Matumizi makubwa ya serikali ndio chanzo cha hizi kodi na tozo za uonevu

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,074
Hakika hii Tanzania sasa imekuwa balaa. Serikali imekosa ubunifu kabisa wa vyanzo vya mapato. Haiwezekani kitu kimoja kilipiwe kodi au tozo mbili.

Hivi karibuni Serikali imekuja na tozo ambayo mweka fedha benki anakatwa kila anapotoa fedha ktk akaunti yake na benki nayo wakati huo huo inakata hakika huu ni wizi wa mchana.

Sababu kubwa ya haya matozo na kodi lukuki ni kutokana na matumizi makubwa yanayofanywa na Serikali. Matumizi hayo ni pamoja na:

1. Ununuzi wa magari ya kifahari kwa viongozi kuanzia ngazi ya wilaya wa chama na Serikali

2. Misafara mikubwa ya viongozi

3. Mishahara na posho kubwa ya wabunge halali na wale 19 wasio halali

4. Wizi mkubwa wa fedha za miradi za Serikali unaofanywa na watendaji na wakandarasi na wazabuni mbalimbali.

Ushauri kwa serikali

Ni vema serikali ikapunguza matumizi yake ili kuwapunguzia wananchi masikini zigo la kulipa kodi

Na tozo lukuki zilizowekwa na serikali.

Pia serikali iwachukulie hatua kali watu wote wanaoiba fedha zake ikibidi ifirisi mali zao ili kufidia wizi walioufanya. Pia serikali iangalie ukubwa wa mishahara ya wabunge kwani ni mikubwa sana na ukizingatia hawalipi kodi na pia kuwalipa mishahara wabunge fake 19 ni uhujumu uchumi wa fedha za umma.

20220726_231115.jpg
 
Tena ikibidi maafisa wa serikali waachane na ma-V8; waongeze bajeti wanunue chopa za ukweli ili kuwahi kwenye miradi na kazi nyinginezo.
Wakitekeleza hili andiko lako naona tutagawana vizuri cake ya Taifa. Maana kwa mwaka tutazika mawaziri wasiopongua watatu kutokana na vifo vya ajali za hizo chopa.
 
Hakika hii tanzania sasa imekuwa balaa.Serikali imekosa ubunifu kabisa wa vyanzo vya mapato.Haiwezekani kitu kimoja kilipiwe kodi au tozo mbili.

Hivi karibuni serikali imekuja na tozo ambayo mweka fedha benki anakatwa kila anapotoa fedha ktk akaunti yake na benki nayo wakati huo huo inakata hakika huu ni wizi wa mchana.

Sababu kubwa ya haya matozo na kodi lukuki ni kutokana na matumizi makubwa yanayofanywa na serikali.Matumizi hayo ni pamoja na:

1. Ununuzi wa magari ya kifahari kwa viongozi kuanzia ngazi ya wilaya wa chama na serikali

2. Misafara mikubwa ya viongozi

3. Mishahara na posho kubwa ya wabunge halali na wale 19 wasio halali

4. Wizi mkubwa wa fedha za miradi za serikali unaofanywa na watendaji na wakandarasi na wazabuni mbalimbali.

Ushauri kwa serikali

Ni vema serikali ikapunguza matumizi yake ili kuwapunguzia wananchi masikini zigo la kulipa kodi

Na tozo lukuki zilizowekwa na serikali.

Pia serikali iwachukulie hatua kali watu wote wanaoiba fedha zake ikibidi ifirisi mali zao ili kufidia wizi walioufanya. Pia serikali iangalie ukubwa wa mishahara ya wabunge kwani ni mikubwa sana na ukizingatia hawalipi kodi na pia kuwalipa mishahara wabunge fake 19 ni uhujumu uchumi wa fedha za umma.

View attachment 2330252
The Citizen updates ? 558bn ?!!
 
Haya ni marudio ya kila mwaka ila hakunaga hatua imewahi chukuliwa
 
Back
Top Bottom