Nifanyeje kurekebisha majina ya Mwanafunzi yaliyokosewa kabla hajafanya mtihani wa kidato cha pili?

tamuuuuu

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
19,966
25,200
Wakuu mtoto majina yake yalikosewa sana kuandikwa kwa usahihi wakati wa usajili darasa la saba, jina Lake na jina la Baba. Hivyo alianza kidato cha kwanza kwa majina hayo hayo licha ya kupambana katika level ya shule kuyaandika sawa lakini mkuu aligoma.

Sasa anaingia kidato cha pili, level ambayo atafanya mtihani na atasajiliwa tena. Naomba mawazo yenu tufanyeje ili tufanikiwe yaandikwe kwa usahihi. Yani niwasikiane na NECTA ama nani ili yawe sawa,maana itasumbua huko mbele ya safari.

NB: msaada wenu uambatane na mawasiliano ya sehemu husika.Ahsanteni

CC: Adolf Mkenda - Waziri wa elimu.
 
Kachukue kiapo Kwa mwanasheria au mahakamani yaani Deed poll peleka shule ni kwake watabadilisha.Mimi ilimtokea mwanangu walibadilisha.
 
Asante sn kaka kwa maelekezo .Naweza process mkoa mwingine and then nikaenda nacho kiapo aliko mtoto?
 
Kachukue kiapo Kwa mwanasheria au mahakamani yaani Deed poll peleka shule ni kwake watabadilisha.Mimi ilimtokea mwanangu walibadilisha.
Deed poll ina process ndefu huwezi kuishia kiapo mahakamani ama kwa mwanasheria tu lazima ufike taasisi zingine kama ardhi, RITA na kwingineko.

Affidavit ndiyo unamalizana mahakamani ama kwa mwanasheria na inahusika kama majina yamekosewa herufi hivyo affidavit inathibitisha jina lilikosewa ni lako na sio kubadilisha kabisa.
 
Kachukue kiapo Kwa mwanasheria au mahakamani yaani Deed poll peleka shule ni kwake watabadilisha.Mimi ilimtokea mwanangu walibadilisha.
Mfano jina kwenye cheti cha kuzaliwa ni Adam halafu kwenye NIDA Adamu hapo unaweza kuchukua tu affidavit kuonesha hayo yote ni majina yako kwa maana yana maana ya jina moja.

Hapo mwanzo hakuna herufi 'u' na jina la pili lina 'u'.
 
Back
Top Bottom