Mataifa mengi ya Afrika hayajaweka Mikakati thabiti ya Usalama wa Mitandao jambo linalowafanya wawe kwenye hatari ya kushambuliwa

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Mpaka kufikia mwaka 2022 bado mataifa mengi ya Kiafrika yanaonekana kuwa nyuma katika ya kuweka mikakati thabiti itakayowezesha usalama wa mitandao katika nchi zao. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia wananchi wengi pamoja na serikali za Kiafrika zinatumia vifaa vya kidijitali katika kuhifadhi taarifa zao muhimu.

Wataalamu mbalimbali wa masuala ya teknolojia wanaeleza kuwa nchi nyingi za kiafrika zipo hatarini kushambuliwa na kuibiwa taarifa zao na wahalifu wa mitandao, mfano Wadukuzi wanadai fidia ili kufungua tovuti za Serikali Msumbiji. Zaidi ya hayo wataalamu hawa wanabainisha kuwa bado serikali nyingi za kiafrika hazijalivalia njuga suala la usalama wa mtandao na kuhakikisha ulinzi wa taarifa zake na za wananchi wake.

Abdul-Hakeem Ajijola na Nate D.F. Allen katika makala yao African Lessons in Cyber Strategy – Africa Center for Strategic Studies wanaeleza kuwa Inakadiriwa kuwa anwani za mtandao milioni 6.2 ziliibwa kutoka kwa Kituo cha Habari cha Mtandao cha Afrika, AFRINIC, shirika lisilo la faida la Kiafrika ambalo lina jukumu la kusimamia usajili wa mtandao wa barani Afrika (the African non-profit responsible for managing the continent’s internet registry). Anwani hizo zilizoibwa zinaelezwa kuwa na thamani ya dola milioni 150, ambazo ni sawa na asilimia 5 ya anwani zote za IP4 za Afrika. Wizi huo ulidaiwa kufanywa na Mtendaji Mkuu wa zamani wa AFRINIC ambaye inaelezwa alishirikiana na bilionea wa Hong Kong kutekeleza uhalifu huo.

Hata baada ya AFRINIC kurudisha anwani, inaelezwa kuwa kampuni ya Hong Kong iliweza kutishia uwezo wa AFRINIC kwa kushtaki na kushawishi mamlaka kufungia akaunti za benki za AFRINIC. Aidha wanaeleza kuwa, Ukosefu Mawakala na Watendaji wa kufanya kazi ya msingi ya kuhakikisha kuwa anwani za IP za Afrika zinamilikiwa na Waafrika ni tishio la moja kwa moja la usalama wa mitandao barani Afrika.

Nini kinatokea Afrika?
Abdul-Hakeem Ajijola
na Nate D.F. Allen katika makala ya African Lessons in Cyber Strategy wanaeleza kuwa Afrika inakabiliwa na mahambulizi mbalimbali mtandao ikiwapo Vitisho kutoka kwa Wahalifu mbalimbali, hujuma ya miundombinu, wizi wa mitandaoni na ukosefu wa wataalamu wa kudhibiti uhalifu huo.

Wanaelezwa kuwa bado, nchi nyingi za Kiafrika hazijabuni mkakati wa kitaifa wa usalama wa mtandao. Nchi nyingi zilizo na mikakati hushindwa kufikia malengo kutokana na kukosa vipengele vya msingi katika mikakati yao pamoja na kutowahusisha Wahikadau na Wataalamu. Mikakati ya kuboresha Usalama wa mitandao Afrika inatekelezwa na nchi chache kama inayoonekana kwenye ramani hi katika mataifa yaliyowekewa rangi ya bluu.

1647268381047.png

Chanzo cha data: United Nations Information Technology Union


Kulingana na takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa (ITU) hivi karibuni zinaonesha kuwa takriban theluthi moja ambayo ni nchi (17) kati ya nchi 54 za Afrika zimekamilisha mkakati wa kitaifa wa usalama wa mtandao, ambao ni chini ya nusu ya wastani wa kimataifa.

Inaelezwa kuwa Serikali ndio mhusika Mkuu linapokuja suala la kudhibiti vitisho vya mtandao. Bila mikakati ya kitaifa, serikali mara nyingi hujikuta zikishindwa kueleza upeo na ukubwa wa vitisho vinavyowakabili. Hii Ramani chini inayonesha mataifa machache yenye mkakati wa kitaifa wa usalama wa mitandaoni.

Je, kuna mikakati yoyote kuboresha Usalama wa mitandaoni katika nchi za Afrika?
1. Makala hii ya African Lessons in Cyber Strategy inaeleza kuwa Kuanzia mwaka wa 2019, Tume ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU), ilianzisha majadiliano na nchi za Afrika ya Magharibi kuhusu Usalama wa Mitandaoni na jinsi wanavyoweza kupambana dhidi ya Uhalifu wa Mtandao (OCWAR-C) na kupitisha Mkakati wa Kikanda wa Usalama wa Mtandao na Uhalifu wa Mtandao.

2. Mfumo wa Umoja wa Afrika wa Ushirikiano wa Polisi (AFRIPOL) uliunda Mkakati wa Uhalifu wa Mtandaoni 2020-2024 ambao unalenga kuimarisha uratibu, kukuza uwezo maalum wa polisi, na kuoanisha mifumo ya kisheria na udhibiti wa uhalifu wa mtandaoni.
Wakati huo huo, Umoja wa Afrika (AU) unafanya kazi ya kuunda na kutekeleza mkakati wake wa usalama wa mtandao wa bara kupitia Kundi lake la Wataalamu wa Usalama wa Mtandao lililoanzishwa hivi karibuni.

Kupitia uundaji wa Jumuiya ya Wataalamu wa Mtandao wa Afrika (ACE), AU inashirikiana na Jukwaa la Kimataifa la Utaalamu wa Mtandao (GFCE) kusaidia kujenga uwezo wa mtandao. Hata hivyo Mikakati ya kuboresha Usalama wa mitandao Afrika inatekelezwa na nchi chache na kwa vipengele vichache kama inavyooneshwa kwenye kielelezo hapa chini

1647268627933.png

Chanzo cha Data: Africa Center for Strategic Studies
Picha: Data zinaonesha baadhi ya nchi za Kiafrika zenye mikakati ya kuweka usalama wa mtandaoni pamoja na vipengele vilivyoachwa

Credit: Africa Center for Strategic Studies, Abdul-Hakeem Ajijola and Nate D.F. Allen
 
Nani ashambulia Africa ili apate nini, bara ambao haliwezi kulisha raia wao eti wawekeze kwenye usalama wa mitandao be serious dude
 
Back
Top Bottom