Matumizi yako hayaendani na kipato chako.Nimeamka asubuhi nina elfu kumi mfukoni , sasa hesabu yake sasa :-
Chai kwa mama niwekee. 1,500/=
Nikatoka kwenda mjini nauli. 1,000/=
Nikala mchana huko mjini. 2,500/=
Nikanunua vocha 1,000/=
Nikanunua maji 600/=
Nimerudi nikanunua bando (MB) 1,000/=
Sasa nina chenchi 2,400/=
Nawaza kula cha jioni na maji pia ya kunywa.
Nitatoboa kweli???
1. Kwa nini upande basi kwenda mjini ? acha Anasa, tembea.
2. Kwa nini unywe maji ya chupa wakati ya bomba yapo bwerere? Anasa hizo
3. Kwa unywe chai asubuhi - acha Anasa
4. Kwa nini ule mchana? Anasa hizo.
Acha Anasa kijana, maana ungeokokoa Tshs. 5600, kwa hiyo ukijulisha na Tshs 2400 ungebakiwa na 7,000. Maisha mnayafanya yawe magumu ninyi wenyewe!! Poor Budgeting