Matokeo ya Kenya yatangazwa (KCSE) linganisha na Tanzania (CSEE)

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
Nimemwangaliwa waziri wa Elimu wa Kenya akitangaza matokeo ya KCSE muda mchache uliopita kupitia Citizen Tv. Kwanza alitanza amejiamini, ana furaha, anapigiwa makofi. Amesema kuwa kiwango cha Elimu kimepanda, na kiwango cha Ufaulu pia kimepanda. Mtindo wao wa utangazaji matokeo sio kama wa Tanzania, alitaja kimikoa, na baadaye akataja wanafunzi kumi bora kitaifa, shule kumi bora kitaifa, akaweka msisitizo wa haya yafuatayo ambayo binafsi nimeona ni Tatizo kwa upande wa Tanzania.
  • Watahiniwa walikuwa 437,762= Waziri akasema Transition to higher Education is 100%
  • Akakiri kuwa Ratiba ilibadilika kidogo kwa wiki 3 kwa sababu ya mgomo wa Waalimu
  • Akasisitiza; Cheating is no longer option in Kenyan Examination process, yaani hakuna udanganyifu
  • Waziri akasema watu 88 WAMEFUNGWA kwa sababu ya kudanganya katika mitihani, au irregulaties mbalimbali
  • Wavulana wamefaulu kwa 55%, na Wasichana 45%...................
  • Akasema wataangalia upya madai ya waalimu kama walivyokuwa wamekubaliana

NIMEMALIZA KUSIKILIZA HIVYO, NIKALINGANISHA NA MATOKEO YETU YA MAJUZI YALIYOTANGAZWA, Nimejiuliza sana sisi tumekosea wapi Watanzania?.
'Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane ndipo tusameheane'. Wanaong'ang'ania kukaa ofisini na wanaambiwa kuwa wametufelisha watoto kwa kutowajibishana, au kwa kufuata sheria kwa uleglege wachukuliwe hatua gani?
 
Wao wametenga 7% nyie mmetenga 1.7% kwenda elimu,wao wameongeza 300% kwa mshahara nyie mna waalimu wa mahakama n.k
 
serikali ilioundwa na vyama vingi lazima iwajibike
sisi tunalia lia tu CCM yajenga nchi kumbe inajenga taifa la wasio na elimu
ni wakati sasa wa kuwa na katiba mpya inayoruhusu vyama vingi kuunda serikali ili kujenga uwajibikaji
bila umakini na kuwa serious hakuna kinachoendelea.
Mtu kama kawambwa aliepigia magoti wananchi ili wamchague ana uchungu gani na elimu yetu?
serikali isipojali waalimu, ikawaboreshea mazingira mazuri ya kazi, maabara zikajengwa,vifaa vikawepo na pia
vitabu nk elimu yetu itabaki kudharaulika daima.
 
Hayo matokeo ni ya kisiasa zaidi la yamelenga kutokuchafua hali ya hewa kipindi hiki cha uchaguzi.uwe mbunifu na mfuatiliaji wa mambo hebu wamletee ndalichako ayasahihishe upya uone shuguli ya jeshi
 
Nimemwangaliwa waziri wa Elimu wa Kenya akitangaza matokeo ya KCSE muda mchache uliopita kupitia Citizen Tv. Kwanza alitanza amejiamini, ana furaha, anapigiwa makofi. Amesema kuwa kiwango cha Elimu kimepanda, na kiwango cha Ufaulu pia kimepanda. Mtindo wao wa utangazaji matokeo sio kama wa Tanzania, alitaja kimikoa, na baadaye akataja wanafunzi kumi bora kitaifa, shule kumi bora kitaifa, akaweka msisitizo wa haya yafuatayo ambayo binafsi nimeona ni Tatizo kwa upande wa Tanzania.
  • Watahiniwa walikuwa 437,762= Waziri akasema Transition to higher Education is 100%
  • Akakiri kuwa Ratiba ilibadilika kidogo kwa wiki 3 kwa sababu ya mgomo wa Waalimu
  • Akasisitiza; Cheating is no longer option in Kenyan Examination process, yaani hakuna udanganyifu
  • Waziri akasema watu 88 WAMEFUNGWA kwa sababu ya kudanganya katika mitihani, au irregulaties mbalimbali
  • Wavulana wamefaulu kwa 55%, na Wasichana 45%...................
  • Akasema wataangalia upya madai ya waalimu kama walivyokuwa wamekubaliana

NIMEMALIZA KUSIKILIZA HIVYO, NIKALINGANISHA NA MATOKEO YETU YA MAJUZI YALIYOTANGAZWA, Nimejiuliza sana sisi tumekosea wapi Watanzania?.
'Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane ndipo tusameheane'. Wanaong'ang'ania kukaa ofisini na wanaambiwa kuwa wametufelisha watoto kwa kutowajibishana, au kwa kufuata sheria kwa uleglege wachukuliwe hatua gani?

Mbona naona Siasa tu hapo. Hakuna Takwimu za maana. Wangapi wamepata Div I, II,III ??. Sijaona kitu kinachokushangaza.
 
sisi wizara yetu changamoto ya kwanza ni kutopata mawaziri wenye elimu wanaoongoza wizara nyeti ya elimu.
 
Kulinganisha matokeo ya Kenya na yetu ni sawa na kulinganisha akili na Ujinga. Wakati sisi tunashindana kuongoza kwenye Ujinga, wenzetu wanapigana kuukimbia. Kama mtoto wa rais anasoma shule ya bei mbaya na anapata division 4, unategemea vipi ataweza kuithamini elimu!
 
Mkuu inamana wanafunzi wa Kenya hawatumii simu na facebook?!
Maana nilimsikia kiongozi mmoja wa serkal akisema chanzo cha kufeli wanafunzi ni matumizi ya simu na facebook na wala sio sera mbaya ya elimu!!!
 
Nimemwangaliwa waziri wa Elimu wa Kenya akitangaza matokeo ya KCSE muda mchache uliopita kupitia Citizen Tv. Kwanza alitanza amejiamini, ana furaha, anapigiwa makofi. Amesema kuwa kiwango cha Elimu kimepanda, na kiwango cha Ufaulu pia kimepanda.
hapo kwenye red ni kwa sababu kiwango cha budget ya elimu kimepanda pia ambapo opposite yake ina apply hapa kwetu!
 
Sasa ndugu yangu sie kweli sasa hivi tunaweza kujilinganisha na wakenya? hivi huyu mulugo angekuwa ni waziri wa elimu wa kenya sasa hivi bado angeendelea kuwa waziri (Tanzania ni muungano wa visiwa vya zimbabwe na pemba). Huyu kawambwa nae na issue yake ya mitaala feki kwa wenzetu bado angekuwa anakula kodi zetu pale wizarani? Wenzetu hawataki na hawana mambo ya kipuuuuuuzi kama sisi. Kijiko wanaita kijiko, hakuna lugha ya konakona. Sasa hivi wanampango wa kuweka treni la stima sie hata hiyo ya technolojia ya mwaka 1885 imetushinda kuiendesha. Juzi tu hapa kulikuwa na mashindano ya vyuo vikuu vya East Afrika, Tanzania (wenyeji) tuliwakilishwa na vyuo saba (7) tu. Kenya walileta vyuo 17 na uganda vyuo 19. Sasa hapa ninajiuliza hivi kweli tuna viongozi makini kwenye hii sekta ya elimu?? Tunahitaji mapinduzi makubwa sana kwenye muundo wetu wa serikali otherwise hizi ni rasharasha tu, tutegemee mazito zaidi ya haya. Haya mambo ya kupeana vyeo kwa fadhila madhila yake ndo haya (waliofeli 86%). Yanatia uchungu sana kuwaona wadogo zetu mitaani kwaajili ya ujinga wa mazuzu wawili tu ambao wanakula viyoyozi tu ofisini kwa kodi zetu.YANA MWISHO HAYA
 
Hayo matokeo ni ya kisiasa zaidi la yamelenga kutokuchafua hali ya hewa kipindi hiki cha uchaguzi.uwe mbunifu na mfuatiliaji wa mambo hebu wamletee ndalichako ayasahihishe upya uone shuguli ya jeshi

ha ha ha ha ha ha! Mkuu Ndalichako anatisha yule mama sijui huwa anatumia marking schm ya somalia?
 
Mbona naona Siasa tu hapo. Hakuna Takwimu za maana. Wangapi wamepata Div I, II,III ??. Sijaona kitu kinachokushangaza.

Kenya wanatumia GPA style,,, mambo ya division hayo hayawahusu... Wao wanacheki average ya mwanafunzi kwenye national exams
 
waTz kulialia tu oohh wakenya wanachukua ajira zetu...nadhani sababu sasa iko wazi
 
Mbona naona Siasa tu hapo. Hakuna Takwimu za maana. Wangapi wamepata Div I, II,III ??. Sijaona kitu kinachokushangaza.

mkuu mleta mada,hii nchi haiishi wabishi embu kama unaweza tafuta web site ya hiyo wizara ulete ufaulu wao ili ujazie nyama hii hoja yako nzuri ndio tutaweza kulinganisha na hizo zero zetu.
 
mkuu mleta mada,hii nchi haiishi wabishi embu kama unaweza tafuta web site ya hiyo wizara ulete ufaulu wao ili ujazie nyama hii hoja yako nzuri ndio tutaweza kulinganisha na hizo zero zetu.

Sasa tunasifia, wavulana 55% wamefaulu na wasichana 45% wamefaulu, Hiyo nayo Takwimu?.
 
Back
Top Bottom