Matokeo ya form four 2008

Kilimanjaro yafanya kufuru matokeo kidato cha nne

2009-02-09 10:10:02
Na Joseph Mwendapole


Shule za mkoa wa Kilimanjaro zimeongoza katika
kundi la shule 20 zilizofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne yaliyotangazwa jana na Baraza la Taifa la Mitihani, ambayo mwaka huu ufaulu ni wa asilimia 75.8.

Taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kusainiwa na Katibu Mtendaji wake, Dk Joyce Ndalichako, jumla ya watahiniwa 233,848 walifanya mtihani huo Oktoba mwaka na waliofaulu ni 168,420.

Katika kundi la shule 20 bora zenye watahiniwa zaidi ya 35 na chini ya 35, mkoa wa Kilimanjaro umeingiza shule sita, ukifuatiwa na Iringa ambayo imeingiza shule nne Dar es Salaam, Singida, Pwani na Kagera zikiingiza shule mbili kila moja. Wakati Mbeya na Tanga zimeingiza shule moja kila moja.

Dk. Ndaliachako katika taarifa yake kinyume cha miaka ya nyuma ambayo hakufanya mkutano na waandishi wa habari kutoa tangazo hilo muhimu, imezitaja shule kumi bora zenye watahiniwa 35 au zaidi kuwa ni sekondari ya wasichana ya St. Francis ya mkoani Mbeya iliyoshika nafasi ya kwanza Marian Girls ya Pwani nafasi ya pili St. Joseph-Kilocha Seminari ya Iringa nafasi ya tatu Uru Seminari ya Kilimanjaro nafasi ya nne na Seminari ya Dungunyi mkoani Singida nafasi ya tano.

Nyingine ni Sekondari ya Wasichana ya Anwarite ya Kilimanjaro nafasi ya sita St. Mary Goreti ya Kilimanjaro nafasi ya saba Sekondari ya Wavulana ya Feza ya jijini Dar es Salaam nafasi ya nane Seminari ya Don Bosco ya Iringa nafasi ya tisa na sekondari ya Rosmini ya Tanga bafasi kumi.

Taarifa hiyo ilitaja shule kumi bora zenye watahiniwa chini ya 35 kuwa ni sekondari ya Scolastica ya Kilimanjaro iliyoshika nafasi ya kwanza.

Feza Girls ya Dar es Salaam nafsai ya pili
Brookebond ya Iringa nafasi ya tatu Bethelsabas Girls ya Iringa nafsai ya nne Maua Seminari ya Kilimanjaro nafasi ya tano Rubya Seminari ya Kagera nafasi sita St. Mary`s Junior seminari ya Pwani nafasi ya saba Katoke Seminari ya Kagera nafasi ya nane Kilomeni Sekindari nafasi ya tisa na St. Carolus ya Singida nafsai ya kumi.

Taarifa hiyo ilitaja shule kumi za mwisho zenye watahiniwa 35 au zaidi ambazo zimepangwa kuanzia ya kwanza hadi ya mwisho kuwa ni: Selembala ya mkoani Morogoro Kilindi ya Pemba Ngwachani ya Pemba Michiga mkoani Mtwara Ummussalama ya Pwani Chunyu ya Dodoma Busi Dodoma Uondwe pemba Nala ya Dodoma na Maawal ya mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo shule kumi za mwisho zenye watahiniwa chini ya 35 ni Juhudi Academy ya Zanzibar, Mima ya Dodoma, Selenge ya Singida, Kijini ya Zanzibar, Kwamkoro ya Tanga, Kwala ya Pwani, Mtende ya Zanzibar, Ng\'oboko ya Shinyanga, Mbuzini ya Pemba na Sekondari ya Ufundi ya Mwadui Shinyanga.

Kati ya waliofaulu wasichana ni 76,472 na wavulana ni 91,948 na waliofeli mitihani hiyo ni 65,428.

Taarifa hiyo inaonyesha kuwa kuna ongezeko la watahiniwa 3,284 waliofaulu mtihani huo ikilinganishwa na idadi ya waliofaulu mwaka jana.

Hata hivyo, taarifa hiyo ilisema kuwa asilimia ya ufaulu inaonyesha kushuka kwa asilimia 10 kutoka asilimia 85.9 ya mwaka juzi hadi asilimia 75 kwa mwaka jana.

Katika ubora wa ufaulu, wavulana wameongoza kwa waliopata daraja la kwanza na kuwaacha wasichana mbali.

Takwimu za Baraza hilo zinaonyesha kuwa wavulana waliopata daraja la kwanza ni 3,743 wakati wasichana ni 1,578.

Katika matokeo ya mwaka 2007 wavulana waliopata daraja la kwanza walikuwa 4,349 wakati wasichana walikuwa 1,900.

Taarifa hiyo ilisema watahiniwa 41,018 waliofanya mtihani wamefaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu ikilinganishwa na watahiniwa 44,348 waliopata madaraja hayo mwaka 2007.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu katika masomo ya lazima, wavulana wameongoza katika kufaulu wakiwa ni 56,172 ikilinganishwa na wasichana 40,459 waliofaulu.

Katika somo la Hisabati wavulana waliofaulu ni 26,532 kati ya watahiniwa 85,625 wavulana waliofanya mtihani huo, wakati wasichana waliofaulu ni 11,145 kati ya wasichana 69,214 waliofanya mtihani huo.

Kwa upande wa somo la Kingereza wavulana waliofaulu ni 57,122 kati ya wavulana 86,158 waliofanya mtihani huo, wakati wasichana waliofaulu ni 41,314 kati ya wasichana 69,522 waliofanya mtihani huo.

Katika somo la Baiolojia wavulana waliofaulu ni 46,183 kati ya wavulana 85,510 waliofanya mtihani huo, wakati wasichana waliofaulu ni 25,385 kati ya 69,121 waliofanya mtihani huo.

Wavulana wameendelea kuongoza pia katika somo la Kiswahili ambapo waliofaulu somo hilo ni 69,051 kati ya wavulana waliofanya mtihani huo na wasichana waliofaulu ni 57,960 kati ya 69,512 waliofanya mtihani huo.

Kwa upande wa somo la Jiografia wavulana waliofaulu ni 55,449 kati ya wavulana 86,002 waliofanya mtihani huo wakati wasichana waliofaulu ni 36,256 kati ya wasichana 69,505 waliofanya mtihani huo.

Taarifa hiyo ilionyesha kuwa wavulana wameongoza pia katika somo la Civics ambapo waliofaulu walikuwa 56,172 kati ya wavulana 86,112 waliofanya mtihani huo, wakati wasichana waliofaulu ni 40,459 kati ya wasichana 69,527 waliofanya mtihani huo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ufaulu kwa masomo unaonyesha kuwa watahiniwa wamefanya vizuri zaidi katika somo la Kiswahili ambapo asilimia 81.5 ya watahiniwa wamefaulu.

Ufaulu katika somo la Hisabati uko katika kiwango cha chini ambapo ni asilimia 24.3 tu ya watahiniwa waliofaulu somo hilo.

Baraza hilo limesitisha matokeo ya watahiniwa 5,135 ambao hawajalipa ada ya mtihani na kwamba yatatolewa mara watakapolipa.

Pia limesitisha matokeo ya watahiniwa 495 kutokana na wakuu wa shule husika kutolipa ada ya watahiniwa pungufu ya 35 hadi hapo watakapolipa ada wanayodaiwa.

Baraza hilo pia limefuta matokeo ya watahiniwa 347 kwa kubainika kufanya udanganyifu katika mitihani.

SOURCE: Nipashe

kwa nini wengi wetu tumekuwa tunaongelea mambo ya makabila sana unakutana na mtu atkulizawewe eti ni kabila gani hususan wasichana hii inatokana na nini kwa nini au kuna nini ndani yake
 
Kinachoniboa na hayo matokeo ni kutokuandika majina halisi ya watahiniwa badala yake wametumia namba za mtihani. What is so special about namba za mtihani? Wanalinda privacy ya nani?

Itawasaidia sana wazazi na sisi tuliombali tunaowasomesha ndugu huko tufahamu matokeo. Hapa nilishadanganywa namba ya mtihani ya mtu aliyepata Div 1 huku najua fika huyo mtoto hana uwezo wa kupata Div 1 na nimeshathidbitishiwa hivyo kuwa amepata 0.

Warudi kuandika majina kama walivyokuwa wakifanya siku zote.
 
Kinachoniboa na hayo matokeo ni kutokuandika majina halisi ya watahiniwa badala yake wametumia namba za mtihani. What is so special about namba za mtihani? Wanalinda privacy ya nani?
Wabongo bwana....wewe mbona hutumii jina lako halisi?
Unalinda privacy ya nani?
 
Wabongo bwana....wewe mbona hutumii jina lako halisi?
Unalinda privacy ya nani?

Yo Yo wewe ni soo!

Yaani nimecheka sina hamu!

Ama kweli bongo kila mtu ana zake!

On a serious note, nadhani baraza halijakosea..kuweka namba ni vyema. Kama una mtoto wako au ndugu yako ni swala la kumwambia akupe namba tuu. Mengine yatajiset. JAMANI, kama alivyoainisha mkuu hapa Yo Yo..kila mtu anapenda privacy yake ilindwe.. so is here kwenye board. Tusiwaonee hawa watoto. Put yourself in their shoes...hivi kweli leo hata kama unafanya masters UK au US..ungependa matokeo yako ya semister yatundikwe kila mtu aone? Think about it! Sana sana hapa tunataka majina kusudi tuanze kuchambua personalities..mtoto wa fulani nk...Which I think is not good.

Ni mtizamo tuu
 
Ukija Ufisadi wachaga wanashambuliwa wao ndio masteering

Likija suala la watu wenye nyazifa mbali mbali wachaga wanaitwa wakabila na kupendeleana.

Likija Suala la kilimanjaro kutoa warembo wengi wanaambiwa walitoa rushwa ya ngono.

Linapokuja suala la kuoana wanaambiwa wao ni wabaguzi hawataki makabila mengine

Likija shule za kilimanjaro kufanya vizuri....

Ni lini tutaacha kuongelea wachaga????

Je, hatuoni kwa kuwaongelea kila wakati ndio tuna wapa umaarufu na pia tunawaongezea comfidence ya kufanya mambo makubwa zaidi?????? we are creating superiority and inferiority complex)
 
Ila aise kwa haya matokeo..tunahitaji kufanya kazi ya ziada.

Duh..harafu mmeangalia zile centre za private? ambako watu wanafanya mtihani wakiwa uraiani kama kujiendeleza? yaani watu wamefeli vibaya mno! Na hao ndo unakuta ni walimu wanafundisha shule kibao za hapa TANZANIA. Now, kama mwalimu kafeli..ataweza kufaulisha wengine?

Masomo ya sayansi yanakwammisha wengi sana. I hope we can do something to aleviate this looming disaster. Harafu wanaoumia zaidi ni watoto wa wakulima, maana wanasoma vijijini na huko hakuna walimu wa kutosha.
 
Wakuu,
Mimi naomba kufahamishwa kitu kimoja hapa... hawa jamaa zetu wanaweza vipi kutaja mkoa fulani kuongoza/kushika mkia ikiwa kila mkoa una idadi tofauti ya shule na wanafunzi wake?..

Mathalan. tuseme mkoa wa Kilimanjaro una shule za secondari 30 na mkoa wa Pwani una 3 tu lakini katika matokeo Pwani shule moja imechukua mshindi wa pili na zile nyingine hazipo ktk idadi ya 20 za juu lakini pia hazipo ktk idadi ya shule za chini kabisa.. iweje izidiwe na Kilimanjaro yenye shule 30 na kati yake 6 zimechukua nafasi ya shule bora 20..(mind U huu ni mfano tu)....
Kwa maana hii nashindwa kuelewa pale tunapochukua idadi ya shule ktk top 20 toka mkoa fulani na kuupa ushindi wakati mkoa mwingine hauna idadi sawa ya shule na wanafunzi..

Mimi nadhani ingekuwa bora sana watumie hizo asilimia kulingana na idadi ya shule au wanafunzi wenyewe mashuleni. Kwa mfano Mkoa wa Dar yenye shule za sekondari 40 wamekaa mtihani wanafunzi 40,000 na walioshinda ni 20,000 ipewe asilimia yake na Mkoa wa Shinyanga wenye shule za sekondari 10, wanafunzi waliokaa mtihani ni 10,000 walioshinda ni 7,000 ichukuliwe kuwa mkoa wa Shinyanga umechukua nafasi ya juu kuliko Dar kwa sababu ya asilimia kubwa ya wanafunzi walioshinda kulingana na shule na wanafunzi wake..

Nadhani hata ktk Utajiri na Umaskini wa nchi hupimwa kutokana na pato la Taifa against idadi ya watu wake kuliko kutazama namba ya watu au pato peke yake..Hivyo inaturahisishia kufahamu ni mkoa gani unahitaji sana kuboreshwa elimu iwe ni kutokana na vifaa, walimu au fedha kwa sababu kutajwa kwa shule moja kuwa juu/chini ya daraja haitupi picha kamili ya elimu mkoa mzima..

Haya ni mawazo yangu tu sijui kama nimekosea!
 
Kwani hao watoto wanaosoma kwenye hizo shule za mkoa kwa Kilimanjaro wanatoka Kilimanjaro pekee? As far as I know wanatoka sehemu yeyote ya Tanzania as long as wamekidhi qualification na kupata nafasi ya kusoma kwenye shule hizo.
 
Hivi hayo makabila yameandikwa wapi ktk report hiyo hapo juu!... au uzee tena maanake mimi sijaona kitu hiyo!
 
Tatizo la Zenj,elimu na dini viko mutually exclusive.

Tukirudi kwenye somo la hesabu kwa ujumla.Ingawa ubora wa walimu unachangia,mzizi wa tatizo uko kwenye preconceived notions kuwa Maths ni ngumu.Mtoto wa miaka 12 anakwambia,''I am not a Maths person'' au ''Maths ni genetic disorder kwenye ukoo wetu''.Huyu hata apewe mwalimu wa aina gani,hesabu itakuwa mbinde.Hata hivyo,katika baadhi ya shule ambazo wanahimiza (if not force) wanafunzi wao kujifikiria as Maths oriented students...speaking for myself,St.Francis and Marian Girls,sio kwamba wote wanaosoma huko hawana imani za ''ugonjwa wa hesabu'',ila system inawasaidia kutambua kuwa imani hizo hazina mashiko na kuwapa nafasi ya kuprove it so.Je hii inawezekana katika shule nyingine pia?Without doubt.

Vitengo vya elimu aside,majumbani mwetu-wazazi,makaka na madada tuache tabia ya kuendekeza imani za kutoweza hesabu kwa wanafamilia wenu.Utakuta mzazi anawaka moto ukifeli Biology,Chemistry au English,ikija kwenye hesabu unasikia,''Oh well,Maths jitahidi tahidi''.And that's it!Wrong!Every student should be able to perfom well in Maths as in any other subject.And don't give me one of those,''Aaa bwana,unajua watu wamejaliwa vipaji tofauti''.I'll tell you what vipaji tofauti means....a 98 in Chemistry and an 85 in Maths.Not average enough?Then a 75 in History and a 68 in Maths.Au ufeli masomo yote kabisa on average tujue kweli hii special needs.Vinginevyo,tunajipotezea tu competent human resource kwa kuendeleza vijidesturi vya kipuuzi.
 
Last edited:
Wakuu,
Mimi naomba kufahamishwa kitu kimoja hapa... hawa jamaa zetu wanaweza vipi kutaja mkoa fulani kuongoza/kushika mkia ikiwa kila mkoa una idadi tofauti ya shule na wanafunzi wake?..

Mathalan. tuseme mkoa wa Kilimanjaro una shule za secondari 30 na mkoa wa Pwani una 3 tu lakini katika matokeo Pwani shule moja imechukua mshindi wa pili na zile nyingine hazipo ktk idadi ya 20 za juu lakini pia hazipo ktk idadi ya shule za chini kabisa.. iweje izidiwe na Kilimanjaro yenye shule 30 na kati yake 6 zimechukua nafasi ya shule bora 20..(mind U huu ni mfano tu)....
Kwa maana hii nashindwa kuelewa pale tunapochukua idadi ya shule ktk top 20 toka mkoa fulani na kuupa ushindi wakati mkoa mwingine hauna idadi sawa ya shule na wanafunzi..

Mimi nadhani ingekuwa bora sana watumie hizo asilimia kulingana na idadi ya shule au wanafunzi wenyewe mashuleni. Kwa mfano Mkoa wa Dar yenye shule za sekondari 40 wamekaa mtihani wanafunzi 40,000 na walioshinda ni 20,000 ipewe asilimia yake na Mkoa wa Shinyanga wenye shule za sekondari 10, wanafunzi waliokaa mtihani ni 10,000 walioshinda ni 7,000 ichukuliwe kuwa mkoa wa Shinyanga umechukua nafasi ya juu kuliko Dar kwa sababu ya asilimia kubwa ya wanafunzi walioshinda kulingana na shule na wanafunzi wake..

Nadhani hata ktk Utajiri na Umaskini wa nchi hupimwa kutokana na pato la Taifa against idadi ya watu wake kuliko kutazama namba ya watu au pato peke yake..Hivyo inaturahisishia kufahamu ni mkoa gani unahitaji sana kuboreshwa elimu iwe ni kutokana na vifaa, walimu au fedha kwa sababu kutajwa kwa shule moja kuwa juu/chini ya daraja haitupi picha kamili ya elimu mkoa mzima..

Haya ni mawazo yangu tu sijui kama nimekosea!

Couldn't have been said any better.
 
Mkuu Yasin ni kweli inasumbua, wangepanga katika "alphabetical order" ingekuwa rahisi. Fanya hivi, ukitaka pata shule kwa urahisi, mfano hiyo shule inaitwa TABORA, basi bonyeza "control+F" (ninamaana anza kubonyeza "control key" na bila kuachia bonyeza F), ingiza jina la shule yako katika sehemu "Find", halafu bonyeza next, itatafuta shule yenye jina TABORA, sasa kama ziko nyingi (Tabora boys, Mzee Tabora, Tabora) utakuwa unaangalia mpaka uipate unayoitaka.



Duu asante sana mkuu nashukuru sana tena sana....Maana nilikuwa nasumbua kichwa nifanye nini maana shule nyingi alafu sina jinsi asante sana mkuu kwa utaalaam wako mzuri!!
 
Hivi kwa nini shule nyingi za wamisionari ndo zinatesa sana???Ningeomba kutoa ushauri kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar wajitahidi sana kuajili waalimu wa kutosha toka huku Bara.Angalia shule nyingi za Zenj zimefanya vibaya.


Kwa sababu zina facilities bora kuliko shule nyengine nyingi, mfano walimu bora, maabara, vitabu nk.
The Roman catholic institutions nyingi zikiwemo shule hapa duniani huwa zinaendelezwa na kupata backup fundings kutoka RC na ndio ukaona wanaweza kumiliki kutoa best Education na kuajiri walimu bora, na hii sio kwa Bongo tu hadi Ulaya na Marekani RC faith schools ziko juu pengine nyuma ya Jewish schools tu ambazo ndio ziko top zaidi.
 
....matokeo hayana tofauti na kazi waliyofanya hao waliotengeneza website, website gani huwezi hata navigate,huwezi hata kutafuta jina la shule mpaka ufinye macho juu chini juu chini...yaani unaweza kutumia saa nzima kutafuta unachotafuta,huu ulipuaji wa kazi sijui utaisha lini,ni aibu kubwa kwa watu wanaosimamia elimu kama NECTA kuwa website mbovu kama hii,next year tafadhari msionyeshe watu hii aibu!
 
....matokeo hayana tofauti na kazi waliyofanya hao waliotengeneza website, website gani huwezi hata navigate,huwezi hata kutafuta jina la shule mpaka ufinye macho juu chini juu chini...yaani unaweza kutumia saa nzima kutafuta unachotafuta,huu ulipuaji wa kazi sijui utaisha lini,ni aibu kubwa kwa watu wanaosimamia elimu kama NECTA kuwa website mbovu kama hii,next year tafadhari msionyeshe watu hii aibu!

Hamna pesa za kigeni!
 
sasa na wengine vuteni soksi mfanye vizuri kama Kilimanjaro...acheni kupiga piga kelele!

Facts speak for themselves!
 
Last edited:
Kuna haja ya kuwakutanisha Walimu wa sekondari toka Kilimanjaro na mikoa mingine ili wale wa Kilimanjaro wawaambie walimu wa kutoka mikoa mingine siri kubwa ya mafanikio yao ili nao wajaribu katika mikoa waliyomo ili kupata matokeo ya juu kama Kilimanjaro. Hongera Walimu na wanafunzi wa Kilimanjaro mafanikio mliyoyapata hayaanguki toka mbinguni bali yanatokana ni kujituma kwenu na kuthamini umuhimu wa elimu katika dunia ya leo.
 
Bongo ni full ubabaishaji mpaka inatia aibu......walimu wababaishaji, wanafunzi wababaishaji, wazazi wababaishaji, kila kitu ni ubabaishaji mpaka li-serikali ni la kibabaishaji!! Matokea ya mwaka huu ni mabovu kwasababu "pepa" halikuvuja...wakiendelea na udhibiti wa "pepa" kama mwaka jana basi in 10 yrs itabidi wa-import wanafunzi kutoka nje ya nchi kusoma kwenye vyuo vikuu vyetu!!

Tanzania imeoza....!!

Mh..!
 
Back
Top Bottom