Story of Change Maswali yaliyogonga kichwa ushindi wa lazima

Jareka Uandishi

New Member
Apr 18, 2018
4
45
Je, ni kweli hakuna ajira kisa wasomi ni wengi? Kusema wahitimu hawana uwezo wa kuajiriwa au kujiajiri?

Je, vijana tunaelewa kuwa maendeleo ni mchakato na si kulala masikini ukaamka tajiri?

Je, tumegundua kuwa elimu ya sasa na ile ya miaka ile ni tofauti kitakwimu kabla ya kusema kwa nini hatuajiliwi? Mpaka mwisho wa andiko hili utapata majibu na mapendekezo.


Elimu ni ujuzi/maarifa alionao mtu unaomwezesha kukabiliana na maisha yake pamoja na changamoto. Maendeleo ni ile hali ya mtu, kundi au taasisi kubadilika kutoka hatua moja kwenda nyingine kiuchumi na kifikira. Kusoma andiko hili mpaka mwisho manufaa yake yatakuwa kuongeza wigo kifikra zitakazo amsha maono.

Ni kweli kuwa ajira hakuna kwa sababu wasomi ni wengi. Kila mwaka kuna wahitimu ngazi tofauti lakini hakuna taasisi zinazokua na kuwa na uwezo wa kuajiri wahitimu wa kila mwaka. Kwa maana hiyo wachache huajiriwa wengine huendelea kusubiri sandakalawe ya mwenye kupata apate… Swali langu ni kwa nini hili suala huendelea kukua. Kwamba taasisi husika ikiwemo ya udahili haioni hili suala?

Wahitimu wa vyuo vikuu wameandaliwa kuajiriwa na hii iko wazi (wasimamizi). Kwa sababu kama tangu mtu kuanza shule mfano akiwa na miaka 7+ miaka 16 ya masomo kwa mwanafuzi wa moja kwa moja. Ndani ya miaka hiyo elimu inayoamsha hali ya kujiajiri ni asilimia ndogo. Mitaala yetu asilimia kubwa ni nadharia ambayo mwanafunzi hana sehemu ya mwendelezo baada ya mwalimu kutoka darasani zaidi ya kujisomea daftari lenye nadharia.

Maana yake baada ya elimu ya mwalimu kufundisha kwa vitendo ndani ya maabara akitoka siku imeisha tusubiri kesho tena. Maabara inafungwa hivyo mwanafunzi hana sehemu ya kufanya mazoezi ya kile mwalimu alichoelekeza. Hii ni kwa shule nyingi, wengi tumepitia maisha haya. Baada ya kuhitimu vyuo vikuu tujiajiri ndio kauli inayoonekana kuwa nyepesi kutoka. Je katika mazingira hayo kuna namna rahisi zaidi ya mtu mwenyewe kujipambania upya? Tuendelee.

Je, hii ndiyo taswira ya maisha ya sasa ya utandawazi na maendeleo ya teknolojia? Ni kwa nini wizara isiliangalie. Suala la udahili kwenye kozi zilizo na watu ambao hawana ajira, zinadahili wapya kwenye uwiano sawa wa waliotoka na kuingia bila mabadiliko na mikakati ya kuondoa tatizo. Mfano kubadili mtaala na kudahili kulingana na uhitaji hasa kwa ngazi ya kuandaa wasimamizi kama nilivyoeleza mazingira ya elimu ya chuo kikuu. Wengine wakaenda kwenye kozi ambazo vitu wanavyojifunza vyuo vya kati hukutana navyo mtaani. Mfano mwanafunzi wa veta akisoma uchomeleaji ajira mtaani atazikuta za kuchomelea. Watu wanajenga na vitu vingine vingi.

Hivyo anaweza kudunduliza kimalengo akajiajiri au akaajiliwa. Mtu akienda SIDO akasoma usindikaji wa vyakula, vitafunwa, keki angalia mtaani watu wanajilamba midomo kisa vitafunwa, ukiachana na mikate. Hoja yangu ni kuwa dunia inabadilika na jamii yake, basi katika kweli hiyo, elimu hii inatusaidia lakini kuna baadhi ya maudhui tunayoendelea nayo teknolojia imeyamaliza uhai tunaweza kwenda na mabadiliko. Mbinu ya kutoka hapa siyo kulaumu wahitimu bali kuwaelimisha namna wanavyoweza kujiajiri huku mitaala ikiangaliwa katika mazingira ya sasa.

Kuna namna kubwa ya kuweza kuchunguza kila idara na uhitaji wake. Udahili ukawa hivyo kwa vigezo vya ufaulu watavyojiwekea kiutaratibu. Hii itasaidia kuwatoa wale walio mtaani katika hali ya uhitaji wa ajira. Utasema endapo wasomi wakiisha kwa sababu ya udahiliwa mpya? Haiwezekani kwani baada ya kumaliza wimbi hilo udahili unaongezeka kulingana na uhitaji tena. Hiyo ni pale tu kama msingi wa elimu utaendea kuwa mnufaika wa elimu kuajiriwa. Kama mitaala inaandaliwa katika mkutadha wa kumfanya mnufaika apate sitadi za kujiajiri basi hapa hapana ukomo. Elimu iendelee kuwa ukombozi.

Zaidi ya hapo kuna mambo mengi tunayaishi lakini mitaala yetu haijayasisitiza hasa uga wa vipaji, dunia sasa inanufaika na vipaji pia elimu ya ujasiriamali. Mfano mitindo, mziki, mapambo, vitu ambavyo wahitimu baada ya kukaa mtaani na kukosa ajira wameamua wenyewe kujiajiri kupitia idara hizo. Mfano wanasuka, wapambaji na ushonaji n.k ambavyo wamejazia maarifa baada ya kumaliza vyuo katika kutafuta harakati za kujikwamua.

Pongezi kwao maana wanaendelea kukubali kuwa jamii na maisha yanabadilika. Sasa kama hii inawezekana, jamii inanufaika kwa huduma zao kwa nini wasitoke walikosomea wakiwa wanajua tayari? Ili akiwa mtaani awaze kujiajiri kuliko tena kozi fupi (short course)?

Je, elimu yetu haitusaidii kuona kuwa elimu ya miaka 1980-20 imekuwa tofauti katika Nyanja nyingi, ikiwemo hii ya wiano na ajira?

Ni kweli kuwa ukweli unauma lakini bora anayekufichulia maradhi ili utafute tiba shukurani kwake ni pale utakapona. Kumbe kulalamika hakutamtoa mtu nyumbani aende kuajiriwa ukizingatia awamu ya sasa kutafuta kazi unapitia mitihani zaidi ya ile ya chuo. Baada ya kuwa limegundulika hivyo tunayo nafasi ya kuwaza tofauti. Pitia hatua za huyu mchumia juani alivyolia kivulini mbali na changamoto za wahitimu kuwa wengi.

Safari ya kutafuta mafanikio baada ya elimu ya chuo kikuu.

Ni vigumu kwa kauli yangu kusema kuwa elimu yetu imepitwa na wakati kiasi cha watu kukosa sifa, tukubali mazingira yamebadilika. Jambo linaloikabili elimu yetu ni kutobadilika kulingana na wakati..

Mhitimu mmoja alihitimu chuo akagundua kwa upepo uliokuwepo hakukuwa na mazingira ya kupata ajira hasa serikalini na pengine katika taasisi binafsi. Alianza kuangalia maisha yatakuwaje ili aweze kufika sehemu ambayo alikuwa akitamani. Alihangaika kutafuta kazi kwani alielewa anayo elimu tayari. Anywhere if possible with simple exceptional. Kwa maana hiyo, aliamini anaweza pata kazi nje ya idara.

Basi alipata kazi ya kufundisha kwenye shule ya mchepuo wa kiingereza (English Medium), Iliyopo jijini dar es salaam. Hakika alifanya kazi kwa mafanikio. Ndani ya masomo aliyopewa mtihani wa kwanza yote alipata wasitani wa 75+. Hakika aliona amefanya vizuri kwa vile ilikuwa ni mara ya kwanza kufundisha. Lakini aliitwa na mtaaluma nakuambiwa bado sana …. Hakukata taamaa wala kuingiwa na woga aliendelea awamu iliyofuata alipata wasitani wa A, A hata haikutosha maana alikuwa na utashi kuona masomo yake yanaongoza kati ya saba kipindi kile.

Hatima ilifika masomo yake yalianza kuongoza na hapo kazi ikawa ni kulinda heshima. Mbali na shughuli hizo za ufundishaji nje ya muda wa kazi alirejea kwenye taaluma yake kaangalia namna anavyoweza kunufaika kulingana na kile alichosoma akiwa chuoni. Kwa vile alikuwa amesoma shahada ya awali ya Kiswahili Isimu. Alichagua idara alizopenda ndani ya kozi yake. Ndipo alipoanza kuhariri vitabu na kutafsiri vitabu. Alifanya kazi nyingi hata kwa malipo ambayo alijua wazi siyo stahiki. Alifanya kazi kama sehemu ya kukuza uzoefu.

Miaka ilienda baadae akasikia kuna habari ya kufundisha Kiswahili nje ya nchi. Ikawa mwenda bure si mkaa bure huenda akaokota. Alisoma kozi ya utimilifu ili kuelekea fursa hiyo lakini hakufanikiwa. Usipopata leo huenda ukapata kesho. Aliona ni sehemu ya mapambano kuelekea nchi ya ahadi. Akiwa anaendelea na harakati za mapambano kuna kampuni kubwa ilitangaza nafasi za kazi na yeye alifanikiwa kupata taarifa na kuomba kazi hiyo.

Siku ilifika kupigiwa simu kuhudhuria usahili. Hakuacha hii fursa ipite, wahenga wanasema kuishi kwingi ni kuona mengi hivyo kwa miaka aliyokuwa mtaani alifanya usahili mara nyingi.. Kazi alizokuwa akifanya kwa malipo ya chini zilimbeba siku ya usahili kama uthibitisho wa aliyokuwa akieleza. Je, msakatonge mwenzangu unawaza katika mazingira haya kama mbadala wa changamoto au ndio upo upande wa maneno matupu yahavunji mfupa?

Je, wahitimu wa vyuo kwenye changamoto ya kazi mnawaza kitu kama hiki? Kumbuka taaluma ni ile ile na wahitimu wa vyuo ni wengi lakini waajiri wanapenda kumuajiri mtu ambaye mbele zake anaonekana ni tofauti na wengine. Mbali na kumahiri vitu ndani ya kozi uwe na nyongeza ya kukutofautisha na wengine.

Ili kwenye usahili uwe na kitu cha ziada na unaweza kujibu suali na una uzoefu gani. Kumbuka tatizo siyo kwamba hawana uzoefu bali hawajui huo uzoefu ni upi. Kupitia njia ya msakatonge juu hapo alijibu suala la uzoefu kwa kazi alizokuwa akifanya binafsi na kuajiriwa. Ukitaka kufanikiwa zaidi anza harakati za hizi mapema. Tafuta cheti ujuzi na baadhi ya namna ya kujitofautisha. Hili lipo pia katika mazingira ya biashara ya sasa watu hufunga biashara kwa sababu ya kushindwa kujitofautisha. Mfano kupitia mfano wa juu mtu ambaye alisoma na hakuwahi kufanya kazi hiyo angeshindanaje na yule ambaye ana kazi ambazo ameisha zifanya? Huku ni kushinda kwa lazima.

Rai yangu, kauli kuwa wanahitimu hawaajiriki kama sehemu ya kuficha kizazi kisicho na ajira siyo sawa. Ingekuwa kweli hivi vyuo wanavyohitimu vinasimamiwa na nani? Baada ya kugundulika hivyo ni hatua gani zimechukuliwa? Pia kujiajiri siyo haraka sana kwa wote wakati kipindi chote miaka 10+ wapo darasani japo wachache wanaweza kutokana na misingi yao ilivyojengwa kuanzia familia. Nilisikitishwa kuona mtu aliyeajiriwa miaka na miaka anahimiza kujiajiri ila yeye akitumbuliwa mbali na kuajiriwa muda ana anguka na kuzimia.

Ipo nafasi ya kuchagua watu kulingana na maombi yao japo lilikuwa linafanyika lakini litiliwe mkazo. Mtu anapoenda chuo kusoma kile alichokuwa akipenda akirudi mtaani au hata kabla ya kurudi anakuwa amegundua pengo la kufanyia kazi nayo ikawa ajira kwake. Hivyo ni faida kiasi gani SIDO ikiboresha huduma na ikasikika zaidi, mtu akienda akasomea usindikaji wa chakula akatatua matatizo ya lishe mtaani kwa kuzalisha chakula bora lakini ajira atatoa pia. Atatatua tatizo na kipato atapata kuna mengi huko pia. Je, vipi veta na faida zake wengi tunazijua tunaona vijana wakitoka wanavyochakalika kuliko yule atembeaye ana bahasha. Mkazo unaweza kuwekwa huku kila baada ya kidato cha nne ili tupate pembe tatu yenye uwiano wa kujengana.

Usiogope watu wanakuonaje wakati hata wao wanajiuliza unawaonaje.
 
Upvote 1

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom