Matumizi ya elfu kumi yangu leo

Matumizi ya elfu kumi yangu leo

Nimeamka asubuhi nina elfu kumi mfukoni , sasa hesabu yake sasa :-
Chai kwa mama niwekee. 1,500/=
Nikatoka kwenda mjini nauli. 1,000/=
Nikala mchana huko mjini. 2,500/=
Nikanunua vocha 1,000/=
Nikanunua maji 600/=
Nimerudi nikanunua bando (MB) 1,000/=
Sasa nina chenchi 2,400/=
Nawaza kula cha jioni na maji pia ya kunywa.

Nitatoboa kweli???
Mhmm matumiz makubwa sana kwa mtu mwenye kipato kidogo.
Labda kama hufikilii kesho.
Chai kwa hiyo bei yako ni ya siku tatu.
Lunch mkuu buku unapata,sema ujatafuta sehemu tu huduma zetu zilipo.
Nauri sawa.
Maji sawa lakn ya jero yanatosha.

Mhmm lkn ushaur mwingine gharama zikizidi fata tu agizo la mkuu sema umejitahidi ushazidi wa 7

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm mpk sasa hivi nmeshatumia elf 9 na ndio kwanza saa 4 asbh
 
Huku mafia utapaweza sasa? Maji ya jero dar huku 1000, soda zote 1000, bia ya 1500 dar huku 3000
 
Nimefuatilia hizi hoja zenu kwa umakini uliotukuka kwa kweli naona number inapayukwa kwa viwango vya kuridhisha so far so good.
 
Hivi awamu hii watz tunaishi chini ya $ ngapi Kwa Siku?

OvA
 
Huku mafia utapaweza sasa? Maji ya jero dar huku 1000, soda zote 1000, bia ya 1500 dar huku 3000
Dar maisha ndiyo rahisi sasa huko kwingine itakuwaje jamani. Buku kumi haina kazi tena.
Mia imebakia kukwangulia vocha.
 
Nimeamka asubuhi nina elfu kumi mfukoni , sasa hesabu yake sasa :-
Chai kwa mama niwekee. 1,500/=
Nikatoka kwenda mjini nauli. 1,000/=
Nikala mchana huko mjini. 2,500/=
Nikanunua vocha 1,000/=
Nikanunua maji 600/=
Nimerudi nikanunua bando (MB) 1,000/=
Sasa nina chenchi 2,400/=
Nawaza kula cha jioni na maji pia ya kunywa.

Nitatoboa kweli???
200623da0d8b2259dbdef7150d007122.jpg
 
Hivi awamu hii watz tunaishi chini ya $ ngapi Kwa Siku?

OvA
Hata hatutabiriki, kuna sehemu Tanzania hiihii ukiitafuta miatano utajuta, katika kijiji wanaweza kuwa nayo watatu tuu
 
Si ungekunywa chai ya rangi, kikombe sh.100/= na maandazi 4 @ Tshs.100/= kwa hiyo chai ungetumia 500/=.
Kuhusu maji ya kunywa si unywe yale ya "kudown load?" kwa maana uchemshe mwenyewe nyumbani ubebe kwenye chupa la maji ya Kilimanjaro.
 
Nimeamka asubuhi nina elfu kumi mfukoni , sasa hesabu yake sasa :-
Chai kwa mama niwekee. 1,500/=
Nikatoka kwenda mjini nauli. 1,000/=
Nikala mchana huko mjini. 2,500/=
Nikanunua vocha 1,000/=
Nikanunua maji 600/=
Nimerudi nikanunua bando (MB) 1,000/=
Sasa nina chenchi 2,400/=
Nawaza kula cha jioni na maji pia ya kunywa.

Nitatoboa kweli???
Ushauri wa bure,uwe unalala kutwa nzima ili kusave pesa,uwe unakula mlo wa usiku tu ambao ni 2,000 kwa hiyo utakuwa umesave 8,000/= kwa kila siku,huna haja ya bundle au maji pindi uwapo umelala.
Mjini mipango!!
 
Nikilala kutwa hiyo ten nitaipataje? Maisha yangu nayajua mwenyewe.
 
Nimeamka asubuhi nina elfu kumi mfukoni , sasa hesabu yake sasa :-
Chai kwa mama niwekee. 1,500/=
Nikatoka kwenda mjini nauli. 1,000/=
Nikala mchana huko mjini. 2,500/=
Nikanunua vocha 1,000/=
Nikanunua maji 600/=
Nimerudi nikanunua bando (MB) 1,000/=
Sasa nina chenchi 2,400/=
Nawaza kula cha jioni na maji pia ya kunywa.

Nitatoboa kweli???
Utatoboa tu ondoa shaka! woiii ebu kula mie nilishajisemea kama natafuta pesa mwenyewe kula kwangu ndo muhimu.Ukiwa nazo piga hata breakfast buku kumi hamna shida kabisa yanini kujibana haya maisha yapo tu.Tumbua mzee ukikosa unaomba assists. teh teh
 
Nimeamka asubuhi nina elfu kumi mfukoni , sasa hesabu yake sasa :-
Chai kwa mama niwekee. 1,500/=
Nikatoka kwenda mjini nauli. 1,000/=
Nikala mchana huko mjini. 2,500/=
Nikanunua vocha 1,000/=
Nikanunua maji 600/=
Nimerudi nikanunua bando (MB) 1,000/=
Sasa nina chenchi 2,400/=
Nawaza kula cha jioni na maji pia ya kunywa.

Nitatoboa kweli???
Hapo kwenye listi vitu vingine ni anasa, eg Bando(MB) hata hiyo mambo ya kula mchana, Mkuu wewe inaonekana bado ni mgeni kwenye hii awamu. Piga ndefu ukale kwenu. saasawa
 
Hapo kwenye listi vitu vingine ni anasa, eg Bando(MB) hata hiyo mambo ya kula mchana, Mkuu wewe inaonekana bado ni mgeni kwenye hii awamu. Piga ndefu ukale kwenu. saasawa
Bando ni muhimu ili niweze kuwa updated, na saa nyingine maisha mengine yanapatikana through bando. Kuna fursa humo na viwezeshi vya kipato wakati mwingine.
 
Back
Top Bottom