Nawashukuru CHADEMA kwa matendo yao ya kizalendo

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,223
22,303
Nikiwa kama kijana mdogo mwenye umri wa miaka 38 na mwanachama hai wa CCM nimeona nitakuwa sio muungwana nisipochukua nafasi hii kuwashukuru CHADEMA hasa viongozi wao wakuu kwa matendo yao ya kizalendo. Ikumbukwe tangu kuanza kwa awamu hii ya 6, makada wengi wa CHADEMA hasa wale waandamizi wamerudisha upendo kwa nchi yao na kuwa wazalendo. Nawapongeza sana.

Inawezekana kwa kujua au kutokujua lakini itoshe kusema kwamba matendo ya viongozi wa CHADEMA ni ya kizalendo na yanaashiria jinsi gani wana imani na serikali ya awamu ya 6 chini ya Dr Mama Samia Suluhu Hassan. Binafsi siamini kama kuna bahati mbaya kwenye siasa kwahiyo kwa upande wangu najua viongozi waandamizi wa upinzani wanajua wanachokifanya ila hawataki kwenda moja kwa moja kwenye point. Je, ni matendo yapi? Tutaangalia kauli na vitendo vikubwa vilivyofanyika na wapinzani tangu kuanza kwa awamu ya 6.

Tukijukumbusha mwenendo wa mwenyekiti wa kudumu Mbowe mara baada ya kutoka gerezani ni kuwa hakutaka jambo lolote lile zaidi ya maridhiano na kuwaasa wafuasi wake kupitia mikutano ya hadhara kumsapoti Rais Mama Samia na kutotumia kauli za hovyo kuponda. Na Sultani Mbowe hakuishia kuongea tu bali alihakikisha Mama Samia anakubalika na wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) na akaenda mbali zaidi kwa kuwezesha Rais Mama Samia kuwa mgeni rasmi kwenye shughuli ya BAWACHA kule Moshi. WanaCCM lazima tumshukuru Mbowe na CHADEMA kwa ujumla kwa sapoti hii.

Makamu mwenyekiti Lissu naye hakutaka kubaki nyuma. Mara baada ya kulipwa pesa zake alizokuwa anadai toka awamu ya 5, hakusita kushukuru na kuipongeza serikali ya CCM. Lissu amekuwa akisapoti CCM kijanja sana katika namna ambayo wenye akili tumemwelewa na kuamua kuandika uzi wa kumshukuru. Wakati akijua suala la ushoga ni chukizo kwa watanzania yeye Lissu akaamua kutamka hadharani hawezi ingilia faragha za watu. Ile kauli ilikuwa na nia ya kupunguza kuaminika kwa CHADEMA na kuongeza imani kwa CCM. Asante sana Lissu.

Mwenyekiti wa CHADEMA kaskazini, Lema naye kama ilivyo kwa Lissu amekuwa akihakikisha CHADEMA inakosa kuaminika na kuhakikisha CCM inakubalika zaidi. Lema naye hakutaka kabisa kuachwa nyuma na kina Lissu kwa kutamka hadharani jinsi alivyosaidiwa na mwenyekiti wa CCM Mama Samia kwenye mambo yake binafsi. Yeye alienda mbali zaidi kwa kumshukuru mwenyekiti mstaafu Dr Kikwete. Mara baada ya shukrani zake alianza kauli zake zinaudhi kwa makundi muhimu kwenye uchaguzi. Kusema hadharani kazi ya bodaboda ni laana wakati maelfu ya bodaboda ndo waliompokea KIA ilikuwa ni janja yake ya kutusapoti CCM. Asante Lema. Wakati kauli yake kwa bodaboda haijapoa akaja na nyingine ya kushambulia kina mama kwa kusema VICCOBA ni laana. Tunashukuru sana Lema kwa kuhakikisha vijana na kina mama wanaipa kura CCM na kuinyima CHADEMA. Iwe fundisho kwa wale bodaboda waliokupokea KIA.

Mnyika na viongozi wengine wao wanatusapoti kwa kukaa kimya na kutoeleza sera za chama chao. Huwa wanasikika kwenye mambo yasiyo na madhara. Kwa mfano mwenyekiti wa BAVICHA, John Pumbulu, alijitokeza na kudai watu wamsusie msanii Diamond Platnumz. Tunamshukuru pia.

ASANTENI SANA CHADEMA KWA KUHAKIKISHA DR MAMA SAMIA ANASHINDA KWA KISHINDO 2025.
 
Hivi ni kweli unakuwa hujui kuwa bila majeshi na kwenye uwepo wa TUME HURU sisiemu haishindi au unakuwa unajifurahisha?
 
"Nikiwa kama kijana mdogo mwenye umri wa miaka 38" - Nukuu
Mkuu, miaka 35 ndiyo umri wa ujana mdogo unaishia.

Angalizo: Isije kuwa unaishi bado kwa shemeji, mume wa dada yako, ndiyo ikawa sababu ya kufikiri u bado kijana mdogo.
 
Back
Top Bottom