Averos
JF-Expert Member
- Aug 6, 2010
- 993
- 695
Kuna taarifa kutoka kwa wasahihishaji wa mtihani wa kidato cha pili wa mwaka 2012 kuwa HALI NI MBAYA SANA na kuna shule huenda zikakosa kabisa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tatu kwa mwaka 2013! Taarifa zinaeleza kuwa wakati wastani wa kufaulu ni Alama 30, shule kwa Kanda ya Kusini-Lindi na Mtwara wanafunzi wake wameshindwa kabisa kufikisha wastani huo na wengi wao wameishia wastani wa 10 hadi 15! Ikumbukwe kuwa kuanzia mwaka 2012 wanafunzi watakaoshindwa kufikisha wastani wa alama 30 hatawaruhisiwa kuendelea kidato cha tatu bali watatakiwa kukariri kidato cha pili! Matokea ni mabaya sana, lakini swali la kujiuliza ni kuwa TATIZO LIKO WAPI?