & MAONI YAKO EWE KIJANA WA KITANZANIA)

Ushauri wangu, “je swala/jambo unalolitazamia ndani ya mtandao wa kijamii lina tija gani kwenye maendeleo yako ewe kijana wa kitanzania?” Endapo jibu ni “ndio” basi kwa namna moja ama nyingine ni fursa kwako basi itumie ipasavyo kama “hapana” basi badili mtazamo wako kwenye matumizi unayofanya ndani ya mitandao ya kijamii. Elekeza fikra zako kwenye nini kinachokufaidisha kimaendeleo(UCHUMI) zaidi na si kukonga nyoyo (psychological pressure).

KARIBU KWA MTAZAMO WAKO/WENU EWE MSOMAJI WA JUMBE HII.
Imeandikwa na (C.B.K.)

MAREJEO;
 
Back
Top Bottom