DOKEZO Wanafunzi wa Muhimbili tulioomba mkopo kwa Diploma hatujapata, HESLB wapo kimya na Udahili unafungwa wiki ijayo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Habari Wana Jamii Forums naomba kuwasilisha hoja yangu ili kupaza sauti, mamlaka zisikie na ikiwezekana hatua zichukuliwe haraka.

Sisi Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi. Muhimbili (MUHAS) tunaojiunga au tunaotarajiwa kujiunga katika masomo ya Shahada ya Kwanza kutokea Ngazi ya Diploma hatuzingatiwi kabisa na Bodi ya Mikopo (HESLB) wakati wengi wetu Diploma yenyewe tumesoma kwa kuchangiwa na ndugu na wazazi, baadhi ni kwa kukopa huku na kule, mpaka tukamaliza.

Tunategemea Serikali itushike mkono ili tuweze kuendelea lakini inatusahau kaka, nina wenzangu tuliotoka Diploma tumepata nafasi ya MUHAS lakini hakuna aliyepewa mkopo kwa waliotokea Diploma.

Ada ya Shilingi Milioni 1.8 ni kubwa kwetu, tunaomba Bodi ya Mikopo (HESLB) watupunguzie walau nusu basi maana mpaka sasa wengine bado hatujaripoti chuo kwa kuwa hatuna hiyo nusu ya ada kwa ajili ya udahili, mwisho wa udahili ukifika tunakuwa tumepoteza hiyo nafasi.

Ikiwa mchakato huo utakuwa unashindikana ni kheri wangekuwa Wanaweka watu wazi kwamba umepata au umekosea kuliko kumtia mtu moyo ‘for nothing’ maana kama unaweza kumwambia ‘your application is verified complete wait for allocation process’ hii inamaana wamepitia documents, wameona kuna vigezo ndio maana wamemwambia asubirie allocation process, ajabu wanabadilisha wanaandika ‘your application is being processed wait for final results’

Ujumbe wa aina hiyo wameandikiwa waombaji wote ambapo wamekamilisha maombi, kitakachotokea watu tutanyimwa mikopo (imebaki wiki moja ya udahili) kisha tukose masomo na tutalazimika kusubiri mwakani.

Kibaya zaidi hawawezi wazi kama mtu umekosa mkopo na kwa vigezo vipi?

Bora wangeweka wazi mapema ili kama kuna mtu anatafuta mpango mbadala afanye hivyo mapema kabisa.

Ukitaka kuamini hilo kupitia akaunti ya HESLB wenyewe ambao wameweka tangazo la kuelezea watu waliopata mikopo, comments nyingi watu wanalalamika kuwa hawajapata mikopo, inamaana waliopata wote hawatumii Istagram au mitandao ya kijamii, mbona hawasemi chochote!

Wanafunzi wa MD na DDS ambao wamepata mkopo katika Chuo cha MUHAS ambao entry qualifications yao ni Diploma, hakuna kama wapo basi watakuwa wachache sana.

Ukitaka kujua pia kuna shida, HESLB hawatoi majina ya walionufaika na mkopo huo kutokea katika Diploma, wanaishia kusema kwa namba za jumlajumla.

Ikiwa Serikali imetenga fedha kweli za mkopo kwa Wanafunzi wa Diploma na hatupati basi TAKUKURU wanatakiwa kuingialia kati na kufuatilia kinachoendelea.
 
mkopo kwa ajili ya watu wa diploma ni kwa ajili ya watu wanaosoma ngazi ya diploma sio waliotoka diploma.alietoka diploma wanaku consider as equivalent sawa na mtu wa form six.so mkopo wako upo ndan ya zile bil731 na sio 48bil za wat wa diploma
 
mkopo kwa ajili ya watu wa diploma ni kwa ajili ya watu wanaosoma ngazi ya diploma sio waliotoka diploma.alietoka diploma wanaku consider as equivalent sawa na mtu wa form six.so mkopo wako upo ndan ya zile bil731 na sio 48bil za wat wa diploma
Inaeleweka hyo shida ni kwamba hakuna taarifa znazoweka wazi kama umepefa au umekosa
 
Back
Top Bottom