JaxenDL
JF-Expert Member
- May 17, 2022
- 976
- 2,301
Mwanangu mmoja alikuwa anasoma Muhimbili MD, yupo mwaka wa pili. Sasa wakati mimi napiga zangu field pale Sinza Palestina, siku moja kwenye pita-pita zangu nikakutana naye. Mawasiliano tukapiga story nyingi, maana kitambo hatujaonana. Nikamwambia, “Weekend moja nitaenda kukusalimia Campus yenu ya MUHAS kule Chole Road.”
Siku hiyo nimeenda, jamaa akaanza kunipa michongo ya ujasiriamali na kampuni wanaiita QNET 😅. Akanipa ramani nzima ya sehemu walipo, akaniambia kesho niende kwa ajili ya interview ya kwanza. Walikuwa wamekodi nyumba fulani pale Sinza Kijiweni.
Kesho yake nimetoka zangu hospitali Sinza, pale mida ya saa 8 mchana. Nikamcheki mwanangu, twende kwenye hiyo interview. Akanielekeza mpaka tukafika eneo la tukio.
Ile nafika tu, napokelewa na “Good morning.” Nikashtuka, sikuelewa nijibu nini 😂. Halafu wananiita kwa jina langu! Mwanangu akasema, “Usiwe na wasiwasi, ndo salamu za kampuni hizo.”
Sasa akanikutanisha na boss wao. Nilipomwona tu usoni nikamkumbuka, kumbe tumesoma naye Pandahill. Basi tukaenda ofisini, akanipa maelekezo kibao. Mara sijui QNET wameidhamini hadi Man City 😂.
Kisha baadaye akaja kusema, “Hii ni interview ya kwanza. Kesho muda kama huu huu uje kwa ajili ya interview ya pili, ambayo ndiyo utasajiliwa na kuanza kulipwa.”
Natoka tu nje, nakuta wananipigia makofi watu kibao pale sebuleni, ambao hata mwanzoni hawakuwepo 😂. Na wengine ndio naanza kuwaona ni watu tuliosoma nao Pandahill. Wanasema, “Hongera sana!” 😂😂
Basi tukatoka na mwanangu ananisindikiza, huku anasisitiza, “Kesho hakikisha unakuja mwanangu.” 😅
Nilivyofika maskani, nilicheka sana nilichoshuhudia siku hiyo. Kesho yake mchana jamaa alipiga simu nyingi sana, sikupokea.
Urafiki ukafa.
Ila cha kushangaza, milima haikutani, lakini binadamu tunakutana 😅.
Mwaka 2023, kipindi nafanya kazi Dodoma, nikaja kukutana naye UDOM. Yupo mwaka wa pili tena MD kule Muhimbili, alifeli 😅.
QNET imeharibu ramani za maisha ya vijana wengi sana.
Ukimleta mtu mmoja na yeye akimleta mtu , huku tayari wewe utakua unaingiza laki mbili kwa wiki.
Na kazi hii unaifanya online ata ukiwa nyumbani