Matokeo ya Kidato cha Pili 2012, Shule zakosa wanafunzi wa kidato cha TATU 2013!

Averos

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
993
695
Kuna taarifa kutoka kwa wasahihishaji wa mtihani wa kidato cha pili wa mwaka 2012 kuwa HALI NI MBAYA SANA na kuna shule huenda zikakosa kabisa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tatu kwa mwaka 2013! Taarifa zinaeleza kuwa wakati wastani wa kufaulu ni Alama 30, shule kwa Kanda ya Kusini-Lindi na Mtwara wanafunzi wake wameshindwa kabisa kufikisha wastani huo na wengi wao wameishia wastani wa 10 hadi 15! Ikumbukwe kuwa kuanzia mwaka 2012 wanafunzi watakaoshindwa kufikisha wastani wa alama 30 hatawaruhisiwa kuendelea kidato cha tatu bali watatakiwa kukariri kidato cha pili! Matokea ni mabaya sana, lakini swali la kujiuliza ni kuwa TATIZO LIKO WAPI?
 
Tatizo ni mgomo baridi wa walimu. Nipo ninafanya utafiti katika shule za sekondary na msingi jijini Dar es salaam. Nitawaleteeni hapa matokeo muone. Kusema ukweli ni kwamba walimu mashuleni hawana tena muda wa kufundisha. Wapo busy na biashara zao. Nitafungua thread na kuleta mchanganuo kamili wa nini kinaendelea mashuleni.
 
How valid is the taarifa?

Mkuu Averos, nadhani msisitizo hasa uko katika msingi(Basics/Primary level)..watoto wengi wanaufaulu usioeleweka, yaani amefaulu lakini kibahati(kusoma, kuandika na kufanya/kukokotoa hesabu ni tabu).Mwanafunzi kama huyu awapo katika mazingira mapya (Sekondari) na akiwa anatambua wazi udhaifu wake, ni ngumu kufanya juhudi maana , kunakuwa na "inferiority complex" hasa kwa baadhi ya wale wenye uwezo.Na inakuwa vigumu kwa mwalimu, hasa kujitoa(devotion) kwa maana ya muda, majukumu mengine ya kijamii n.k

Tuanzie mwanzo kabisa(Shule za msingi), maana watoto wengi huenda shule kama routine/mazoea.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Lukolo hapo bado sijaelewa, Mgomo huu ni wa kuigomea serikali au ni wa walimu kuwa bize na kazi Biashara zao, hata hivyo sio wote wenye Biashara!
 
Na huo ni mwanzo tu,hadi hapo serikali itakapokuja na mpango wa standing allowance

Hahahahahahhahahahahaha! hii imeniacha hoi, Mkuu Ngaramtoni Standing allowance inakuwaje na hulipwa kwa kuangalia vigezo vipi, mwalimu afundishae akiwa amekaa anastahiki hii kitu?
 
nakuunga mkono hippocratessocrates, na hii ni kutokana na umbumbumbu wa viongozi wetu kufanya vitu vyote kisiasa, wanajenga majengo lakini kusema ukweli wale watoto wanaenda sekondari pasipokuwa na sifa thabiti na uwezo wa kimasomo. Mimi nashauri wasije wakavunja kanuni hiyo kustandardize, hii shock ni alarm nzuri sana kwa subsequent years, kila transition ina gharama zake.
 
How valid is the taarifa?

Mkuu Averos, nadhani msisitizo hasa uko katika msingi(Basics/Primary level)..watoto wengi wanaufaulu usioeleweka, yaani amefaulu lakini kibahati(kusoma, kuandika na kufanya/kukokotoa hesabu ni tabu).Mwanafunzi kama huyu awapo katika mazingira mapya (Sekondari) na akiwa anatambua wazi udhaifu wake, ni ngumu kufanya juhudi maana , kunakuwa na "inferiority complex" hasa kwa baadhi ya wale wenye uwezo.Na inakuwa vigumu kwa mwalimu, hasa kujitoa(devotion) kwa maana ya muda, majukumu mengine ya kijamii n.k

Tuanzie mwanzo kabisa(Shule za msingi), maana watoto wengi huenda shule kama routine/mazoea.

Mkuu hippocratessocrates hapo umeleta neno la maana sana, Bila ya Msingi hapana nyumba, Shule ZETU za msingi ni usanii mtupu, walimu wengi hawana Content ya masomo wanayofundisha! tukiimarisha Msingi naamini mambo yatakaa sawa!
 
nakuunga mkono hippocratessocrates, na hii ni kutokana na umbumbumbu wa viongozi wetu kufanya vitu vyote kisiasa, wanajenga majengo lakini kusema ukweli wale watoto wanaenda sekondari pasipokuwa na sifa thabiti na uwezo wa kimasomo. Mimi nashauri wasije wakavunja kanuni hiyo kustandardize, hii shock ni alarm nzuri sana kwa subsequent years, kila transition ina gharama zake.

tatizo kubwa lilipo kitendo cha kuondoa umuhimu wa mtihani darasa la nne ndio kimeleta hasara hii ngoja tusubiri bomu jengine tena..
 
mama kwa heshima na kwa taadhima nayangoja kwanza matokeo ya darasa la saba ndio ntachangia
 
tatizo walimu wapo kwenye mgomo,wamegoma kimya kimya
sababu nyingine wanafunzi wenyewe wana mengi
wengi wao hawapo siliasi na masomo
ni simu,facebuku, ngono na ulevi
wanafikir wanamkomoa kikwete,,, teh teh teh
 
Mkuu Lukolo hapo bado sijaelewa, Mgomo huu ni wa kuigomea serikali au ni wa walimu kuwa bize na kazi Biashara zao, hata hivyo sio wote wenye Biashara!
Mkuu mgomo ni dhidi ya serikali. Na si wote wanafanya biashara, wengine wanafanya twisheni. Walimu hawana kabisa morale ya kufanya kazi.
 
Kama ni mtwara na Lindi hata sishangai na kule tatizo kubwa ni wazazi ndo wanawashawiwhi watoto wao wafeli.
 
Mgomo si chanzo,tatizo ni msingi wa elimu,kama mwanafunzi wa sekondar hajui kusoma na kuandika amefauluje darasa la saba
 
Back
Top Bottom