Mateso ya udahili wa wanafunzi vyuoni yameanza kuonekana

Ndugu yangu ondoa hii imani iliyojaa kwenye mawazo ya watanzania wengi "ukiona mtu ana mtazamo tofauti na wewe mnasema ametumwa" kadri miaka inavyoenda akili na uelewa wa watu hasa vijana unapungua.
Umeongea point mkuu, hila mambo kama hayo hayakosi
 
Mfumo wa udahili wa pamoja kwa njia ya mtandao ulitengenezwa kutokana na tafiti zilizofanyika kuhusu manufaa yake katika kuwapunguzia wanafunzi na wazazi gharama za kutafuta, kuomba, na kujiunga na vyuo hapa nchini. Kuutengeza mtandao huu ulitumia gharama kubwa hadi uweze kutumika.

Baada ya kuachana na mfumo huu hivi sana wanafunzi wameanza kuonja joto ya jiwe. Application form sasa ni sh. 50000. Ukitaka kuwa na uhakika wa kupata nafasi chuoni huna budi ufanye applications kwenye vuo 3 au zaidi
Yamekua hayo wakuu
 
Japokuwa TCU walikuwa na mapungufu yao lakini walijitahidi kadiri walivyoweza kudahili wanafunzi wenye sifa hata kwa wengine kupangiwa vyuo ambavyo hawakuviomba kabisa. Pia waliweza kudhibiti kwa kiasi chake mianya ya rushwa na upendeleo wa kikabila na udini katika udahili.

Kuruhusu udahili vyuoni moja kwa moja ni kutaka kufungua mianya ya rushwa na upendeleo wa kikabila na udini katika udahili na kufahamiana. Kuna watu wasiokuwa na sifa lakini wana uwezo kiuchumi watahonga ili wapate nafasi na kozi wanazozitaka pia upendeleo wa kikabila na kidini.

Na ili mwanafunzi ajihakikishie nafasi itambidi achukue fomu zaidi ya chuo kimoja hivyo kuongeza gharama za application. Wakati wa TCU hela unayoilipia unajaza vyuo vitano.

Je huyu mtoto wa maskini atakuwa na uwezo wa kukusanya fomu zaidi ya moja au je ataweza kuhonga ili apate nafasi?

Ni mtazamo wangu tu. Nadhani wale waliopata vyuo enzi za matriculation wanayajua haya.
Natamani wahusika waje kuona post kama hizi na wafanyie kazi maoni ya wadau
 
Acha kupotosha watu yan kila chuo kina gharama yake, ngoja nitaje nilizoona, mwalimu nyerere Memorial - 30000,cbe-35000 , NIT-50000 kwa haraka nimeona acha panic subir hiyo tarehe 22/7 vyuo vyote wakianza kupokea ndo ulalamike... Acha kuwatetea TCU wezi tu me nilipangiwa chuo ambacho xikujaza naenda TCU wananionaje cjui akati mimi ndo nilikuwa nakesha kuitafuta one

Kwamba na ONE yako ukapangwa chuo ambacho hukuchagua?

Siamini

Ninachojua,CAS imesaidia sana watoto wa masikini wenye matokeo mazuri kutimba vyuo vikuu vya taifa kama UDSM,MUHAS,SUA etc
 
Acha kupotosha watu yan kila chuo kina gharama yake, ngoja nitaje nilizoona, mwalimu nyerere Memorial - 30000,cbe-35000 , NIT-50000 kwa haraka nimeona acha panic subir hiyo tarehe 22/7 vyuo vyote wakianza kupokea ndo ulalamike... Acha kuwatetea TCU wezi tu me nilipangiwa chuo ambacho xikujaza naenda TCU wananionaje cjui akati mimi ndo nilikuwa nakesha kuitafuta one
Sawa kwa hizo data zako nadhani mfumo huuu mpya utawagharimu sana hasa watanzania wenye kipato cha chini!!!! Kwan kama ukijaribu kufanya maombi kwa vyuo vitatu itagharimu takribani tsh 90000.Kiufupi hali itakuwa ngumu sana.
 
Vyuo vitano na round tano namba imehamia kwenye udahili sasa me nilijua mapema hii ni njia mpya ya kukusanya hela tu :D :D :D :D TCU walikua na mapungufu yao ila walikua na msaada mkubwa kwa kweli na hata kama waliplka watu vyuo hawavitaki mbona walikuwa wanatoa nafasi ya kuhamia unapopataka
Exactly!!!!!!!
 
K
Kuapply chuoni direct bado Ni rahisi , assume umeapply vyuo vitatu vyenye application sh 35,000 per chuo *3 equal to 115,000 - tcu gharama 50,000equal to 65,000 incremental cost , mtu aliyeapply direct amechaguliwa vyuo vya mkoa anaoishi, eg DSm, so there no need of bus fares, mtu wa tcu amepelekwa songea , nauli ya songea 32500 *2 equal to 65,000, so tcu root and direct appl all have 115000, incremental Ni zero kwa likizo moja Tu. Nategemea utasafiri songea zaidi ya mara tano mpaka unamaliza chuo , kwa hiyo 32500 *2*4equal to 260,000 loss (cost to tcu appl channel or saving to direct to school appl channel , kwa hiyo sio kweli kwamba ukiapply via tcu ni rahisi kuliko direct ,hapo sijaweka hidden cost mfano kuchoka ,etc
Assume pia competition imekua kubwa, uliko omba kote umekosa, inabd usubiri mwaka mwingine wa masomo na kumbuka huo mwaka kuna watu wanamaliza shule kuna balaa la huo mwaka wanafunzi kuwa na ufaulu mkubwa, utajikuta umeenda songea mwenyewe bila kupenda... Kama mwanzo opportunity cost ilikua zero sasa itaongezeka in terms of time wastage kama tukisema tuangalie factors nyingne tofauti na financial factors.
 
Wangapi wanaishi mikoa yenye vyuo ili iwe kama unavyosema?
Wakat wengi wakitazamia kujiunga udsm wahitimu wangap wanaoishi Dar?
Umejitahidi kuandika ila kwa upande wangu naona hamna mantik au labda unieleweshe vzr kwa kunijib maswal yangu hayo
Exactly!!!!!
 
Nilimsikia Rais juzi akizuia kila wizara kujenga "data center". Wazo zuri kwa maana ya kupunguza gharama na kuongeza ufanisi.

Same logic should apply kwa CAS ya TCU. Wangeweza kulink mfumo huo wa CAS na ile wa mikopo kwa ufanisi zaidi. Hii ya kila chuo kuwa ba "CAS" yake ni kurudi nyuma miaka 15.
 
100% ni hasara tu na kupotezeana mda certificate elf20 ulichagua vyuo vi3 leo hii NIT elf30 CBE 25 IfM 20 kuna na vyengine cjui bei gan huko na degree elf50 uliomb vi5 kwa round 5 saiv ni per university tunarud nyuma baada ya kwenda mbele cjui nani ameiroga Africa ttzo kubwa ni kwamba kila anaekaa anakuja na lake hakuna muendelezo wa maendeleo mwenangu amejenga barabara mm najenga kituo cha afya ni vurugu mechi tu amejenga barabara mwengine anakuja anavunja anaanza upya mpaka lini tutaishia kunawa tu
Kuna watu wametumia fursa kwa manufaa yao. Wana ushawishi mkubwa sana katika siasa za Tanzania. Walilaani udahiri wa TCU kwa maslahi yao
 
Acha kupotosha watu yan kila chuo kina gharama yake, ngoja nitaje nilizoona, mwalimu nyerere Memorial - 30000,cbe-35000 , NIT-50000 kwa haraka nimeona acha panic subir hiyo tarehe 22/7 vyuo vyote wakianza kupokea ndo ulalamike... Acha kuwatetea TCU wezi tu me nilipangiwa chuo ambacho xikujaza naenda TCU wananionaje cjui akati mimi ndo nilikuwa nakesha kuitafuta one
Gud
 
Kwa upande wangu mimi sijaona tatizo la CAS lilikua nini wakati kabla ya kuselect chuo unachotka kuna statement inakuambia unachochagua kiwe right choice kwa maana ata ukapelekwa chaguo la mwisho emechagua utakuwa uchizi unachagua medicine huna vigezo na huipendi unaieka tu au vigezo unavyo ila huipendi unaieka bahat nasibu umepewa hiyo unamlaumu nani wakat umechagua muhimu umepata chuo na course hamia unayoitaka nafac zipo wazi kuna watu wanafkir kama huu mfumo watu

hawatoachwa watatemwa sana tu kutokana na kujaa kwa wanafunz na huezi kujua wanataka watu wangapi na wameomba wangapi nisiri yao tu utaomba watachukua kiasi chao wengine watakaa pembeni udahili umefungwa unasubir mwakan
Wapo wamiliki wa vyuo binafsi wanalalamika eti CAS ilikuwa inawazuia kudahiri wanafunzi wengi wa aina fulani (dini, kabila, kanda, kipato) na kuwaleta wanafunzi wengi wa aina fulani (dini, kabila, kanda, kipato, kiwango cha elimu) bila hiari yao. Wakajikuta wanatoa elimu kwa watu wengi wasiokusudiwa na sera zao na kuwakosesha nafasi walengwa.
 
Back
Top Bottom