Matokeo ya Igunga na Maana yake Kwa CHADEMA kuelekea chaguzi nyingine

Freshbrain

Member
Oct 3, 2011
29
82
Nimefuatilia kwa makini matokeo ya uchaguzi wa Igunga wa tarehe 2/10/2011. Chadema Imeshinda, imevuna Kura 23,260 from ZERO ndani ya mwaka mmoja ikiwa Imeshindwa na CCM kwa kura 26,484 kwa margin ya kura 3224 huku kura 1185 zikiharibika kwa CHAMA ambacho uchaguzi uliopita kilikuwa hakishikiki Igunga,CCM, isitoshe wameshindana na vikwazo vingi sana katika njia ya kufikia hapo ilipofika IKIWEMO KUSHINDANA NA SERIKALI NZIMA, SERIKALI STAAFU i.e RAISI MSTAAFU N.K.

Kwa kuzingatia sapoti waliyoipata kwa wana-igunga, wakati huu wakifuatilia irregularities zilizojitokeza kipindi cha UCHAGUZI hata kama kulikuwa na wizi wa kura wasisahau HESHIMA kubwa waliyopewa na wana-Igunga. WAMEWAAMINI SANA TENA SANA SANA.

Ninachopenda kukishauri chama hiki pendwa na kilicho mioyoni mwa watanzania wengi kwa sasa, ni kuwa kuna umuhimu wa kuandaa mkutano/mikutano ya kushukuru wana-igunga kwa sapoti waliyotoa kipindi chote kabla ya kampeni, katika kampeni na kwa kuwapatia kura za kutosha 23,260.

I believe Great Thinkers,CHADEMA and all Tanzanians will support this Idea of a Freshbrain. God bless Tanzania, God bless Tanzanians and God Bless CHADEMA. Peoples' Power
 

cheze

JF-Expert Member
Apr 27, 2011
501
329
Pamoja na kupoteza katika uchaguzi mdogo wa Igunga,CHEDEMA ndicho kilichopata mafanikio kuliko vyote,toka kura 0 hadi 23000.
 

MartinDavid

JF-Expert Member
May 22, 2009
874
144
Surely ni ukweli kabisa.. 23thou plus siyo haba hata kidogo...

tujipange tu 2015 tutashinda..

God Bless Africa, God Bless Tanzania, God Bless Chadema....
 

Mtoto Wa Mbale

JF-Expert Member
May 15, 2011
457
300
Kuna haja ya Viongozi wa CHADEMA kufanya mkutano mkubwa Igunga kwa ajili ya kuwashukuru wapiga kura na wanaigunga wote kwa kuwaunga mkono.

Wasipofanya hivyo watakuwa hawajawatendea vyema wananchi zaidi ya 23,260 waliowaunga mkono. Ikumbukwe kuwa wako wananchi wengi waliokosa fursa ya kupiga kura kwa mizengwe.
 

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,753
6,526
kweli tupu wazee, wametangaza nikiwa nje ya utandawazi, ngoja nitafute update thread yenye matokeo halisi
 

Escobar

JF-Expert Member
Sep 16, 2011
574
439
Nimefuatilia kwa makini matokeo ya uchaguzi wa Igunga wa tarehe 2/10/2011. Chadema Imeshinda, imevuna Kura 23,260 from ZERO ndani ya mwaka mmoja ikiwa Imeshindwa kwa margin ya kura 3224 huku kura 1185 zikiharibika kwa CHAMA ambacho uchaguzi uliopita kilikuwa hakishikiki Igunga,CCM, isitoshe wameshindana na vikwazo vingi sana katika njia ya kufikia hapo ilipofika IKIWEMO KUSHINDANA NA SERIKALI NZIMA, SERIKALI STAAFU i.e RAISI MSTAAFU N.K.

Kwa kuzingatia sapoti waliyoipata kwa wana-igunga, wakati huu wakifuatilia irregularities zilizojitokeza kipindi cha UCHAGUZI hata kama kulikuwa na wizi wa kura wasisahau HESHIMA kubwa waliyopewa na wana-Igunga. WAMEWAAMINI SANA TENA SANA SANA.

Ninachopenda kukishauri chama hiki pendwa na kilicho mioyoni mwa watanzania wengi kwa sasa, ni kuwa kuna umuhimu wa kuandaa mkutano/mikutano ya kushukuru wana-igunga kwa sapoti waliyotoa kipindi chote kabla ya kampeni, katika kampeni na kwa kuwapatia kura za kutosha 23,260.

I believe Great Thinkers,CHADEMA and all Tanzanians will support this Idea of a Freshbrain. God bless Tanzania, God bless Tanzanians and God Bless CHADEMA. Peoples' Power

You are 100% Right! Message delivered, kama Slaa haymow humu i believe dada Regia Mtema will take this kwa wahusika kwa utekelezaji.
 

holowane

Member
Jan 8, 2009
40
12
Nakubaliana na wewe Freshbrain. Lakini tujiulize wizi huu utaendelea mpaka lini? Tunyamaze na kuwashukuru wananchi wa Igunga, halafu basi? Tunatakiwa kufanya kitu kama watanzania wapenda haki na maendeleo. Askari mnaosimamia utulivu kwa niaba ya chama tawala pamoja na posho zenu kuchakachuliwa hebu amkeni na muwe tayari kusimamia haki. Na nyie watumishi wa serikali mnaokubali kupindisha haki kwa ajili ya kutetea nafasi zenu, jueni kwamba nafasi hizo si za kudumu pamoja na watoto wenu. Mtakuja kulipia tena kwa gharama kubwa zaidi, kama si kesho basi keshokutwa.

CHADEMA OYEE
 

Freshbrain

Member
Oct 3, 2011
29
82
Sure Guys, wananchi wameonyesha imani kubwa sana kwao katika ambalo lilikuwa kwenye mikono ya ccm for 18 years. Inabidi wawashukuru na wala CDM haikuwa kwenye ramani ya huko.
 

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,921
3,213
heeee, itawezekanaje cuf mwaka jana (juzi tu uchaguzi mkuu) wapate zaidi ya kura 10000 halafu leo kura 2000??

There is a fishy game there between ccm and cuf.

Hapa kura za cuf zimenunuliwa na ccm.

Any way, cdm imepata ushindi hata kama haijapewa jimbo.

Mungu yupo, inshalah tutachukuwa jimbo next time kama tulivyochukua biharamulo.
 

NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
362
Naungga mkono hoja....MIA KWA MIA

uongozi wa CHADEMA unapaswa kucheza karata hii muhimu ya kisiasa (hata kama wana lengo la kukata rufaa matokeo) kurudi tena kwa mikutano ya hadhara kwa kata na kuwaambia wana IGUNGA ahsanteni kwa sababu kuna kila sababu ya kuonesha kuwa wana Igunga wamekiamini sana CHADEMA...

Hili si la kupuuzia kwa chama ambacho kinatafuta kila upenyo wa kukubalika kati ya wananchi....
 

MSEJA

Member
Aug 4, 2011
7
1
Wanachadema wote tujipongeza sana kwa matokeo hayo! Sisi tunatisha na safari yetu inamwanga mkubwa kabisa. Haiwezekani kabisa ngome ya CCM kwa miaka yote hiyo halafu tupte kura zaidi ya 23,000. Magamba bado wanatumia mtaji wako mkubwa wa UJINGA WA WATANZANIA WALIO WENGI. Lakini siku zinakuja ambapo kila mmoja ataona kwa macho yake mawili na siyo kuoneshwa na mtu mwingine ukwelli ulipo.Kenya yametokea, Zambia yametokea kwanini isiwe kwetu! Wanatumia umaskini na ujinga wa Wawatanzania ambao umesababishwa na wao wenyewe kuwadanganya na kuwahadaa Watanzania. Chadema msichoke kutoa elimu endeleeni hii ni dalili nzuri. TUNAOMBA VIONGOZI WA CHADEMA NENDENI IGUNGA MKAWASHUKURU WANANCHI WALIOELIMIKA NA KUTAKA MABADILIKO. ASANTENI SANA WANANCHI WA IGUNGA MLIOFUNGUKA, WASAIDIENI NA WENZENU HAO AMBAO MACHO YAO BADO YAMEVAA MAGAMBA HAWAWEZI KUONA.

PEOPLES POWER CHADEMA SONGA MBELE KUBALI MATOKEO, LAKINI FREEDOM IS COMING VERY SOON!!!!!
 

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,623
4,281
Naungana na wewe Freshbrain kwa 100%! Hakuna sababu kwa wana CCM kusherehekea ushindi huu Kiduchu kwa mbwembwe, Chadema wananchi wa Igunga wameonyesha imani kubwa mno kwa chama hiki na ni matumaini yangu kua Chadema wasisite kwenda kutoa shukrani zao kwa wana Igunga hakika mwaka 2015 wanaweza kulichukua hilo jimbo. "Wao wanapesa sisi tuna Mungu"
 

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,250
731
Hakika Chadema wanastahili pongezi, walipigana kiume na watawala wetu wameupata ujumbe kuwa zile zama za kujichukulia majimbo bila kutoa jasho zimepita.
 

Marytina

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
8,251
4,558
Chama cha Allah kimeshinda IGUNGU
nigeria-muslim-eid-al-adha-2010-11-16-6-30-13.jpg
 

Mundu

JF-Expert Member
Sep 26, 2008
2,707
635
Huu ni ushindi kabisa kwa CHADEMA...lazima mie niwapongeze wana Igunga kwa kuiamini Chadema kwa kunywa lager... karibuni NDOVU bariiiidiiiiiii
 

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,570
7,148
Ushauri ni mzuri sana ulioutoa,ni kawaida yetu Watanzania kutoa shukrani kwa chochote kile,kiwe ni kidogo au kikubwa.Kwa sbb uchaguzi huu uligubikwa na mizengwe mingi ipo siku wizi huu utafika kikomo.Mungu wabariki Watanzania,kibariki chama cha Chadema
 

Freshbrain

Member
Oct 3, 2011
29
82
Nakubaliana na wewe Freshbrain. Lakini tujiulize wizi huu utaendelea mpaka lini? Tunyamaze na kuwashukuru wananchi wa Igunga, halafu basi? Tunatakiwa kufanya kitu kama watanzania wapenda haki na maendeleo. Askari mnaosimamia utulivu kwa niaba ya chama tawala pamoja na posho zenu kuchakachuliwa hebu amkeni na muwe tayari kusimamia haki. Na nyie watumishi wa serikali mnaokubali kupindisha haki kwa ajili ya kutetea nafasi zenu, jueni kwamba nafasi hizo si za kudumu pamoja na watoto wenu. Mtakuja kulipia tena kwa gharama kubwa zaidi, kama si kesho basi keshokutwa.

CHADEMA OYEE

Well said Mkuu. Huu wizi utaisha kadiri tunavyosonga mbele..nani alijua watu wa Igunga wangeweza kusapoti upinzani kwa level hii???. Pamoja na CDM kushukuru kwa kuonyesha appreciation kwa wapiga kura wa Igunga, wanapaswa kujipanga na kuhakikisha daftari la wapiga kura linaboreshwa. Kampeni nzuri zaidi itakuwa ya kuhamasisha vijana ambao wanaisapoti wajiandikishe kwa wingi na kuwapa elimu ya uraia kuwa kitambulisho kile ni kwa lengo la kupiga kura na siyo fasheni. Naamini tukifika Hapo, CCM will surely Go.
 

BJEVI

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
1,359
250
chonde chonde VIONGOZI WA CHADEMA,Mkawashukuru wanaigunga,wamewaamini mnooooooooooooooooooooooooo.Ahsanteni sana.
 

Ikwanja

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
2,082
581
Mambo ya kuyafanya.

Pipooooooooozo Pawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, Hongeara sana CDM kwa ushindi Igunga. Naomba tujipange kwenye operation sanaga ili CDM irudi tena igunga kuwakumbusha wana Igunga kuhusu ahadi za magamba ambazo zimetumika kama hongo kwa watu wa vijijni na wanaiginga wote.
1. Kujenga malambo ya maji katika katazote 26 ndani ya miaka minne, ambapo kwa miaka 50 iliyopita wameweza malambo mawili tu
2. Kupeleka maji kutoka kahama, jambo ambalo limeshindikana kwa miaka 50 iliyopita
3. Kujenga miundombinu ya barabara na daraja ambalo imeshindikana kwa miaka 50 iliyopita.
4. Bei ya bidhaa, (sukari n.k) ishuke, Maana kwa sasa nasikia maisha hayashikiki igunga

wakiweza kufanya hayo yote basi CDM itakuwa imeweza kuikomboa igunga na hivyi watakuwa ni washindi halali wa jimbo hilo, ukizingatia kwa miaka yote ya RA hakuna kitu kilichofanyika.

Kwa hiyo naomba makamanda wetu hakuna kulala mpaka kieleweke, Kashindye sis tunajua kuwa wewe ni mbuge, fanya advocacy kwa wanaigunga ili waweze kudai hayo hapo juu kwa nguvu zote.
 
22 Reactions
Reply
Top Bottom