Matokeo ya form four 2008

Kufeli kwa somo la hesabu nathani hapa serikari inatakiwa kuwa na sera maalumu itakayo toa incentive kwa watu wana soma masomo ya sayansi. Kwa kumbukumbu zangu swala la kuchukia masomo ya sayansi limeshamili kuanzia miaka ya 2000 na kuendelea. Nakumbuka katika kizazi chetu baada ya kumaliza form six PCM 'Physics, Chemistry and Maths' almost 70% ya wanadalasa walisema hawana mpango na course za sayansi kwa level ya chuo kikuu na ndivyo ilivyo kuwa. Wengi walichagua course za biashara university kisa ndizo zinazo lipa uraiani kuliko sayansi ambayo shule yake ni ngumu na mwisho wake mishahara mbuzi. Sumu hii imekua ikisambaa kwakasi hata katinga level za sekondary. Hivyo hata wale wanaosoma hesabu kutotilia mkazo somo hili.

Kwa upande mwingine, yawezekana pia kukawa na upungufu wa walimu wa hesabu. Hivyo nimuhimu kureview education system na kuona tatizo ni nini na nini kifanyike kunusuru hari hii ikiwa ni pamoja na kufuta kauri ya kwamba ''Maths ni ugonjwa wa kitaifa''.
 
Elimu ya Tanzania itaendelea kushuka siku hadi siku kama hakutakuwa na sera maalumu ya kuongeza mapato ya waalimu. Kama mazingira ya Waalimu yataboreshwa, wengi watakimbilia huko. Elimu ndio kila kitu, elimu ndio afya, ulinzi, uchumi nk. Tunatakiwa kuwekeza katika elimu. Watu wakichaguliwa uwalimu, wengi hawaendi, na wanaoenda ukifuatilia hawakufanya vizuri shuleni. Sasa waliofanya vibaya shuleni ndio waalimu wetu.

Nikizungumza na waalimu wa zamani, utajua jinsi jamii ilivyokuwa inawaheshimu, enzi hizo kuchaguliwa kwenda kusomea uwalimu ilibidi uwe umefaulu vizuri. Ndio maana miaka ya nyuma ufaulu wa wanafunzi ulikuwa mzuri. Hivyo hakuna short cut hapa, ni mazingira na posho ya waalimu kuboreshwa ili wanafunzi wavutiwe. Hebu fikiri mwalimu ana kilaka, mwalimu anaomba nauli kwa wanafunzi, kutakuwa na msukumo wanafunzi kuupenda uwalimu. Na kama hawatapenda kuwa waalimu, ina maana wataojiunga na uwalimu wengi wao watakuwa ni wale wameshindwa kupata sifa ya kujiunga na fani wanazoona zinalipa. Pia sisemi kuwa hakuna waalimu bora, ila wamekata tamaa, wakipata nafasi huacha hiyo kazi.

Kila mtu anaangalia kusoma masomo yanayolipa, hiyo ndio asili ya mwanadamu. Hivyo tuwajengee waalimu mazingira bora, ili vizazi vyetu viipende hiyo kazi.
 
Matokeo haya ya vijana kwa kweli yanasikitisha hasa hiyo Maths. Nakumbuka enzi zetu jinsi tulivyolipenda somo hilo na jinsi lilivyotupenda pia. Niliamini wakati huo na hata sasa kwamba mtu akiwa mkali wa hesabu then for sure mambo yote mengine yatakwenda sawa. hata baadhi ya philosopher wa zamani apart from philosophy walipenda pia music na maths.

Nafikiri sababu moja ni walimu (wao wenyewe walifaulu kwa grade D in maths na sasa wanafundisha maths na pia walimu wengi wa hesabu secondary wanapenda kujigamba na badala ya kuwatia moyo wanafunzi walipende somo hilo wao huwa-discourage). wanafunzi pia mentality yao kwamba hesabu ni ngumu na pia kwamba masomo ya science hayalipi na ni magumu.

Jingine ni sera hizi tulizonazo. hebu fikiria walimu wa 'voda-fasta' na pia hii issue ya shule za kata zenye majengo na wanafunzi tu.

ingawa sasa tunasema matokeo ni mabaya hivi kuna mtu anafikiria miaka miwili ijayo tutakapopata first batch la wanafunzi wa shule za kata matokeo yatakuwaje ?

Nakulilia Tanzania. Nakulilia Tanzania, kizazi hiki ..... viongozi hawa .... mhhh..
 
Shule za kata tutaona mengi...I dont even wish kuona hilo.

Matokeo mabovu ya hesabu yana anza toka msingi mtoto akiwa na msingi mbovu wa hesabu ambao mara kwa mara ndio unatoa end ya matokeo ya FORM 4.
Kwanza walimu imekuwa mtu kakosa option ya kupata kazi ndio anaamua kwenda ualimu wengine anaona bora aache ualimu awe mshonaji....mishahara nayo hata ikitoka kuipata kwa wakati ni shida...achilia mbali siku za mwisho wa mwezi NMB ATM utaona vya kuona...nenda kenyatta street mwanza.Utajua na maana gani.

Kuna mifano mingi mtu kakaa bila kazi kwa miaka hata 4,akioana maisha magumu anatafuta cheti chake cha form 4 4 yrs back...anakwenda ku apply ualimu..ilia apate chochote....huyu hana wito kabisa.Hawa sasa kuna wangine kuna wenye 4 zile za mwisho kabisa...anaenda ualimu kisha anakuja fundisha hesabu la saba...jamani sasa tunategemea kupata product gani?

Hawezi kuwa na mapenzi na kazi yake hata kidogo...kikawaida walimu ilikuwa ni wito ulioambatana na motisha kutoka kwa wazazi,serikari etc...nakumbuka Mwadui Secodary miaka ya 1975-1980 Headmaster alikuwa anaona ni fahari shule yake wanafunzi kufaulu,walimu walikuwa karibu wote ni University Graduate Teachers...yaani hata kama maslahi ni madogo...ila wazazi walikuwa wanamsifia...serikari...sasa hivi..wazazi nao hata kuwapenda walimu hakuna kabisa...ilimradi anapesa anajua mwalimu atafanya lolote.
 
Kwanini somo la hisabati watu hufeli sana, yaani asilimia 75.67 wamefeli?
Na kila mwaka hisabati huongoza kwa kuwa na wanafunzi wengi waliofanya vibaya! Why?

Hii ni hatari kwa taifa letu, tukumbuke hisabati ndio msingi wa maendeleo kwa nchi yoyote ile, iwapo watu wanafeli hisabati, hapo ipo shida vilevile uwezekano wa kufeli masomo mengine ni mkubwa. na shindwa kuelewa ni kwanini watu kila kukicha ndio wanazidi kufeli hisabati, na hii si nchini kwetu tu hata kwa mataifa makubwa kama uingereza na marekani, kiwango cha kufaulu hisabati kinashuka kila siku. sasa je huku kufeli hisabati kunauhusiano na aina ya yakula tunavyo kula?
 
Kwanini somo la hisabati watu hufeli sana, yaani asilimia 75.67 wamefeli?
Na kila mwaka hisabati huongoza kwa kuwa na wanafunzi wengi waliofanya vibaya! Why?

Hii ni hatari kwa taifa letu, tukumbuke hisabati ndio msingi wa maendeleo kwa nchi yoyote ile, iwapo watu wanafeli hisabati, hapo ipo shida vilevile uwezekano wa kufeli masomo mengine ni mkubwa.hii inathibitishwa kwa matokeo ya mwaka huu ambapo kiwango cha kufaulu kimeshuka pia japo mitihani iliibiwa sana.nina shindwa kuelewa ni kwanini watu kila kukicha ndio wanazidi kufeli hisabati, na hii si nchini kwetu tu hata kwa mataifa makubwa kama uingereza na marekani, kiwango cha kufaulu hisabati kinashuka kila siku. sasa je huku kufeli hisabati kunauhusiano na aina ya yakula tunavyo kula?
 
Hivi kwa nini shule nyingi za wamisionari ndo zinatesa sana???
Ningeomba kutoa ushauri kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar wajitahidi sana kuajili waalimu wa kutosha toka huku Bara.Angalia shule nyingi za Zenj zimefanya vibaya.
 
Kiwango cha ufaulu kidato cha nne chashuka

SHULE 10 BORA NI BINAFSI, WAVULANA WAONGOZA

BARAZA la Mitihani la Taifa limetangaza matokeo ya mitihani ya taifa kwa watahiniwa wa kidato cha nne (F IV) kwa mwaka 2008 huku kiwango cha ufaulu kikishuka kwa asilimia 10 ikilinganishwa na mwaka 2007.

Pia, katika matokeo hayo, shule zilizoshika nafasi 10 za kwanza ni watu binafsi na mashirika ya dini kutoka Tanzania Bara, huku Zanzibar ikikosa hata shule moja katika kundi hilo, wakati shule 10 za mwisho zikiwa mchanganyiko wa zile zinazomilikuwa na watu binafsi na serikali, tatu kati ya hizo zikiwa ni za Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa ya Baraza la Mitihani ambayo imesainiwa na katibu mtendaji wake, Joyce Ndalichako, watahiniwa waliofanya mtihani ni 233,848 sawa na asilimia 96.84 ya waliosajiliwa wakati watahiniwa 7,624, sawa na asilimia 3.1, wakishindwa kufanya mtihani kwa mwaka 2008.

Kuhusu ubora wa kufaulu, wavulana wanaongoza kwa asilimia 3.22 dhidi ya 1.49 ya wasichana daraja la kwanza, wakati daraja la pili wavulana wakiwaacha tena wasichana kwa asilimia 5.86 dhidi ya asilimia 2.71 ya wasichana.

Ufaulu wa masomo ya lazima unaonyesha kuwa somo la Kiswahili linaongoza likiwa na asilimia 81.59 ya ufaulu, likifuatiwa na Kiingereza (63.23). Somo la siasa linashika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 62.09, likifuatiwa na jiografia (58.97) na la mwisho ni hisabati (24).

Katika matokeo hayo wavulana wanaongoza kwa asilimia 79.21 dhidi ya asilimia 72 ya wasichana kwa wanafunzi wa shuleni, huku wale wa kujitegemea wanaume wakiongoza kwa 62.65 dhidi ya asilimia 55.86 ya wanawake.

Watahiniwa 347 wamefutiwa matokeo yao kutokana na udanganyifu, ambao 192 ni wa watahiniwa wa shuleni huku 155 wakiwa wa kujitegemea.

"Idadi hiyo ni pungufu kulinganisha na ya mwaka 2007 ambapo jumla ya watahiniwa 597 walifutiwa matokeo, 526 kutoka shuleni na 71 wa kujitegemea," inaeleza taarifa ya Ndalichako.

Taarifa hiyo inazitaja shule 10 bora kuwa ni Shule ya Wasichana ya St. Francis (Mbeya), Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Marian (Pwani), Seminari ya St. Joseph-Kilocha (Iringa), Seminari ya Uru (Kilimanjaro) na Seminari ya Dungunyi (Singida).

Nyingine ni, Shule ya Wasichana ya Anwarite (Kilimanjaro), St. Mary Goreti (Kilimanjaro), Shule ya Wavulana ya Feza (Dar es Salaam), Seminari ya Don Bosco (Iringa) na Rosmini (Tanga).

Pia shule 10 bora zilizokuwa na watahiniwa chini ya 35 ni pamoja na Scolastica (Kilimanjaro), Feza (Dar es Salaam), Brookebond (Iringa), Bethelsabas (Iringa) na Seminari ya Maua (Kilimanjaro).

Nyingine ni Seminari ya Rubya (Kagera), Seminari ya St. Mary Junior (Pwani), Seminari ya Katoke (Kagera), Kilomeni (Kilimanjaro) na St. Carolus (Singida). Katika mtihani wa Maarifa (QT) watahiniwa 5,653- sawa na asilimia 27.02- ikiwa ni pungufu ya mwaka 2007 wakati asilimia 24.44 ya watahiniwa walifaulu.

"Hivyo kiwango cha ufaulu kwa mtihani wa maarifa kimeongezeka kwa asilimia 2.58 mwaka 2008 ikilinganishwa na mwaka 2007," inaeleza taarifa ya Ndalichako.

Oktoba mwaka 2008 jumla ya wanafunzi 233,848, sawa na asilimia 96.84 ya wanafunzi wa kidato cha nne nchini kote walifanya mtihani wao wa taifa.

Source : Mwananchi




Jamani mbona hakuna hata shule moja iliyoko katika kumi bora inayomilikiwa na Bakwata au shirika lolote la kiislam.Ukiangalia kwa makini shule nyingi zilizofanya vizuri ni za mashirika ya dini ya kikristo.
 
Jamani,

Kuna mtu ana haya matokeo? Naomba ayaweke kwenye mtandao ili nasi tuweze kuyapata. Huko sipati kitu - na hii siyo mara ya kwanza, bila shaka server yao imeelemewa tena.

Ingekuwa bora kama webmaster wao angekuwa anaweka matokeo kwenye server mbalimbali (hasa za Marekani au hata na Ulaya) ili kuepuka matatizo ya bandwidth wakati Watanzania wanapotafuta matokeo haya kwa mpigo.

Nashukuru kwa msaada wenu.

Cliff
 
Nimeshapata ufumbuzi. Website inafanya kazi sasa, na kwa msaada wa WinHTTrack nitawasaidia hata wakulima pale kijijini kwetu kupata matokeo.

Cliff


Jamani,

Kuna mtu ana haya matokeo? Naomba ayaweke kwenye mtandao ili nasi tuweze kuyapata. Huko sipati kitu - na hii siyo mara ya kwanza, bila shaka server yao imeelemewa tena.

Ingekuwa bora kama webmaster wao angekuwa anaweka matokeo kwenye server mbalimbali (hasa za Marekani au hata na Ulaya) ili kuepuka matatizo ya bandwidth wakati Watanzania wanapotafuta matokeo haya kwa mpigo.

Nashukuru kwa msaada wenu.

Cliff
 
Nimeshapata ufumbuzi. Website inafanya kazi sasa, na kwa msaada wa WinHTTrack nitawasaidia hata wakulima pale kijijini kwetu kupata matokeo.

Cliff
Umepata ufumbuzi gani? mi bado nahangaika, sijapata kitu...web ya NECTA naona imezidiwa....ebu nisaidie or kama vipi nataka matokeo ya St. Joseph Kilocha Seminary, Matola Seconday,Maghang Sec na Njombe Sec kama utaweza kuyaona hapo!

Cheers
 
Umepata ufumbuzi gani? mi bado nahangaika, sijapata kitu...web ya NECTA naona imezidiwa....ebu nisaidie or kama vipi nataka matokeo ya St. Joseph Kilocha Seminary, Matola Seconday,Maghang Sec na Njombe Sec kama utaweza kuyaona hapo!

Cheers

Nenda kwenye RUN andika cmd kisha ingia katika dos mode
ikifungua dos andika hivi: tracert The National Examinations Council of Tanzania then press enter
Itaanza ku Trace router then ikimaliza tu angalia router ya mwisho utaona ip adress kisha fungua kwenye command line uandike hivi: Ping NNNN.NNNN.NNNN.HHHH -t alafu press enter hizo NN na HH ni IP adress ya router ya mwisho baada ya ku trace. ukimaliza itaanza kuping then wewe minimize hizo dos zako na utaendelea kufungua page zako kwa speed nzuri tu bila matatizo.
Ni ngumu kidogo lkn kwa watu wa network wanaweza kuelewa kiurahisi sana.
 
Jamani hizi ni baadhi ya quotes ambazo naona zitaleta ugomvi hapa.

...
Jamani mbona hakuna hata shule moja iliyoko katika kumi bora inayomilikiwa na Bakwata au shirika lolote la kiislam.Ukiangalia kwa makini shule nyingi zilizofanya vizuri ni za mashirika ya dini ya kikristo.

Hongereni St......seminary.

Hivi hizi shule zetu za kiislamu zilizoamua kujiita seminary mbona bado hazifanyi vizuri? Kulikuwa na force fulani kutoka wizarani kuziita seminari au hilo wimbi la kuongeza neno "seminary" lilitokana na nini hasa! Anyway, ni nje ya mada. Samahani wakuu. Pengine nitaianzishia thread yake.

Serikali tafadhali ingilia kati suala la Elimu Visiwani...
 
Unajuwa mimi sikupenda kabisa mpangilio wao walivyoweka maana wamechanganya sana herufi bora wangepanga kwa herufi ingekuwa vizuri zaidi maana wamechanganya alafu shule ni nyingi sana sasa kama shule ingekuwa inaanzia na M ilibidi mtu unakwenda kwenye M kama shule inaanzia na S mtu unakwenda kwenye S lakini sasa hapo kuipata shule nadhani utachukua 1 hour mpaka upate shule unayotafuta..........Sijui wenzangu mnasemaje hapo!!
 
Kilimanjaro yafanya kufuru matokeo kidato cha nne

2009-02-09 10:10:02
Na Joseph Mwendapole


Shule za mkoa wa Kilimanjaro zimeongoza katika
kundi la shule 20 zilizofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne yaliyotangazwa jana na Baraza la Taifa la Mitihani, ambayo mwaka huu ufaulu ni wa asilimia 75.8.

Taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kusainiwa na Katibu Mtendaji wake, Dk Joyce Ndalichako, jumla ya watahiniwa 233,848 walifanya mtihani huo Oktoba mwaka na waliofaulu ni 168,420.

Katika kundi la shule 20 bora zenye watahiniwa zaidi ya 35 na chini ya 35, mkoa wa Kilimanjaro umeingiza shule sita, ukifuatiwa na Iringa ambayo imeingiza shule nne Dar es Salaam, Singida, Pwani na Kagera zikiingiza shule mbili kila moja. Wakati Mbeya na Tanga zimeingiza shule moja kila moja.

Dk. Ndaliachako katika taarifa yake kinyume cha miaka ya nyuma ambayo hakufanya mkutano na waandishi wa habari kutoa tangazo hilo muhimu, imezitaja shule kumi bora zenye watahiniwa 35 au zaidi kuwa ni sekondari ya wasichana ya St. Francis ya mkoani Mbeya iliyoshika nafasi ya kwanza Marian Girls ya Pwani nafasi ya pili St. Joseph-Kilocha Seminari ya Iringa nafasi ya tatu Uru Seminari ya Kilimanjaro nafasi ya nne na Seminari ya Dungunyi mkoani Singida nafasi ya tano.

Nyingine ni Sekondari ya Wasichana ya Anwarite ya Kilimanjaro nafasi ya sita St. Mary Goreti ya Kilimanjaro nafasi ya saba Sekondari ya Wavulana ya Feza ya jijini Dar es Salaam nafasi ya nane Seminari ya Don Bosco ya Iringa nafasi ya tisa na sekondari ya Rosmini ya Tanga bafasi kumi.

Taarifa hiyo ilitaja shule kumi bora zenye watahiniwa chini ya 35 kuwa ni sekondari ya Scolastica ya Kilimanjaro iliyoshika nafasi ya kwanza.

Feza Girls ya Dar es Salaam nafsai ya pili
Brookebond ya Iringa nafasi ya tatu Bethelsabas Girls ya Iringa nafsai ya nne Maua Seminari ya Kilimanjaro nafasi ya tano Rubya Seminari ya Kagera nafasi sita St. Mary`s Junior seminari ya Pwani nafasi ya saba Katoke Seminari ya Kagera nafasi ya nane Kilomeni Sekindari nafasi ya tisa na St. Carolus ya Singida nafsai ya kumi.

Taarifa hiyo ilitaja shule kumi za mwisho zenye watahiniwa 35 au zaidi ambazo zimepangwa kuanzia ya kwanza hadi ya mwisho kuwa ni: Selembala ya mkoani Morogoro Kilindi ya Pemba Ngwachani ya Pemba Michiga mkoani Mtwara Ummussalama ya Pwani Chunyu ya Dodoma Busi Dodoma Uondwe pemba Nala ya Dodoma na Maawal ya mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo shule kumi za mwisho zenye watahiniwa chini ya 35 ni Juhudi Academy ya Zanzibar, Mima ya Dodoma, Selenge ya Singida, Kijini ya Zanzibar, Kwamkoro ya Tanga, Kwala ya Pwani, Mtende ya Zanzibar, Ng\'oboko ya Shinyanga, Mbuzini ya Pemba na Sekondari ya Ufundi ya Mwadui Shinyanga.

Kati ya waliofaulu wasichana ni 76,472 na wavulana ni 91,948 na waliofeli mitihani hiyo ni 65,428.

Taarifa hiyo inaonyesha kuwa kuna ongezeko la watahiniwa 3,284 waliofaulu mtihani huo ikilinganishwa na idadi ya waliofaulu mwaka jana.

Hata hivyo, taarifa hiyo ilisema kuwa asilimia ya ufaulu inaonyesha kushuka kwa asilimia 10 kutoka asilimia 85.9 ya mwaka juzi hadi asilimia 75 kwa mwaka jana.

Katika ubora wa ufaulu, wavulana wameongoza kwa waliopata daraja la kwanza na kuwaacha wasichana mbali.

Takwimu za Baraza hilo zinaonyesha kuwa wavulana waliopata daraja la kwanza ni 3,743 wakati wasichana ni 1,578.

Katika matokeo ya mwaka 2007 wavulana waliopata daraja la kwanza walikuwa 4,349 wakati wasichana walikuwa 1,900.

Taarifa hiyo ilisema watahiniwa 41,018 waliofanya mtihani wamefaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu ikilinganishwa na watahiniwa 44,348 waliopata madaraja hayo mwaka 2007.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu katika masomo ya lazima, wavulana wameongoza katika kufaulu wakiwa ni 56,172 ikilinganishwa na wasichana 40,459 waliofaulu.

Katika somo la Hisabati wavulana waliofaulu ni 26,532 kati ya watahiniwa 85,625 wavulana waliofanya mtihani huo, wakati wasichana waliofaulu ni 11,145 kati ya wasichana 69,214 waliofanya mtihani huo.

Kwa upande wa somo la Kingereza wavulana waliofaulu ni 57,122 kati ya wavulana 86,158 waliofanya mtihani huo, wakati wasichana waliofaulu ni 41,314 kati ya wasichana 69,522 waliofanya mtihani huo.

Katika somo la Baiolojia wavulana waliofaulu ni 46,183 kati ya wavulana 85,510 waliofanya mtihani huo, wakati wasichana waliofaulu ni 25,385 kati ya 69,121 waliofanya mtihani huo.

Wavulana wameendelea kuongoza pia katika somo la Kiswahili ambapo waliofaulu somo hilo ni 69,051 kati ya wavulana waliofanya mtihani huo na wasichana waliofaulu ni 57,960 kati ya 69,512 waliofanya mtihani huo.

Kwa upande wa somo la Jiografia wavulana waliofaulu ni 55,449 kati ya wavulana 86,002 waliofanya mtihani huo wakati wasichana waliofaulu ni 36,256 kati ya wasichana 69,505 waliofanya mtihani huo.

Taarifa hiyo ilionyesha kuwa wavulana wameongoza pia katika somo la Civics ambapo waliofaulu walikuwa 56,172 kati ya wavulana 86,112 waliofanya mtihani huo, wakati wasichana waliofaulu ni 40,459 kati ya wasichana 69,527 waliofanya mtihani huo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ufaulu kwa masomo unaonyesha kuwa watahiniwa wamefanya vizuri zaidi katika somo la Kiswahili ambapo asilimia 81.5 ya watahiniwa wamefaulu.

Ufaulu katika somo la Hisabati uko katika kiwango cha chini ambapo ni asilimia 24.3 tu ya watahiniwa waliofaulu somo hilo.

Baraza hilo limesitisha matokeo ya watahiniwa 5,135 ambao hawajalipa ada ya mtihani na kwamba yatatolewa mara watakapolipa.

Pia limesitisha matokeo ya watahiniwa 495 kutokana na wakuu wa shule husika kutolipa ada ya watahiniwa pungufu ya 35 hadi hapo watakapolipa ada wanayodaiwa.

Baraza hilo pia limefuta matokeo ya watahiniwa 347 kwa kubainika kufanya udanganyifu katika mitihani.

SOURCE: Nipashe
 
Last edited by a moderator:
Unajuwa mimi sikupenda kabisa mpangilio wao walivyoweka maana wamechanganya sana herufi bora wangepanga kwa herufi ingekuwa vizuri zaidi maana wamechanganya alafu shule ni nyingi sana sasa kama shule ingekuwa inaanzia na M ilibidi mtu unakwenda kwenye M kama shule inaanzia na S mtu unakwenda kwenye S lakini sasa hapo kuipata shule nadhani utachukua 1 hour mpaka upate shule unayotafuta..........Sijui wenzangu mnasemaje hapo!!

Mkuu Yasin ni kweli inasumbua, wangepanga katika "alphabetical order" ingekuwa rahisi. Fanya hivi, ukitaka pata shule kwa urahisi, mfano hiyo shule inaitwa TABORA, basi bonyeza "control+F" (ninamaana anza kubonyeza "control key" na bila kuachia bonyeza F), ingiza jina la shule yako katika sehemu "Find", halafu bonyeza next, itatafuta shule yenye jina TABORA, sasa kama ziko nyingi (Tabora boys, Mzee Tabora, Tabora) utakuwa unaangalia mpaka uipate unayoitaka.
 
Kilimanjaro wako Wachaga peke yao kwa kuangalia makabila, na Wapare jee?, lakini kwa TZ bado katika hizo shule hata kama wengi wao watakuwa ni makabila ya Kilimanjaro, bado kuna idadi tosha ya makabila mengine toka sehemu mbalimali ya TZ.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom