Matajiri wa Moshi miaka ya 90 hadi 2000's

jmushi1 ni kweli kuwa utajiri wa Kidumbuyo ulitokana na fedha alizopora mto karanga kwenye ajali ya basi la Safina?
Naskia kulikuwa na waarabu kwenye ile ajali walikuwa na fedha nyingi sana na Kidumbuyo alikuwa mmoja ya watu wa kwanza kufika baada ya ajali kutokea
Thomaa Kidumbuyo unamjua mkuu mzee fulani ni Mushi Kama wewe aliishi kibosho, nadhani biashara ilivokuwa tight ya blanket alirudi nyumbani na kuendelea kupambana na ufugaji pia alikuwa ana butcher za nyama nyingi sana, watoto wake saivi wako poa pia, naona alipewa Prado yeye anabebea migomba, na mbolea...
 
jmushi1 ni kweli kuwa utajiri wa Kidumbuyo ulitokana na fedha alizopora mto karanga kwenye ajali ya basi la Safina?
Naskia kulikuwa na waarabu kwenye ile ajali walikuwa na fedha nyingi sana na Kidumbuyo alikuwa mmoja ya watu wa kwanza kufika baada ya ajali kutokea
Ni mwingine, yeye alikuwa bwana mdogo kabisa. Ameshafariki lakini, jina limenitoka, nikikumbuka ntakujulisha. Alikuwa kama na makengeza flani hivi! Alitajirika kwenye ile ajali. Ila ule mto karanga una historia ndefu!😀
 
Habari za mida wana jf

Kipindi nakuwa moshi town pale wenyewe wanapaita mji wa wagumu, kulikuwa na matajiri wanajulikana na kusifika sana.
Walikuwa maarufu sana hadi makanisani.Ukienda kanisani ukimwona hata mke wake unabaki waooo
Walikuwa hadi na siti zao kristu mfalme pale.waliishi uzungun,wengine njia ya old moshi.

Kuna siku tumeenda nyumbani kwa rafiki yetu mmoja tulikuwa tunasomanaye mafundisho kanisan maeneo ya uzunguni kule,huo mjumba looh tulibak mdomo wazi.Na ilikuwa first time naona swimming pool nyumban.

Anyway zama zimepita, wengi wameaga dunia,wengine wapo ila umaarufu sio kama zamani.Nilikuwa natoka familia ya kikapuku kabisa so nilitaman siku moja at least na sisi family yetu iweze kuwa na jina kama family zile ama hata visenti tu.

Kuna mzee mmoja alikuwa maarufu sana hapo moshi town,alikuwa na maduka,garages,mabar,mabasi na biashara kibao.Alikuwa anaheshimika kama mfanyabiashara mkubwa moshi.Na wengi tuliamini hivyo.Bwana weeh siku moja katika harakati zake,akapatwa na majanga kwenye mbuga za Kenya, akapigwa risasi akafa,wenzie walifanikiwa kukimbia.Ikaja fahamika mzee alikuwa mwindaji haramu kwenye mbuga ya tsavo,alikuwa anawinda tembo na kuuza pembe na ndio ulikuwa siri ya utajiri wake.

Alirudishwa moshi akaenda zikwa kwao migombani ,after wards Mali zile zikayeyuka kama barafu. Since then nikajifunza kutokutamani cha mtu kwani hujui kakipataje. Utajiri una siri kubwa so vijana wenzangu tufanye kazi.Usiamini story za nilianza na kushona viatu stend,huwa hawasemi ukweli.
mzee Oraa, alikuwa mwizi wa magari, baadae akawa na kwik communication, hivi bado ni fogo?
 
eeh bhana alikuwa na watoto wake Bruno na nani sijui, siku hizi mwanae ana Rhidah club pale KDC, njiwa naye mambo yalikwenda kombo wanawe ndio waapambana
Mzee bado yupo anapambana japo uchumi umeyumba kidogo lakini kuna amani ipo.Brono,, justin wapo
 
Jani mhindi wa chaulo, bagia na koni hatari Sana nilikuwa nasoma mawenzi ps mapumziko ya 4 asb fasta kwa Jani tunachanga mpaka ifike Mia na 50 kula bagia au chaulo
 
Habari za mida wana jf

Kipindi nakuwa moshi town pale wenyewe wanapaita mji wa wagumu, kulikuwa na matajiri wanajulikana na kusifika sana.
Walikuwa maarufu sana hadi makanisani.Ukienda kanisani ukimwona hata mke wake unabaki waooo
Walikuwa hadi na siti zao kristu mfalme pale.waliishi uzungun,wengine njia ya old moshi.

Kuna siku tumeenda nyumbani kwa rafiki yetu mmoja tulikuwa tunasomanaye mafundisho kanisan maeneo ya uzunguni kule,huo mjumba looh tulibak mdomo wazi.Na ilikuwa first time naona swimming pool nyumban.

Anyway zama zimepita, wengi wameaga dunia,wengine wapo ila umaarufu sio kama zamani.Nilikuwa natoka familia ya kikapuku kabisa so nilitaman siku moja at least na sisi family yetu iweze kuwa na jina kama family zile ama hata visenti tu.

Kuna mzee mmoja alikuwa maarufu sana hapo moshi town,alikuwa na maduka,garages,mabar,mabasi na biashara kibao.Alikuwa anaheshimika kama mfanyabiashara mkubwa moshi.Na wengi tuliamini hivyo.Bwana weeh siku moja katika harakati zake,akapatwa na majanga kwenye mbuga za Kenya, akapigwa risasi akafa,wenzie walifanikiwa kukimbia.Ikaja fahamika mzee alikuwa mwindaji haramu kwenye mbuga ya tsavo,alikuwa anawinda tembo na kuuza pembe na ndio ulikuwa siri ya utajiri wake.

Alirudishwa moshi akaenda zikwa kwao migombani ,after wards Mali zile zikayeyuka kama barafu. Since then nikajifunza kutokutamani cha mtu kwani hujui kakipataje. Utajiri una siri kubwa so vijana wenzangu tufanye kazi.Usiamini story za nilianza na kushona viatu stend,huwa hawasemi ukweli.
Wachaga wengi utajiri wao ulikuwa wa kupora na ujambazi. Wengi wao Wana utajiri wenye ukakasi
 
Kuna mmoja alipata ajali mbaya njia ya moshi-arusha akafa papo hapo. Kilichofuta mali zake zilipukutika kama majani makavu kwa sababu hata mke wake hakuwa anazifahamu mali nyingi za mumewe.
Huyu sio Yule ambaye mke wake alikufa Kabla ya yeye kupata ajali?
 
Inasikitisha…

Watoto ndio hupata shida sana kwani wengi wao unakuta walilelewa kama mayai kipindi mamboa kiwa swafi.
Sasa hali inapobadilika ghalfla, wengi wao huishia kukata tamaa ya maisha ikiwa na kukacha masomo yao na mwisho wa siku kuja kuwa watu huni mitaani (umalaya,walevi, ganja,nk).
Wengi wao mazingira ya wakati huo yaliwaharibu! They did not believe in education, Kwa sababu wengi wazazi wao walikuwa hawajasoma lakini walifanikiwa kwenye biashara hasa za Kenya/Tanzania(Kitobo).

Mazingira ya wakati ule yaliwadanganya sana. Biashara za magendo za Kenya/Tanzania sasa hivi zimedhibitiwa wengi wao wanasota na kujiliwaza na Bangi!!
 
Jani mhindi wa chaulo, bagia na koni hatari Sana nilikuwa nasoma mawenzi ps mapumziko ya 4 asb fasta kwa Jani tunachanga mpaka ifike Mia na 50 kula bagia au chaulo
Muhindi Makaputura mzee wa juisi na keki mnamkumbuka? Opp. Mawenzi NBC br. Bado yupo vile vile hajabadilika .
 
Back
Top Bottom