Maswali ya Wazanzibari kwa CCM

Maswali ya Wazanzibari kwa CCM

Hizo ni porojo za kampeni.. Mbona Maalim alikuwa makamu wa Rais na hakufanikiwa kuwatoa?
Mwinyi ndio waziri wa ulinzi, kwanini asiwatoe ? Hajathubutu hata kuwazungumzia hao masheikh, maneno ya huku kaufyata kwenye suala la kuwatetea waislamu wenzake. Hata kampeni zake ni ivyo ivyo tuu, nitacopy-paste yale yote ya Magufuli! Amesahau Magufuli hana hata kitu kimoja alichofanya kule visiwani.
 
Mkuu MrFroasty, kwanza it's wrong kumtaja Polepole kwenye issues za kiserikali, hizi issues ulizoibua hapa sio issues za kichama, CCM, ni issues za kiserikali, URT.

Mimi nitajibia mambo mawili, la mkopo wa dola milioni 200 za Exim bank ya China kupanua bandari ya Zanzibar na issue ya mafuta.

1. Mkopo.
Mikopo ya kimataifa ni issue ya muungano, kimataifa Zanzibar sio nchi, Zanzibar ni sehemu ya JMT, nchi ni Tanzania, hivyo Zanzibar haiwezi kukopa as Zanzibar, bali ina uhuru wa kutafuta mikopo na misaada ya kimaendeleo.

Lakini anaye idhinisha hiyo mikopo ni JMT, hivyo Zanzibar ilipotafuta mkopo huo wa $ 200 milioni, na kukubaliwa na Exim Bank ya China, nani aliyefanya feasibility study to establish that cost?.

Ili kukopeshwa mkopo wa kimataifa wa kiserikali ni lazima serikali ya muungano ndio itoe government guarantee. Serikali yetu inaweza kutoa government guarantee kwa kitu ambacho hawakijui!.

Kwa faida ya wasiojua kuhusu government guarantee, serikali inapotoa government guarantee, inamaanisha Zanzibar, ikishindwa kulipa, Tanzania ndio tunalipa, hatuwezi kuji commit kulipa kitu tusichokijua, hivyo serikali yetu iliamua kwa nia njema kabisa process ianze upya, starting with a new feasibility study tuje na realist costs, tuwasainie hiyo government guarantee mpatiwe huo mkopo mpanue hiyo bandari.

Na kwa wasio fahamu hii issue wasitake kuifanya kisiasa ikaonekana ni kero ya muungano, serikali yetu yenyewe imeishawahi kugomea mkopo wa Exim Bank upanuzi bandari ya Dar es Salaam na pia kugomea ujenzi wa bandari ya Bagamoyo kutokana na mazonge mazonge.

WaChina they are very good kwenye lobbying, baadhi ya miradi hawafuatia international good practice procedures.
Kinachofanyika kwenye baadhi ya miradi ni hiki
  1. Wao ndio wanatoa suggestions ya kufanya mradi fulani, ukikubali
  2. Wao ndio wanafanya feasibility study and establish the cost
  3. Wao ndio wanatafuta funding kuufund mradi huo na ni lazima ujengwe na Chinese companies
  4. Hapo ndipo Exim Bank ya China huingia na masharti yao ya ajabu ajabu wanakuwa tayari kutoa fedha zote za mradi ikiwemo a 20 year grace period!. Bomba la Gesi Mtwara:A "20 -Year Grace Period" ya Mkopo wa Exim Bank-China ni "Changa la Macho?!".
  5. Ili fedha zitoke, wanahitaji government guarantee ili mkishindwa kulipa, serikali ndio iwepa bure huo mradi
  6. Wao ndio wajenzi kwa mtindo wa Built and operates hadi mkopo utakapolipwa.
  7. Mkishindwa kulipa, wanataifisha mradi unakuwa mali yao.
  8. Gharama usually ni highly inflated ili kutoa kickbacks za maana kwa waliofanikisha.
  9. Mambo kama haya tuliyakataa hapa Omari Nundu: Sioni sababu ya kujiuzulu
  10. Pia tuliyakataa katika bandari ya Bagamoyo
Mafuta,
Japo Mafuta ni issue ya muungano, sheria ya mafuta ni sheria ya muungano, ila sheria imetoa mamlaka kwa Zanzibar kutunga sheria yake ya mafuta bila hitaji la kubadili katiba na kuyatoa mafuta kwenye mambo ya muungano.

P
Unaposema Zanzibar si nchi huku mkituaminisha ina rais wake na mamlaka yake inabidi kwanza muuondoe huo mkanganyiko ili tusiwaulize maswali magumu zaidi...
Kwa maana MUUNGANO WALINDWA KWA MARUNGU NA MAPANGA NA OLE WAKE AUCHOKONOAE!!!
HII HUTOA PICHA RAHISI KWAMBA "NI MUUNGANO WA MASHAKA"
Laa si hivyo ungejadiliwa sebuleni na lile la serikali tatu pendekezwa lisingewatia watu mashaka.
Kuna dhulma inaendelea pande zote mbili
 
Mwinyi ndio waziri wa ulinzi, kwanini asiwatoe ? Hajathubutu hata kuwazungumzia hao masheikh, maneno ya huku kaufyata kwenye suala la kuwatetea waislamu wenzake. Hata kampeni zake ni ivyo ivyo tuu, nitacopy-paste yale yote ya Magufuli! Amesahau Magufuli hana hata kitu kimoja alichofanya kule visiwani.
Tutamfikishia hilo.. I hope atalifanyia kazi.. Pia waziri wa ulinzi hausiki.. Mhusika ni waziri wa mambo ya ndani na waziri wa katiba na sheria.
 
Mkuu Macos , kwanza hakuna nchi inayoitwa Tanganyika, wala Zanzibar, nchi inaitwa Tanganyika na nchi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, zote mbili zilikufa siku ile ya muungano kwa kuungana kuwa kitu kimoja, tukaunda nchi moja ya JMT, hivyo sasa Tanzania ni nchi moja tuu ya JMT, Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT.

Kwenye hili la upanuzi wa bandari ya Zanzibar, kama nilivyo jibu kwenye jibu langu la msingi, kinachelewesha ni taratibu tuu, tena kwa taarifa yako, sio tuu kupanua bandari ya Zanzibar bali in future, kuifanya Zanzibar kuwa a free port kama Japan, Singapore na Dubai, makampuni makubwa ya kuuza magari kama Be Forward waweke yard zao Zanzibar, the rest of Africa badala ya kuagiza magari kutoka Japan na Dubai, waagize kutoka Zanzibar !.

Kwavile Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, Tanzania ndio baba na Zanzibar ni mtoto, baba ni baba na mtoto ni mtoto, kama ilivyo kwa masikio hayawezi kuzidi kichwa!.

Hili la kuitana ukoloni mara utumwa ni maneno maneno tuu ya vitimbakwiri, Zanzibar inapokea asilimia 4.5% ya misaada yote ya Tanzania inayopokea kutoka nje.

Hivyo kwenye kuleta maendeleo sometimes JMT lazima iidhibiti Zanzibar, ili kuleta even development, mfano kwenye issue ya sukari, Zanzibar ina kiwanda cha sukari ambacho kinazalisha sukari ya kutosha ku suppliers soko la Zanzibar. Huko Zanzibar kilo ya sukari ni TZS 1,500 tuu. SMZ inaruhusu Wafanyabiashara wa Zanzibar import sukuri kutoka nje, matokeo yake sukari inayozalishwa kiwanda cha Zanzibar inadodea kiwandani!.

Wenye kiwanda cha sukari Zanzibar wanataka kuleta sukari hiyo huku bara kwasababu huku bei ni kuanzia TZS 2,500. Serikali ya JMT imewagomea!. Maadam Zanzibar inajitosheleza kwa sukari, tumieni sukari yenu mnayozalisha, na sio mzalishe sukari msiitumie, mtake kutuletea huku bara, huku mkitumia cheap imported sugar, hatuwakubalii!. Lengo la hatua hii muhimu ni kuwalazimisha Zanzibar mjitegemee. Hii ndio kazi ya Baba responsible!.

On top of mgao wa asilimia 4.5% ya pato la taifa, bado Zanzibar tunakupeni umeme bure!, hamlipi!. Tanesco ilitaka kuwazimia umeme, msivyo na shukrani mkasema zimeni tuu, nyie mtawasha vibatari!. Tunawapeni elimu ya juu bure, ajira, mnamiliki ardhi huku, mnafanya biashara huku, maduka makubwa karibu yote huku bara ni ya Wapemba!. Badala ya kutushukuru, ama kweli shukrani ya punda mateke!.

Siku zote tumekuambieni acheni kelele!, maadam mnayo sheria ya kura ya maoni, amueni moja...
Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja!.

P.
KWA ATAKAYE IBA KURA BORA APATE UGONJWA WA UKICHAA MILELE MAANA WATU HAWA WANATUZUNGUSHA VICHWA SANA TUTAOMBA MASAADA SOUTH KOREA (WOTE HATUWEZI KUWA WATOTO)
 
Mkuu mdudu , acha tabia za vidudu humu, unauliza kitu kuhusu serikali humu jf, kwani humu ndio serikalini?. Kuna Msemaji wa serikali humu kukujibia?. Ukiuliza lolote humu jukwaani kuhusu jambo lolote, yoyote mwenye jibu, atakujibu!. Kama ni maswali kwa serikali tuu, mpe Mbunge wako akakuulizie Bungeni usubirie majibu ya serikali, ukileta humu, utajibiwa na sisi Watanzania wazalendo wa taifa hili, tupo!.
P
KWA ATAKAYE IBA KURA BORA APATE UGONJWA WA UKICHAA MILELE MAANA WATU HAWA WANATUZUNGUSHA VICHWA SANA TUTAOMBA MASAADA SOUTH KOREA (WOTE HATUWEZI KUWA WATOTO) = MAANA WENGINE SIJUI WANAPAMBANA ILI IWEJE!?

NIKAMA MAWAZO AFADHALI KUELEKEA CHAMA KIMOJA CHA SIASA
 
Swali la nyongeza

Pamoja na Baraza la wawakilishi kuwa na wabunge )wawakilishi wa CCM peke yao kwa miaka mitano,
Je Zanzibar imebadilika na kuwa kama ulaya?
Je kelo,shida na matatizo ya wazanzibar zimeisha?
Shida na matatizo ya binadamu huwa haviishi. Orodhesha nchi zozote unazoziona "zimeendelea" Halafu google au search Youtube kampeni za wagombea wao ndo utagundua kwamba wana shida na matatizo gani japokuwa wewe unaona "wameendelea"
 
- Kwa nini akina Polepole wameshindwa kuiwezesha Zanzibar kupata mkopo wa dola 200 milioni za Kimarekani kwa ajili ya mradi wa bandari ambazo Dkt. Ali Shein alienda kuziomba mwenyewe kwa Rais wa China na kukubaliwa? Mradi wa bandari ulikuwa miongoni mwa vipaumbele vya Ilani yao. Kilichokwamisha kupatikana fedha za mradi huu ni barua tu kutoka kwao akina Polepole. Benki ya Exim ya China ilishakubali kutoa fedha hizo. Zanzibar walipokoseshwa fedha hizo, Wachina hao ndio waliosikitika na sio akina Polepole.
Kwenye mkopo jibu liko hapo nilipoweka mkazo (bold). Iweje anayetaka kukukopesha asikitike badala ya mkopaji au mdhamini?
 
Kwenye mkopo jibu liko hapo nilipoweka mkazo (bold). Iweje anayetaka kukukopesha asikitike badala ya mkopaji au mdhamini?
Japo China ni rafiki zetu, na Benki yao ya Exim, imetukopesha sana katika miradi mingi mikubwa, kwenye hizi dola milioni 200 za upanuzi wa gati ya Zanzibar, mwenye kujua zaidi kinachoendelea humo ni mdhamini na sio mkopaji!. Kilichofanyika ni ku inflate mkopo ili kubakisha kickbacks za maana, hili lilifanyika katika mkataba wa kupanua bandari ya Dar es Salaam, tugawagomea, na limefanyika katika mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo nayo tumeifuta!. Ndugu zetu Wazanzibari msiwe na shaka, maadam anayefuata ni Dr. Hussein Mwinyi na mradi huu hatujaufuta, tuchagilieni Hussein Mwinyi, mambo mazuri Zanzibar yaendelee.

Kwa bahati mbaya wazanzibari inabidi tujichagulie kiongozi tunaemuamini kama ana uwezo wa kuleta suluhisho la matatizo yanayotukabili. Au ulisikia tuna akili za kuchangiwa ? Maana wakoloni wengi wanakuwa na mtazamo kama huu!
 
Tanganyika ikikopa nani ndio guarantee wake?
Kwanza hakuna nchi inayoitwa Tanganyika.
Tanzania ndiyo inayokopa.
Nchi yoyote ambayo ni Sovereign inaruhusiwa kukopa mikopo ya kimataifa.

Zanzibar sio nchi, hivyo haiwezi kukopa yenyewe as Zanzibar kwasababu sio nchi. Ili Zanzibar ikope, mkopo huo lazima uidhinishwe na Tanzania na kudhaminiwa na government guarantee ya JMT.
P
 
Itoshe kusema Tanganyika wanaamini Zanzibar siyo nchi.
Mkuu Bila bila , issue ya Zanzibar kama ni nchi au sio nchi, sio suala la imani, ni suala la establishment na statues.

Japo marekebisho ya katiba ya Zanzibar ya 2010, yanaitambulisha Zanzibar kama nchi na kuitaja mipaka yake na kuuita ni moja ya nchi mbili zilizounda JMT,

Katiba ya JMT, haiyatambui mabadiliko hayo, hivyo kwa mujibu wa katiba ya JMT, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, au Tanzania Zanzibar, hivyo Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT.
P
 
Mkuu mdudu , acha tabia za vidudu humu, unauliza kitu kuhusu serikali humu jf, kwani humu ndio serikalini?. Kuna Msemaji wa serikali humu kukujibia?. Ukiuliza lolote humu jukwaani kuhusu jambo lolote, yoyote mwenye jibu, atakujibu!. Kama ni maswali kwa serikali tuu, mpe Mbunge wako akakuulizie Bungeni usubirie majibu ya serikali, ukileta humu, utajibiwa na sisi Watanzania wazalendo wa taifa hili, tupo!.
P
wee maylla kama hakuna Tanganyika hizo sherehe za uhuru munazosherehekea ni uhuru wa nchi gani
 
Exim Bank ya China noma sasa wanamuenyesha Kenya kwa kushindwa kuanza kulipia SGR (The rail to no where)Wakitaka wapewe bandari ya Mombasa.
China imeanza kutumia udhaifu wa Africa kutengeneza koloni jipya.
 
Pascal Mayalla una chuki na sisi Wazanzibari muda mrefu tu na hili halitaki kurunzi. Tanzania ikikopa nani hutoa go ahead. ? Ukitumia neno Tanzania na sisi Wazanzibari tunakuwa kwenye hilo kapu. Wakati huo huo hayo mambo hufanyika nyuma ya pazia ila sisi tukitaka kukopa wewe na jamaa zako wa Chato lazima mtoe Guarantee.
 
Ni vyema wawaambie Wazanzibari wameshindwa nini kuiletea Zanzibar maendeleo tokea 1977 wakati Chama chao kilipoanzishwa hadi leo? Cha muhimu zaidi, wawajibu Wazanzibari angalau Masuala 7 yafuatayo kati ya masuala zaidi ya 700 ambayo Wazanzibari wanayo:

- Kwa nini walitumia Jeshi mwaka 2015 kupindua matokeo ya Uchaguzi wa Zanzibar? Na kimewashinda nini kuleta maendeleo ya Zanzibar baada ya Mapinduzi hayo wakati Serikali zote mbili wanazitawala wao?

- Kwa nini waliamua kuwasafirisha Masheikh wa Uamsho na kuwafungulia mashtaka Tanzania Bara kwa tuhuma za makosa yaliyofanyika Zanzibar? Kwa nini walifanya hivyo, wakati walijua na walikiri katika vikao kuwa jambo hili ni kinyume na Katiba na Sheria za Zanzibar na hata zile za Tanzania Bara? Na ni kinyume pia na maamuzi na maelekezo ya wazi ya Mahkama Kuu ya Zanzibar na Mahkama ya Rufaa ya Tanzania yaliyotolewa katika maamuzi kadhaa. Utaileteaje Zanzibar maendeleo wakati unaidharau na hutambui hata mamlaka yake ya kikatiba?

- Kwa nini walitunga Katiba Inayopendekezwa mwaka 2014, ambayo kwa wazi na dhahiri ilikusudia kuiangamiza Zanzibar, kinyume kabisa na mapendekezo ya Rasimu ya Tume ya Warioba? Na kwa nini walikataa katakata kuingiza mapendekezo ya Zanzibar yaliyokusudia kuinusuru Zanzibar hata katika mfumo wa Serikali Mbili uliopendekezwa na rasimu yao? Miongoni mwa mapendekezo yaliyokataliwa na akina Polepole, na ambayo yalipendekezwa na Kamati ya Mawaziri wa CCM Zanzibar iliyoongozwa na Balozi Seif Ali Idi, ni pamoja na kuondoa kipengele cha kumpa Rais wa Muungano uwezo wa kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na sehemu na pia lile la kuifanya ardhi kuwa jambo la Muungano.

- Kwa nini akina Polepole wameshindwa kuiwezesha Zanzibar kupata mkopo wa dola 200 milioni za Kimarekani kwa ajili ya mradi wa bandari ambazo Dkt. Ali Shein alienda kuziomba mwenyewe kwa Rais wa China na kukubaliwa? Mradi wa bandari ulikuwa miongoni mwa vipaumbele vya Ilani yao. Kilichokwamisha kupatikana fedha za mradi huu ni barua tu kutoka kwao akina Polepole. Benki ya Exim ya China ilishakubali kutoa fedha hizo. Zanzibar walipokoseshwa fedha hizo, Wachina hao ndio waliosikitika na sio akina Polepole.

Walichokifanya akina Polepole ni kuiambia Zanzibar ifanye upembuzi yakinifu mwengine [feasibility study] kwa vile gharama za ujenzi ni kubwa sana. Kufikia hatua ya Zanzibar kupewa barua hiyo ya kuagizwa kufanya upembuzi yakinifu ilichukuwa zaidi ya miaka mitatu. Suala la nyongeza hapa ni kuwa utafanyaje upembuzi yakinifu, wakati Zanzibar ilishaingia mkataba na Kampuni ya CHEC na kilichobaki ni kutimiza masharti ya awali [conditions precedent]?. Moja ya masharti hayo ni kuandaa maelezo yakinifu ya masharti na gharama za mradi [employer’s requirement], ambayo ndio njia sahihi ya kupunguza gharama.

- Kwa nini akina Polepole wamekataa katakata kuyatoa mafuta katika mambo ya Muungano ili kuiwezesha Zanzibar kuendeleza rasilimali hiyo kwa viwango na taratibu zinazokubalika kimataifa na kibiashara? Kwa nini, badala yake, wamefanya lile walilozowea la ghilba, kwa eti kuipa Zanzibar ruhusa ya kusimamia sekta ya mafuta na gesi asilia, huku wakitunga sheria ya Bunge kusema kuwa utajiri wote wa mafuta ni mali ya Serikali ya Muungano?

Wazanzibari wanaifahamu vyema Serikali ya Muungano hata ikivaa nikabu na juba. Wanaifahamu hata ikihema tu, sikwambii ikitembea au ikiongea. Wanaifahamu kwamba ni Serikali ya Tanganyika. Ndio maana hawajawahi kumsikia Rais wa Serikali hiyo akiitaja Zanzibar na nini wameifanyia katika hotuba yoyote ya kufunga Bunge tokea ya Rais Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na ya hivi juzi ya Rais Magufuli. Kama huamini zitafute. Wazanzibari wamezisoma zote na hawajawahi kuona kitu cha namna hiyo.

- Kwa nini akina Polepole wameuwa biashara na kudamirisha uchumi wa Zanzibar kwa kuiwekea vikwazo vya kikodi, vya kibiashara, mfumo wa fedha na kuinyima haki zake ndani ya Muungano? Wakitaka ushahidi wa jambo hili, nawaomba wakodi hata Uwanja wa Amani, Wazanzibari wawaletee mashahidi wa jinsi ya dhulma ya kiuchumi wanavyoifanya.

Wazanzibari wanahitaji majibu ya masuali haya kabla akina Polepole hawajaja kuwauzia ghilba nyengine. Kimebadilika nini mwaka huu ambacho hakikuwepo miaka iliyopita? Mgombea? Sifa, uwezo au aila yake?

Sababu ya kumpa pole Polepole ni kuwa amesahau ile busara ya wazee: “Sikiliza kwa makini yale yasiyosemwa!”

TANBIHI: Mwandishi wa makala hii, Bwana Othman Masoud Othman, ni mwanasheria mkuu wa zamani wa Zanzibar, ambaye kwa sasa anaendelea kufanya shughuli zake binafsi kwenye taaluma yake ya sheria.
Sasa hiyo Masoud aka Mwanasheria Mkuu We Zamani unatoa arguments za kuua biashara ya wazanzibar kwenda Bara bila kutoa ufafanuzi wa sheria za kodi ambazo ni leading factor katika kujenga biashara iliyo na usawa? Au ujuzi wako wa sheria hauzungumzi suala linaloitwa Equity??
Naomba kasome income tax act ili uilewe na kwenye tax rate uiangalie za Znz zipoje na za Bara zipoje , ndio urudi utueleze nafuu ipo wapi na nini kifanyike ili kuweka haki sawa kwa wote.
Halafu hiyo Bandari ikiwa kubwa hizo bidhaa zitakuwa for local consumption or export or in transit .
Naomba na hilo la Bandari utueleweshe, target yake ni soko lipi na litatekelezwa vipi bila kuungilia mifumo ya kodi
 
Sijui unesema haya kwa akili yako au umehadithiwa hebu jaribu kufuatilia zanzibar kila mwisho wa mwezi inalipa tsh ngapi kwa tanesco halifu wanawauzia umeme ghali sana ulizia tu bara unity shilingi ngapi na zenji ngapi,kuhusu suala la sukari ni dhana ile ile iliyoachwa na hayati kama ni nchi moja vipi sukari ishindwe kuingia bara hii ni biashara huru huwezi kuzui kuingiza sukari zanzibar kisa kiwanda wakati bara kuna uhitaji mkubwa wa sukari
Fuatilia sheria za kodi zinasemaje? Na rate zipoje btn this bara na visiwani
 
Mkuu Macos , kwanza hakuna nchi inayoitwa Tanganyika, wala Zanzibar, nchi inaitwa Tanganyika na nchi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, zote mbili zilikufa siku ile ya muungano kwa kuungana kuwa kitu kimoja, tukaunda nchi moja ya JMT, hivyo sasa Tanzania ni nchi moja tuu ya JMT, Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT.

Kwenye hili la upanuzi wa bandari ya Zanzibar, kama nilivyo jibu kwenye jibu langu la msingi, kinachelewesha ni taratibu tuu, tena kwa taarifa yako, sio tuu kupanua bandari ya Zanzibar bali in future, kuifanya Zanzibar kuwa a free port kama Japan, Singapore na Dubai, makampuni makubwa ya kuuza magari kama Be Forward waweke yard zao Zanzibar, the rest of Africa badala ya kuagiza magari kutoka Japan na Dubai, waagize kutoka Zanzibar !.

Kwavile Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, Tanzania ndio baba na Zanzibar ni mtoto, baba ni baba na mtoto ni mtoto, kama ilivyo kwa masikio hayawezi kuzidi kichwa!.

Hili la kuitana ukoloni mara utumwa ni maneno maneno tuu ya vitimbakwiri, Zanzibar inapokea asilimia 4.5% ya misaada yote ya Tanzania inayopokea kutoka nje.

Hivyo kwenye kuleta maendeleo sometimes JMT lazima iidhibiti Zanzibar, ili kuleta even development, mfano kwenye issue ya sukari, Zanzibar ina kiwanda cha sukari ambacho kinazalisha sukari ya kutosha ku suppliers soko la Zanzibar. Huko Zanzibar kilo ya sukari ni TZS 1,500 tuu. SMZ inaruhusu Wafanyabiashara wa Zanzibar import sukuri kutoka nje, matokeo yake sukari inayozalishwa kiwanda cha Zanzibar inadodea kiwandani!.

Wenye kiwanda cha sukari Zanzibar wanataka kuleta sukari hiyo huku bara kwasababu huku bei ni kuanzia TZS 2,500. Serikali ya JMT imewagomea!. Maadam Zanzibar inajitosheleza kwa sukari, tumieni sukari yenu mnayozalisha, na sio mzalishe sukari msiitumie, mtake kutuletea huku bara, huku mkitumia cheap imported sugar, hatuwakubalii!. Lengo la hatua hii muhimu ni kuwalazimisha Zanzibar mjitegemee. Hii ndio kazi ya Baba responsible!.

On top of mgao wa asilimia 4.5% ya pato la taifa, bado Zanzibar tunakupeni umeme bure!, hamlipi!. Tanesco ilitaka kuwazimia umeme, msivyo na shukrani mkasema zimeni tuu, nyie mtawasha vibatari!. Tunawapeni elimu ya juu bure, ajira, mnamiliki ardhi huku, mnafanya biashara huku, maduka makubwa karibu yote huku bara ni ya Wapemba!. Badala ya kutushukuru, ama kweli shukrani ya punda mateke!.

Siku zote tumekuambieni acheni kelele!, maadam mnayo sheria ya kura ya maoni, amueni moja...
Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja!.

P.
Hapo mwisho umetumia lugha ya kibaguzi wakati ulipoanza ulisema sisi ni nchi moja.
 
Back
Top Bottom