Matokeo ya Kenya yatangazwa (KCSE) linganisha na Tanzania (CSEE)

Na vile vile hakuna Form VI. Sasa mnalinganisha Sukari na Chumvi?

Umeona ehee, Hawa Jamaa kuanzia aliyeleta mada mpaka wanaoshabikia humu ni weupe Kichwani, ni kama mimi niende sijui Togo, nije hapa niwaletee matokeo ya Mtihani wa Togo na kuwaambia angalia wenzetu wanavyofaulisha bila kujua kwamba Togo na TZ tuna mifumo miwili tofauti kama ilivyo Kenya na Tz! Huwezi kulinganisha vitu visivyolingana!

Najua wametuzidi lakini sio sana kama sisi Wa Tz tunavyodhania, bado na wao elimu yao inachangamoto kubwa. Tusijidharau kupita kiasi. Pia Mfumo wa Elimu wa kwao si sawa na wa kwetu. Wao wakitoka Form IV wanaingia chuo kikuu, wakati sisi tunaingia Form VI. Tusilinganishe vitu visivyolingana.
Mkuu ni wapi tulipolinganisha matokeo ya form IV na form VI? Hapa tunazungumzia KCSE na CSEE. Kwa maana hiyo matokeo tunayozungumzia hapa ni yale yale ya kidato cha nne kwa pande zote. Sasa hebu niambie kama na sisi tungekuwa tunawapeleka chuo kikuu moja kwa moja hao wanaomaliza form IV mwaka huu ungekuwaje?

Ukweli ubaki pale pale kwamba sera yetu ya elimu inahitaji marekebisho makubwa sana. Na hawa mawaziri uchwara wanaopewa hizi wizara kwa kufuata ujomba hawatatutoa!! Bado tunachechemea hatujui tuende wapi!
 
Tukiweka hapa mtihani wa Physics wa KCSE na Physics ya CSEE ndio utanielewa na maaanisha nini, We endelea tu kujidharau.
 
sisi wizara yetu changamoto ya kwanza ni kutopata mawaziri wenye elimu wanaoongoza wizara nyeti ya elimu.

Hilo neno nalichukia sana siku hizi. Linatumika kuficha udhaifu wa viongozi wetu! Badala ya kukubali kwamba kuna uzembe, wao wanaia changamoto
 
Hilo neno nalichukia sana siku hizi. Linatumika kuficha udhaifu wa viongozi wetu! Badala ya kukubali kwamba kuna uzembe, wao wanaia changamoto
uzembe ndo changamoto yenyewe, au wewe mwenzetu unaelewaje hilo neno?
 
Sasa ndugu yangu sie kweli sasa hivi tunaweza kujilinganisha na wakenya? hivi huyu mulugo angekuwa ni waziri wa elimu wa kenya sasa hivi bado angeendelea kuwa waziri (Tanzania ni muungano wa Tanganyika na visiwa vya Zimbabwe na Pemba). Huyu kawambwa nae na issue yake ya mitaala feki kwa wenzetu bado angekuwa anakula kodi zetu pale wizarani? Wenzetu hawataki na hawana mambo ya kipuuuuuuzi kama sisi. Kijiko wanaita kijiko, hakuna lugha ya konakona. Sasa hivi wanampango wa kuweka treni la stima sie hata hiyo ya technolojia ya mwaka 1885 imetushinda kuiendesha. Juzi tu hapa kulikuwa na mashindano ya vyuo vikuu vya East Afrika, Tanzania (wenyeji) tuliwakilishwa na vyuo saba (7) tu. Kenya walileta vyuo 17 na uganda vyuo 19. Sasa hapa ninajiuliza hivi kweli tuna viongozi makini kwenye hii sekta ya elimu?? Tunahitaji mapinduzi makubwa sana kwenye muundo wetu wa serikali otherwise hizi ni rasharasha tu, tutegemee mazito zaidi ya haya. Haya mambo ya kupeana vyeo kwa fadhila madhila yake ndo haya (waliofeli 86%). Yanatia uchungu sana kuwaona wadogo zetu mitaani kwaajili ya ujinga wa mazuzu wawili tu ambao wanakula viyoyozi tu ofisini kwa kodi zetu.YANA MWISHO HAYA

Nimeona niweke vizuri hapo kwenye red kwaajili ya record, otherwise tuko pamoja.
 
Ndiyo maana wakijenga reli sisi tunajenga mfereji. Wakijenga highway, sisi tunajenga vichochoro. Kisa? Elimu ndogo!

wanajenga flyover sisi huku wakandarasi wabomoe daraja chini ya kiwango yakikamilika yanapewa jina la kitaifa Dr.Kj
 
Tanzania kujilinganisha na Kenya kielimu na uchapakazi ni sawa na kusema maji ya mfereji=maji ya bahari!! Na EAC watatutawala na kuchukua kazi zote!! Eti mnajidai kuwa na Federation!!! Mpaka Burundi na DRC watatushinda kama hatutakuwa makini.
 
Tukiweka hapa mtihani wa Physics wa KCSE na Physics ya CSEE ndio utanielewa na maaanisha nini, We endelea tu kujidharau.
Naona wewe sasa unataka kudandia treni kwa mbele!!

Mimi nina ushahidi wa mtu aliyetoka KCSE (akiwa amepata B+) na kuja kusoma TZ (yeye ni m-TZ) ACSEE na alichokifanya ni hatari tupu! Juzi ka-graduate Bugando kama MD maana alikuja kusoma PCB hapa Tz. Kilichofanyika kule Kenya hakuwa amefanya mtihani wa Biology, hivyo alipokuja hapa alitakiwa kurudia mtihani wa Biology ya TZ na akafaulu. Sasa unapotuambia Physics ya Kenya na Tz ni tofauti sikuelewi!!

Kazi ni kwa Kawambwa na Mulugo (Mzee wa Zimbabwe!!)
 
Kenya wanajua wanakotaka kwenda na viongozi wao wako fucused kulifikisha taifa lao huko; tofauti na sisi hapa ambapo viongozi wetu are more focused kwenye kuchumia matumbo!

Tumebaki kuwa taifa lisilo na vision wala mission tunapwaga mbuga bila kutambua tunakotaka kuelekea!!

Elimu ndio ufunguo wa maendeleo; sio Kilimo kwanza na matrekta feki; power tillers!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Tume ya Pinda iende Kenya baada ya uchaguzi mkuu wakapigwe darasa; au wamualike Mutula kilonzo waziri wa Elimu wa Kenya aje ampe tuisheni Shukuru Kawambwa na udaktari wake wote anafanya mabo ya aibu tupu!!
 
Wewe watu wanasoma kule acha huku tunatafuta C tatu.elimu ina wadau wengi wanaotekeleza their professional duties sio ushemeji
Hayo matokeo ni ya kisiasa zaidi la yamelenga kutokuchafua hali ya hewa kipindi hiki cha uchaguzi.uwe mbunifu na mfuatiliaji wa mambo hebu wamletee ndalichako ayasahihishe upya uone shuguli ya jeshi
 
Naona wewe sasa unataka kudandia treni kwa mbele!!

Mimi nina ushahidi wa mtu aliyetoka KCSE (akiwa amepata B+) na kuja kusoma TZ (yeye ni m-TZ) ACSEE na alichokifanya ni hatari tupu! Juzi ka-graduate Bugando kama MD maana alikuja kusoma PCB hapa Tz. Kilichofanyika kule Kenya hakuwa amefanya mtihani wa Biology, hivyo alipokuja hapa alitakiwa kurudia mtihani wa Biology ya TZ na akafaulu. Sasa unapotuambia Physics ya Kenya na Tz ni tofauti sikuelewi!!

Kazi ni kwa Kawambwa na Mulugo (Mzee wa Zimbabwe!!)

Kwa hili la hao Vilaza wawili nakuunga mkono.
 
Back
Top Bottom