Maswali ya mwisho juu ya Escrow

Maswali ya mwisho juu ya Escrow

Kama Waziri si mtumishi wa umma,nani anamlipa mshahara na marupurupu mengine na anafanya kazi ya nani na kwa nn?Je Katibu mkuu anapatikana vipi?
Jiulize swali dogo tu likusaidie; Tibaijuka kafukuzwa au kaachishwa kazi? Mbona bado ni MBUNGE na mshahara anao?
 
Hujanijibu mkuu.Mgogoro kati ya wanahisa wa IPTL-watu binafisi serikali imeingiaje hapa?

serikali kupitia shirika la Tanesco walikuwa walipa bili za umeme kwenye Akaunti ya IPTL mabadiliko ya Account ya kulipa bili za Tanesco ilikuwa ni kitu cha kuihusu pia sababu mkataba ulielekeza kuwa pesa zilipwe akaunti ya IPTL.Sasa kuhamisha na kuwaambia wapeleke akaunti ingine ambayo si ya IPTL ni Escrow ACCOUNT serikali ilibidi iridhie kama mmiliki wa Tanesco baada ya kukubaliana na sababu za kuhama huko.ISIJE BAADAYE KUTOKEA IPTL AKASEMA KWENYE AKAUNTI YANGU YA IPTL sioni malipo mmepeleka akaunti ambayo siijui.

Ni kama umepanga nyumba mwenye nyumba akasema pesa za kodi ziwe zinaingia akaunti inayomilikiwa na yeye na mkewe sasa baadaye akisema uingize kwenye akaunti mpya ya ESCROW lazima usiitike kienyeji itabidi uombe mkae msaini mabadiliko upya kwenye mkataba ndio maana serikali,BOT,tanesco na IPTL ilibidi wakae wote kulijadili hilo na kuwa pesa hizo zikae sehemu salama ya kuaminika kwa pande zote ambayo ni benki kuu pekee.
 
Kweli kuna watu bado wanamtetea rais Kikwete kwa mabaya yote haya? kweli hao watu ndugu zao hawana shida kabisa hapa Tanzania! Ipo siku Mungu atatupa uelewa.
 
Mniwie radhi kwa kuuliza. Nauliza kwa mara ya mwisho. Sitauliza tena. Nitabaki kimya hata kisemwe au kifanywe niní. Sitauliza tena juu ya Escrow. Nitasubiria tu kashfa za bomba la gesi na sukari. Basi.

Kwakuwa tumeambiwa na Rais kuwa mabilioni yaliyokuwemo Escrow yote yalikuwa ya IPTL. Na kwakuwa tumeambiwa na kuaminishwa na Rais kuwa mabilioni ya Escrow yalilipwa au kupewa mwenyewe ambaye ni IPTL.

Na kwakuwa mwenye mabilioni,IPTL,amechukua chake kiutaratibu na Serikali ilijua. Je,uchunguzi na hatua zinazoendelea kuchukuliwa hivi sasa zinalenga niní? Wanaochunguzwa wanachunguzwa kwa makosa yapi hasa?

Hata nisipojibiwa,nitaridhika kama mwafrika!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Umesahau,na Je Tibaijuka amesitishiwa Uwaziri kwa makosa yapi
 
Vipi Kuhusu Rais?yeye ni sehemu ya bunge na ametofautiana nalo-katiba inasemaje juu ya hili?
Kwa kweli Rais wetu kaonyesha ukomavu unaotakiwa kwenye nafasi ile. Kaamua, tusubiri bunge wakikutana watasemaje. Ni mapema mno kuhukumu.
 
Ziliwekwa kule kwa muda kwa kuwa kulikuwa na kesi kati wanahisa wa IPTL.Zikawekwa kwenye akaunti ya ESCROW ambayo hakuna mwenye hisa yeyote angeweza kuchukua hadi kesi imalizike.Zingewekwa akaunti ya IPTL mwanahisa yeyote angeweza amka asubuhi na kuzitoa pesa zote ndio maana zikawekwa kwenye ESCROW ACCOUNT.
Hakika hili ndilo lilikuwa jibu la awali la Prof Muhongo na mwenzake Maswi kuwa escrow ilikuwa ni zao la ugo vi kati ya wana hisa. Baada ya ukaguzi jibu likajulikana kuwa ni malalamiko kati ya Tanesco na IPTL. Sasa hoja ikawa fedha zi za umma kwa sababu zilikuwa ni za kulipia gharama za umeme!
 
Umesahau,na Je Tibaijuka amesitishiwa Uwaziri kwa makosa yapi

Aliomba mchango wa shilingi bilioni moja na milioni mia sita kwa kusema ni kwa ajili ya shule ya BARBO badala ya msaada huo kuingia kwenye akaunti ya shule akauingiza kwenye akaunti yake binafsi.Alikiuka maadili ya kuchangisha kama kiongozi.Ilitakiwa pesa ile kimaadili iingie moja kwa moja akaunti ya shule.
 
Maazimio haya yalifikiwa na Bunge(Wananchi) kwa kuamini/kujua kuwa pesa zile zilikuwa ni za Umma.Kwa Kuwa mkuu wa nchi amethibitisha kuwa pesa zile hazikuwa za umma,Mapendekezo yale yalitakiwa yawe yamejifuta yenyewe.Kuendelea kuchunguza tuhuma hewa ni ufisadi mwingine

Hakuna mahala katika maazimio ya bunge ambapo imesema kuwa hizo ni pesa za umma. Kumbuka hilo. Kama wewe umepaona tuoneshe na sisi. La sivyo unaweza kuwa na maoni yako lakini yasiyo kweli.

Mpaka CAG aliamrsha TANESCO wafute kwenye vitabu vyao kwani hizo pesa hawana haki ya kusema zao.

Mlitaka umeme wa bure?
 
Hela ndio kila kitu. Wew na mm hatujapata kitu kwahiyo waachie wenyewe wajisafishe kwa hiyo na ww kazini kwako iba hela alafu useme sio zakazini kwako japokuwa uliiba
 
Mniwie radhi kwa kuuliza. Nauliza kwa mara ya mwisho. Sitauliza tena. Nitabaki kimya hata kisemwe au kifanywe niní. Sitauliza tena juu ya Escrow. Nitasubiria tu kashfa za bomba la gesi na sukari. Basi.

Kwakuwa tumeambiwa na Rais kuwa mabilioni yaliyokuwemo Escrow yote yalikuwa ya IPTL. Na kwakuwa tumeambiwa na kuaminishwa na Rais kuwa mabilioni ya Escrow yalilipwa au kupewa mwenyewe ambaye ni IPTL.

Na kwakuwa mwenye mabilioni,IPTL,amechukua chake kiutaratibu na Serikali ilijua. Je,uchunguzi na hatua zinazoendelea kuchukuliwa hivi sasa zinalenga niní? Wanaochunguzwa wanachunguzwa kwa makosa yapi hasa?

Hata nisipojibiwa,nitaridhika kama mwafrika!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

mzee Tupatupa, kinachoendelea ndani ya nchi hii ni full comedy. Ukitumia logics na common sense kwa mambo yanayofanyika Tz utaumia sana. Let's just hope that one day things will change.
 
Mzee tupa tupa kama amejikatia tamaa vile maana mpango wao unaelekea kufail sasa.
mzee rudisha hela za mangi,kama ushazila useme member tupitishe mchango.
 
Hakika hili ndilo lilikuwa jibu la awali la Prof Muhongo na mwenzake Maswi kuwa escrow ilikuwa ni zao la ugo vi kati ya wana hisa. Baada ya ukaguzi jibu likajulikana kuwa ni malalamiko kati ya Tanesco na IPTL. Sasa hoja ikawa fedha zi za umma kwa sababu zilikuwa ni za kulipia gharama za umeme!

Kulikuwa kuna issue mbili tofauti, ya tanesco na escrow ilishatolewa maamuzi zamani sana na Kikwete kalielezea hilo, rudia hotuba yake, kama una uwezo huo.

Na pia kulikuwa kuna utata kati ya wabia na ndiyo huo ulipelekea IPTL kuwa chini ya RITA, baada ya mgogoro huo kwisha na kwa kuwa tatizo la IPTL TANESCO liliisha amuliwa na ICSID ikawa hakuna tena kadhia nyingine bali kupata ushirikiano wa pande zote zinazohusika na ndicho kilichafanyika na kufikiwa muafaka uliopitishwa na mahakama.

Na isitoshe, mahakama ikahakikisha kuwa Ruge analipwa na kodi analipa na PAP wanakubali kuwekeza tena kwa bei nafuu kabisa.

Naona mnazunguka mbuyu tu, yote yako wazi kama mchana wa saa sita.
 
Shidaaa umekaririshwa, azimio azimo .

Wewe umesema hili swali mlishajibu sasa mlijibu kama nani au wewe FaizaFoxy ni bunge au serikali au wewe ndiyo Rais wa nchi hii?

Azimio la bunge, Ulitaka azimio langu au lako? huna na sina.

Naona yameikuingia na sasa unabwabwaja tu.

Hii ngoma imedunda tafuteni jingine.
 
mkuu tupatupa uliadi utakuja na majibu ya wale wazee wa dar mbona kimya au uliwapa majibu wazee sisi hatutakiwi kujua?

Tupatupa wa Lumumba,
Wewe unakaa mtaa huohuo wa chama chenu cha mafisadi.Bila shaka unajua kila kitu kinachoendelea hapo.Acha kujifanya hamnazo!
 
Mniwie radhi kwa kuuliza. Nauliza kwa mara ya mwisho. Sitauliza tena. Nitabaki kimya hata kisemwe au kifanywe niní. Sitauliza tena juu ya Escrow. Nitasubiria tu kashfa za bomba la gesi na sukari. Basi.

Kwakuwa tumeambiwa na Rais kuwa mabilioni yaliyokuwemo Escrow yote yalikuwa ya IPTL. Na kwakuwa tumeambiwa na kuaminishwa na Rais kuwa mabilioni ya Escrow yalilipwa au kupewa mwenyewe ambaye ni IPTL.

Na kwakuwa mwenye mabilioni,IPTL,amechukua chake kiutaratibu na Serikali ilijua. Je,uchunguzi na hatua zinazoendelea kuchukuliwa hivi sasa zinalenga niní? Wanaochunguzwa wanachunguzwa kwa makosa yapi hasa?

Hata nisipojibiwa,nitaridhika kama mwafrika!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Wanachunguzwa kwa kula njama kulikosesha taifa kodi ya takribani bilioni 26.Na pia ilibidi IPTL na tanesco wakae na kuelewana kuhusu tozo stahiki kwa IPTL kabla ya akaunti ya escrow tegeta kufungwa ,jambo ambao halikufanyika kutokna na hila na michezo michafu ya wao watuhumiwa.
 
Jiulize swali dogo tu likusaidie; Tibaijuka kafukuzwa au kaachishwa kazi? Mbona bado ni MBUNGE na mshahara anao?
Kwa maana ya kazi ya uwaziri au?ua unamaanisha kazi ya ubunge ni sawasawa na kazi ya Uwaziri?Mkuu nimeshindwa kujua tofauti ya kuachishwa kazi na kufukuzwa,nisaidie
 
Labda alimaanisha kuwa wanafanyiwa "Uchunguzi wa afya zao"....
 
Azimio la bunge, Ulitaka azimio langu au lako? huna na sina.

Naona yameikuingia na sasa unabwabwaja tu.

Hii ngoma imedunda tafuteni jingine.

Tatizo lako uzee umekuganda halafu unakaririshwa vitu usivyovijua sasa unajikuta unajibu kitu ambacho hujaulizwa.

Kapike vitumbua tu.

Only in Tanzania
 
Back
Top Bottom