Mfumo shindani wa udahili wa wanafunzi sasa hivi unafanya vyuo kudahili wanafunzi bila ridhaa yao

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Kwanza napenda kutoa shukrani za dhati kwa Mh.Waziri @wizara_elimutanzania Prof. @professoradolfmkenda , baada ya kupokea malalamiko mengi juu ya wanafunzi kuthibitishiwa na kudahiliwa bila ridhaa yao katika Program (Kozi) na vyuo ambavyo hawakuomba wala hawakuthibitisha .

Haraka sana niliandika changamoto hii, pia nikamfikishia Mh.Waziri wa Elimu Prof.Mkenda usiku na akaahidi kutatua changamoto hii haraka leo, binafsi nampongeza kwa uwajibikaji huu .

Wanafunzi wawili niliyopokea malalamiko yao kuhusu udahili ,mwanafunzi aliyethibitishwa bila ridhaa yake na aliyedahiliwa bila ridhaa yake katika vyuo na kozi ambazo sio chaguo lake , na hivyo Mfumo kuwazuia kuomba vyuo vingine, hatimaye leo wameondolewa katika vyuo hivyo na mfumo umewaruhusu kuomba vyuo vingine na tayari wameomba vyuo vingine katika awamu hii ya pili. Natamani wanafunzi wote waliofanyiwa mchezo huu wa hovyo na vyuo vya namna hii, waondolewe katika vyuo hivyo na wawe huru kwenye mfumo kuomba vyuo vingine wanavyotaka kabla dirisha la pili kufungwa ,pia serikali kupitia TCU itoe muda wa ziada kwa wanafunzi watakao kosa vyuo pia.

Pia TCU leo wameongea na wameonesha concern juu ya changamoto hizi na kutoa Rai kwa vyuo kuacha kuthibitishia wanafunzi.

Lakini pia serikali kupitia Wizara na TCU iangalie suala hili kuna namna taarifa za wanafunzi zinavujishwa kwa vyuo kadhaa na hivyo wanafunzi kuombewa au kudahiluwa bila ridhaa yao.

Sababu huyu mwanafunzi
Haji Juma Rehan ana One ya 7.

Chemistry -B,Physics -B, biology -C

Vyuo vyote ambavyo ni chaguo lake aliomba ila alikosa sababu alionekana ameomba na amedahiliwa chuo cha St. Augustine Campus ya Arusha , Program ya Bachelor of Science in Tourism ,ikiwa hajaomba na hajui kuhusu hiyo Program na hicho chuo na hata akaunt ya maombi katika hicho chuo hana na hajawahi kutengeneza akaunti.

Hivyo,mbali na mchezo wa vyuo kumthibitishia mwanafunzi bila ridhaa yake ,kuna mchezo mwingine vyuo hivi vinafanya kugombea au kudahili wanafunzi katika chuo bila ridhaa yao .

Sababu mambo Muhimu katika udahili wa mwanafunzi katika Mfumo wetu wa udahili ni namba ya kidato cha nne na kidato cha sita ,namba hizi zikiingizwa katika mfumo taarifa zote na Matokeo ya mwanafunzi yanatokea . (Kuna namna Mfumo wetu uboreshwe , namba ya kidato cha nne na sita isiwe taarifa toshelezi kwa mwanafunzi kudahiliwa ,hili TCU walione na serikali kupitia Wizara ya Elimu).

Sasa kuna wasiwasi taarifa hizi za wanafunzi vyuo hivi wanazo , hasa namba ya kidato cha nne na kidato cha tano ,sababu vyuo hivi huwa vinatembelea wanafunzi katika shule zao muda mfupi kuelekea kwenye mtihani kidato cha 6 ,kutangaza vyuo vyao na kuna fomu wanafunzi wanapewa wajaze taarifa zao ,na pia inawezekana pia uongozi wa shule una husika kwenye kutoa taarifa za wanafunzi kwa vyuo hivi hasa namba ya kidato cha nne na kidato cha sita .

Sababu huyu Mwanafunzi Haji Juma Rehani alisoma Tanga Tech ,na hawa Saut Campus ya Arusha waliomdahili waliwahi tembelea shule hiyo Tanga Tech na kujazisha wanafunzi taarifa.

Lakini pia vyuo hivi huwa vina wafuata wanafunzi Jeshini , kutangaza vyuo vyao wakati wanafunzi wapo Jeshini JKT (Kwa mujibu wa sheria) na wanafunzi wanaombwa taarifa.

Ushauri wangu kwa serikali (Wizara ya Elimu) binafsi sioni haja ya vyuo hivi kwenda kufanya matangazo na udalali wa vyuo vyao shuleni kwa wanafunzi au JKT ,sababu tayari kuna muongozo wa TCU kwa wanafunzi, wanafunzi wasisitizwe kusoma muongozo na sio kutoa taarifa zao kwa mazingira ya namna hiyo.

Na wajibu wa kutoa Elimu kwa wanafunzi ni wajibu wa TCU sio vyuo kuwafuata wanafunzi, kufanya hivyo ni kugeuza taasisi hizi kama shule na Makambi ya Jeshi kuwa maeneo ya matangazo ya biashara kwa vyuo,lakini pia mtindo huu huchangia changamoto hii ya taarifa wanazoombwa wanafunzi baadaye zinatumiwa na vyuo hivyo kuwadahili wanafunzi bila ridhaa yao.

Mfumo huu wa sasa wa udahili ,ni Mfumo shindani unafanya vyuo kadhaa hasa vyuo binafsi kuwa na hofu ya kukosa wanafunzi hivyo kutumia njia zote ,wajuazo ili kupata wanafunzi hivyo ni vyema pia serikali kupitia Wizara kujua hali hii ili kukabiliana na michezo yeyote mibaya ya vyuo hivi dhidi ya wanafunzi.

Abdul Nondo.
 
Back
Top Bottom