Mm sio Mzee. Ila kuna namna naisifu Elimu ya Mkoloni.
Kulikuwa na watu wa fani mbalimbali (ufundi stadi) na watu wa taaluma white collar Job.
Sasa hapa katikat kama taifa hawakuipa kipaumbele Taaluma ya fani mbalimbali na wakaona fani sio mwelekeo sahihi. Wakaelekeza kwenywe wasomi na kutengeneza watu weng wa white collar job ambao pia kazi hazipo za kuwasitiri wote.
Kuna mtu anamaliza SUA.
Ila anasubiria aajiriwe.
Wakat mfano kama amesomea Livestock alitakiwa
Awezeshwe afuge na aelimishe jamii inayomzunguka maana anajua mifugo kwa undan . Na ataleta tija kwa jamii na taifa.
Ila sasa mtu kama huyo anataka aajiriwe. Inafikirisha.
Ila ni kwasababu ametaarishwa hivyo.