Matokeo ya Igunga toka kwa NAPE: CCM Yaibuka Kidedea...

Status
Not open for further replies.
Nape Nnauye
Matokeo Igunga.(Jumla kuu ni CCM 26266. CHADEMA 22443)
Na haya ni kata kwa kata...
Mboto CCM 730- CHADEMA 302
Nguvu moja CCM 694 CHADEMA 284
Nkinga CCM1479. CHADEMA 1085
Itumba CCM1079 CHADEMA 590
Nanga. CCM 897. CHADEMA 645
Igurubi CCM 925 CHADEMA 592
Mwisi CCM 926. CHADEMA 992
Mbutu. CCM 1186. CHADEMA 1426
Kinungu. CCM 505 CHADEMA 268
Ngulu CCM 622 CHADEMA 412
Igunga CCM 3181 CHADEMA 3358
Choma CCM 1227 CHADEMA 918
Kining. CCM 700 CHADEMA 451
Mwashiku. CCM 798 CHADEMA 484
Nsimbo CCM 738 CHADEMA 1016
Itunduru CCM 738 CHADEMA 784
Mwamashimba CCM 1224 CHADEMA 1421
Mbutu CCM 1335 CHADEMA 1427
Bukoko CCM 1136 Chadema 931
Nyandekwa CCM 691 Chadema 631
Ndembezi CCM 866 Chadema 806
Chabutwa CCM 545 Chadema 581
Ziba CCM 1053 Chadema 860
Igoweko CCM 1051 Chadema 880
Sungwizi CCM 1225 Chadema 718
Isakamaliwa CCM 525 Chadema 593
OHOOO PEOPLES POWER TENA KWISHNEI!!!!

*******************
Nape kafuta hii status kwenye wall yake kisha kakana kuandika chochote kwenye mtandao

Pilli kata mbili data tafauti jina hilohilo mbutu????
 
Ninachozidi kukukandia Nape ni utoto, kwani lugha zako huonekani kama mtu mwenye wadhifa, ila wale jamaa wa mitaani, na huonyeshi dalili za mtu kupata malezi kwenye familia yenye wazazi wenye nafasi. Unatakiwa jifunze lugha zile za ustaarabu ambazo zinakuweka kwenye heshima yako. Kumbuka huwakilishi kundi la mitaani, bali umma wa watu wenye rika zote na nafasi mbalimbali katika jamii. Hii kitu unaongea hapo kwangu mie unaonyesha ulivyo mtupu kimaadili na kabisa busara na hekima vimekupiga kikumbo mno. Hali hiyo inakuvunjia heshima badala ya kukujengea in future.

Kumbuka tunavyokushauri ni kwa nia njema kabisa, unataka uone jamii yako tunaokuzunguka na kuongea juu yako ni kioo chako cha kujitazama na kujirekebisha kama umefanya visivyo, lakini ufanyavyo ni kama mtu mwenye sikio lililokufa. Jaribu kurudi kachukue somo la uongozi watakusaidia kupata falsafa gani kama kiongozi mwandamizi utumie kwenye umma badala ya hii, maana kuna wazee wenye heshima zao hawatafurahishwa na lugha hizi.

Nikupe darasa: ungeandika kama ifuatavyo ningekuona zimekaa vizuri kichwani:
"Pamoja na jitihaza zote za Chadema na kujigamba kuchukua Jimbo la Igunda imewawia vigumu kwa vile CCM ina mizizi. Hata hivyo tunawapongeza Chadema kwa changamoto waliyotupa na tumejifunza udhaifu wetu namna gani ya kukabiliana nao. Hivyo ushindi wetu kwa kuchukua kata nyingi ni kielelezo cha kukubalika bado kwa chama chetu huko Igunga."

Hii ningekuona kama kichwani umetulia, lakini uliyoongea ni sawa na wale jamaa baada ya kukolea hukenua midomo na kutikisa mabega huku mwili ukiwasisimua kwa awamu kwa vile wamekuwa stimulated by something, you know what I mean? Aka under influence!

kila lugha ina mazingira yake halafu dawa ya moto ni moto huwezi kutoa lugha ya kistaarabu kwa mtu anayetoa lugha za kihuni mi kwanza naona hakuna ubaya wowote kwa kauli hiyo ya nape!
 
Nnauye jr.huyu jamaa amekana kuwa yeye ajaweka post yeyote kwenye jf na kwenye fb ameremove wall ya matokeo ya igunga.Mod kwa nini ihi id ya nnauye jr isiwe blocked kabisa inaharibu sifa ya jf kwa mtu anaefahamika tena kiongoz wa juu ktk chama.huyu bwana umr wake bado mdogo lakini kwangu ni bro vitu anavyofanya sijaviafki kwanini awe muwongo kiasi hiki.mod mpe ban ya life.mtu muwongo ni mbaya kuliko hatari kuliko fisadi.

Umenena mkuu.
 
Pamoja na magamba kushnda kwa ushnd dhaifu jimbo la igunga,bado harakat za mageuz zinasonga mbele na balaa zaid wataisoma namba 2015.jitihada zilizooneshwa na wanamagamba,serikal(mawaziri,rais mstaafu),jeur ya fedha kwa kuwachelewesha wafanyakaz mishahara yao ya sept ili wahonge wapiga kura pamoja na nguvu ya polis na usalama wa taifa ni dhahir tosha kwamba magamba hayakubalik kwa watanzania walioweng. "ushaur"naomba magamba yaliyosalia including lowassa, chenge nawengineo pia wajivue gamba ili muone moto wa chadema.
 
Kwanza ninawapongeza CHADEMA kwa kufanya vizuri katika uchaguzi wa Igunga. Kwa kweli matokeo haya yanaonesha ni kwa kiasi gani CDM inakubalika. Wanamageuzi tusife moyo, huu ni mwanzo mzuri sana, uwezo, nia na ari ya kuiongoza nchi hii 2015 tunayo na tunaweza. Matokeo ya Igunga ni ishara tu kwamba ccm wamefika kileleni na hawana pa kwenda tena. Tuendelee kuzitangaza sera nzuri za CDM na kupinga ubaguzi wa aina yeyote hasa wa kidini ambao unaenezwa na CCM na CUF (CCM B). HONGEREZI WANA CDM IGUNGA - MSIFE MOYO, KAZI NDIYO IMEANZA SASA
 
MMeibiwa kura mlikuwa wapi? Don't be a poor loser!!!

A poor loser has no means to win..........just imagine these organs all in your side
  1. THE DC AND HER ANTICS
  2. NEC
  3. POLICE
  4. STATE INTELLIGENCE
  5. THE RETURNING OFFICER
  6. AND CUF OF COURSE
How the hell could you loose?
 
magwandwa nomaaaaa kelele zote hizo aibu hii sasa inakuaje? Kati ya kata 22 mmeambulia 3 ccm ikiibuka na 18 cuf moja tu, masikini
mmh aisee sijawahi kuona kijana mdogo mwenye mawazo mgando kama nape yani unafurahia nchi yako ikiangamia...mle nyie tushibe sisi!!aya bana mungu akubariki
 
nimesoma hii ikanivutia juu ya huyu kijana!
Wakuu nilimwahidi Nape kama nnavyosomeka hapa chini kumpa USD 100 kama ataenda Igunga na akahutubia mkutano wa kampeni. Hii ni kutokana na maneno yake mwenyewe kama anavyosomeka hapa chini. Sasa zimebaki siku mbili lakini kimya.

Kwa hiyo basi kama nilivyoahidi na kumthibitisha kwamba nilikuwa na nipo serious na ahadi yangu namtumia invisible hela hiyo in few hours tyme. Ikiwa Nape hatakwenda basi tutaipeleka hiyo hela kwenye charity yeyote of our choosing!!!!!!!!!!!

....
...
Dogo inaonyesha umeshaanza kupoteza focus, maana ule moto wenu wa kujivua gamba nadhani ndiyo umeenda huo. Maana sijamsikia Kiongozi wa CCM yeyote huko Igunga akielezea ni namna gani CCM kilivyo chama bora na kwamba sasa kinajisafisha kwa kuvua magamba. Neno gamba vp nalo ni prohibited Igunga?

Ya mwisho, ni kaswali kafupi not meant to offend at all, una ID nyingine au zingine zaidi ya hii ya Nnauye Jr humu JF?
 
mmh aisee sijawahi kuona kijana mdogo mwenye mawazo mgando kama nape yani unafurahia nchi yako ikiangamia...mle nyie tushibe sisi!!aya bana mungu akubariki

huu ni kijana wa mwili ila kiakili amezeeka.
 
Mheshimiwa Nape,
si kawaida yangu kuingia kwenye malumbano hasa yasizo na tija kwa Taifa langu linaloangamia kila kukicha. Pia sina shida na matokeo uliyoyatangaza, kama ni ya kweli na kama dhamira yako haikusuti kwa maana hakukuwa na uchakachuaji. Na pia kama kweli umekaa chini kabla ya kusema maneno uliyoyasema chini ya figures ulizozileta. Binafsi ni kajana mpenda nchi na mwenye kupenda kufuatilia yanayojiri. Ninaomba nikupe tahadhari tu kidogo ndugu yangu, hao unaowakejeli humu wengine ndo hao hao unaokutana nao kwenye kampeni zako za kuimarisha chama. Ukweli kuna kautoto fulani ndani mwako na sikutarajia hili na nina amini chama kinaweza kuona hili mapema kabla hujaharibu kizazi cha vijana wenye mwamko kidogo na chama. Sikuelewi unapopambanisha vijana humu kwenye jamvi ingali kila kukicha uko mikoani unatafuta wafuasi au wanachama ambao ndo hawa hawa vijana unaowakejeli. Binafsi nimesikitikia kauli zako na naamini ujumbe huu utaupata na hata wakuu katika chama wataupata ili uweze kukanywa la!ninaona hata wachache ambao bado wana kaimani na chama wanaondoka taratibu nikiwaona. Pia sintashangaa kama una agenda ya siri ambayo bado wakuu katika chama hawajaingamua au nao kama wewe mko kwenye mission.
Nakutakia siku njema na furahia vyema ushindi wa igunga ingawa tayari unajua yaliyojiri kwenye kura za madiwani kwingineko nchini
Huu ni ushauri wa bure tu na ninaomba wale vijana walitumwa na Nape kuharibu hili jamvi waufikishe na lengo ni kujenga Taifa wala si kubomoa
mwenye machungu na chi
 
Kama hayo matokeo ni kweli basi ni furaha kubwa kwa Chadema ni mabadiliko makubwa na mafanikio makubwa kuonyesha upinzani wa kutosha na kubadilisha mawazo ya wana igunga kwa siku 21 mungu awabariki chadema waendelee na mbio hizo ili tuchukue nchi 2015 CCM kwishnei masikini weeeeeeeeeeee
 
is nape a reliable source ?? any way Good job chadema from nothing to well established party in Igunga.
mnastahili pongezi hasa ukizingatia mlikuwa mnapambana na Nchi nzima, Taasisi za dini, usalama wa Taifa, Mgambo, Polisi
na kadhalika kwahiyo mnastahili pongezi kwani kama CCM kingekuwa kinashiriki kwenye uchaguzi kama chama cha siasa tu na siyo
chama dola naamini ushindi ungekuwa ni wenu.

ongeza na DCs, RCs na MAWAZIRI.
 
MAGWANDWA NOMAAAAA kelele zote hizo aibu hii sasa inakuaje? kati ya kata 22 mmeambulia 3 CCM ikiibuka na 18 cuf moja tu, masikini
Nape,
Ni mwaka jana tu mlipata zaidi ya nusu kura halali zilizopigwa jimbo hili na CHADEMA hata mgombea ubunge haikuwa naye Igunga. Leo unajivunia matokeo haya? Natumaini kasi ya ukuaji huu CHADEMA mtakaa kuutafakari sana tu ingawa hamna namna ya kuuzuia. Endelea tu na ule mradi wa kuvua magamba yaliyobaki kwani hili la Igunga lilikuwa gamba gumu zaidi.
 
CCM mmejitahidi sana baada ya kuchanganya kura zenu na za CUF! Kweli CUF wanayajua mapenzi!
 
CHADEMA OYeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee........................ Peoples Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr


Ndugu zangu wanaharakati wa mageuzi ya kisiasa, kushindwa huku kwa CHADEMA kwa upungufu wa kura elfu 3 tu ni MTAJI mkubwa sana jimboni humo kwa uchaguzi Mkuu 2015. Haiingii akilini CCM imekaa IGUNGA since independence lakini CDM wamekwenda IGUNGA mwaka huu tu, na bado tumeondoka na kura kibao. Kwangu mimi huu ni zaidi ya ushindi wa kwenda bungeni. Hakuna kukata tamaa. Hakuna kulegeza kamba ya mapinduzi. Nia tunayo, ari ipo na nguvu ya umma inatosha. Tumethubutu, tunaweza na tunasonga mbele. Nawasilisha.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom