MrFroasty
JF-Expert Member
- Jun 23, 2009
- 1,195
- 592
Ni vyema wawaambie Wazanzibari wameshindwa nini kuiletea Zanzibar maendeleo tokea 1977 wakati Chama chao kilipoanzishwa hadi leo? Cha muhimu zaidi, wawajibu Wazanzibari angalau Masuala 7 yafuatayo kati ya masuala zaidi ya 700 ambayo Wazanzibari wanayo:
- Kwa nini walitumia Jeshi mwaka 2015 kupindua matokeo ya Uchaguzi wa Zanzibar? Na kimewashinda nini kuleta maendeleo ya Zanzibar baada ya Mapinduzi hayo wakati Serikali zote mbili wanazitawala wao?
- Kwa nini waliamua kuwasafirisha Masheikh wa Uamsho na kuwafungulia mashtaka Tanzania Bara kwa tuhuma za makosa yaliyofanyika Zanzibar? Kwa nini walifanya hivyo, wakati walijua na walikiri katika vikao kuwa jambo hili ni kinyume na Katiba na Sheria za Zanzibar na hata zile za Tanzania Bara? Na ni kinyume pia na maamuzi na maelekezo ya wazi ya Mahkama Kuu ya Zanzibar na Mahkama ya Rufaa ya Tanzania yaliyotolewa katika maamuzi kadhaa. Utaileteaje Zanzibar maendeleo wakati unaidharau na hutambui hata mamlaka yake ya kikatiba?
- Kwa nini walitunga Katiba Inayopendekezwa mwaka 2014, ambayo kwa wazi na dhahiri ilikusudia kuiangamiza Zanzibar, kinyume kabisa na mapendekezo ya Rasimu ya Tume ya Warioba? Na kwa nini walikataa katakata kuingiza mapendekezo ya Zanzibar yaliyokusudia kuinusuru Zanzibar hata katika mfumo wa Serikali Mbili uliopendekezwa na rasimu yao? Miongoni mwa mapendekezo yaliyokataliwa na akina Polepole, na ambayo yalipendekezwa na Kamati ya Mawaziri wa CCM Zanzibar iliyoongozwa na Balozi Seif Ali Idi, ni pamoja na kuondoa kipengele cha kumpa Rais wa Muungano uwezo wa kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na sehemu na pia lile la kuifanya ardhi kuwa jambo la Muungano.
- Kwa nini akina Polepole wameshindwa kuiwezesha Zanzibar kupata mkopo wa dola 200 milioni za Kimarekani kwa ajili ya mradi wa bandari ambazo Dkt. Ali Shein alienda kuziomba mwenyewe kwa Rais wa China na kukubaliwa? Mradi wa bandari ulikuwa miongoni mwa vipaumbele vya Ilani yao. Kilichokwamisha kupatikana fedha za mradi huu ni barua tu kutoka kwao akina Polepole. Benki ya Exim ya China ilishakubali kutoa fedha hizo. Zanzibar walipokoseshwa fedha hizo, Wachina hao ndio waliosikitika na sio akina Polepole.
Walichokifanya akina Polepole ni kuiambia Zanzibar ifanye upembuzi yakinifu mwengine [feasibility study] kwa vile gharama za ujenzi ni kubwa sana. Kufikia hatua ya Zanzibar kupewa barua hiyo ya kuagizwa kufanya upembuzi yakinifu ilichukuwa zaidi ya miaka mitatu. Suala la nyongeza hapa ni kuwa utafanyaje upembuzi yakinifu, wakati Zanzibar ilishaingia mkataba na Kampuni ya CHEC na kilichobaki ni kutimiza masharti ya awali [conditions precedent]?. Moja ya masharti hayo ni kuandaa maelezo yakinifu ya masharti na gharama za mradi [employer’s requirement], ambayo ndio njia sahihi ya kupunguza gharama.
- Kwa nini akina Polepole wamekataa katakata kuyatoa mafuta katika mambo ya Muungano ili kuiwezesha Zanzibar kuendeleza rasilimali hiyo kwa viwango na taratibu zinazokubalika kimataifa na kibiashara? Kwa nini, badala yake, wamefanya lile walilozowea la ghilba, kwa eti kuipa Zanzibar ruhusa ya kusimamia sekta ya mafuta na gesi asilia, huku wakitunga sheria ya Bunge kusema kuwa utajiri wote wa mafuta ni mali ya Serikali ya Muungano?
Wazanzibari wanaifahamu vyema Serikali ya Muungano hata ikivaa nikabu na juba. Wanaifahamu hata ikihema tu, sikwambii ikitembea au ikiongea. Wanaifahamu kwamba ni Serikali ya Tanganyika. Ndio maana hawajawahi kumsikia Rais wa Serikali hiyo akiitaja Zanzibar na nini wameifanyia katika hotuba yoyote ya kufunga Bunge tokea ya Rais Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na ya hivi juzi ya Rais Magufuli. Kama huamini zitafute. Wazanzibari wamezisoma zote na hawajawahi kuona kitu cha namna hiyo.
- Kwa nini akina Polepole wameuwa biashara na kudamirisha uchumi wa Zanzibar kwa kuiwekea vikwazo vya kikodi, vya kibiashara, mfumo wa fedha na kuinyima haki zake ndani ya Muungano? Wakitaka ushahidi wa jambo hili, nawaomba wakodi hata Uwanja wa Amani, Wazanzibari wawaletee mashahidi wa jinsi ya dhulma ya kiuchumi wanavyoifanya.
Wazanzibari wanahitaji majibu ya masuali haya kabla akina Polepole hawajaja kuwauzia ghilba nyengine. Kimebadilika nini mwaka huu ambacho hakikuwepo miaka iliyopita? Mgombea? Sifa, uwezo au aila yake?
Sababu ya kumpa pole Polepole ni kuwa amesahau ile busara ya wazee: “Sikiliza kwa makini yale yasiyosemwa!”
TANBIHI: Mwandishi wa makala hii, Bwana Othman Masoud Othman, ni mwanasheria mkuu wa zamani wa Zanzibar, ambaye kwa sasa anaendelea kufanya shughuli zake binafsi kwenye taaluma yake ya sheria.