Maswali ya mwisho juu ya Escrow

Maswali ya mwisho juu ya Escrow

Anayebisha kuwa pesa siyo za IPTL natilia shaka sana akili zake huenda zinashida mahala fulani.

ni za IPTL kwa hukumu ipi? account ilifungiwa pesa ziwekwe wakati ikisubiriwa muafaka kwenye mgogoro baina ya IPTL na TANESCO mgogoro umeisha?? acha kutumia akili za pongo wewe?!
 
Kwa hili sakata la ESCROW Rais ametoa funzo kubwa sana kwa waliomtangulia na watakaokuja:

-Kwanza ni somo la utawala bora unaofuata misingi ya sheria, kanuni tulizojiwekea kwenye utumishi na mamlaka mbalimbali;
-Pili ni mgawanyo wa madaraka kikatiba na kisheria juu ya mihimili yetu mitatu ambayo ni Dola, Mahakama na Bunge;
-Tatu ni juu ya dhana nzima ya uwajibikaji pale inapolazimu kufanya hivo na
-Nne ni ITIFAKI na nidhamu.

Kwa kweli ambao hamtaki kumwelewa Rais wetu ni kwa kuwa tu mliamua kwa pupa, kwa jazba, kwa visasi na mihemuko ya kisiasa. Kwa mfano, ilikuwaje Bunge zima likashindwa kuelewa taratibu za kuwawajibisha Majaji? Ilikuwaje Bunge zima likashindwa kuelewa kuwa Katibu Mkuu ni Mtumishi wa UMMA na ziko taratibu za kufuatwa ili kumwondoa madarakani?
Mkuu unaakili sana big up.Nisaidie tu hili moja.Hivi waziri (mfano mama Tibaijuka) ni Mtumishi wa nani?
 
Huyu Singa aliiangusha KANU kwa deal zake na mtoto wa Moi sasa anaiangusha CCM kwa deal zake na familia ya Rais
Msilishwe maneno na celebrities wa siasa zetu za Bongo. Serikali ya Moi ilianguka baada ya KANU kugawanyika mapande. Sio kwa ajili ya Singasinga.
 
Maazimio haya yalifikiwa na Bunge(Wananchi) kwa kuamini/kujua kuwa pesa zile zilikuwa ni za Umma.Kwa Kuwa mkuu wa nchi amethibitisha kuwa pesa zile hazikuwa za umma,Mapendekezo yale yalitakiwa yawe yamejifuta yenyewe.Kuendelea kuchunguza tuhuma hewa ni ufisadi mwingine
Mkuu huyo bibi anayajua yote hayo ila anajaribu kupotosha umma.
Kuficha wizi ni kitu kigumu sana , ni sawa sawa na mtu mzima kujaribu kujisitiri na taulo la mtoto mdogo, unafunika hapa , pale panafunuka basi inakuwa tabu tupu.
 
Escrow is money or property which is given to someone, but which is kept by another person until the first person has done a particular thing or met a particular requirements( mainly LEGAL).
Rais wetu alikuwa sahihi kwa tafsiri hiyo. Tuendelee tu na porojo za akina Kafulila.
Hujanijibu mkuu.Mgogoro kati ya wanahisa wa IPTL-watu binafisi serikali imeingiaje hapa?
 
Hilo swali tumeshalijibu humu, unaonesha ni mvivu wa kutembea-tembae JF kwenye mada zinazohusu hii kadhia, si kitu, hili hapa jibu la aliyeuliza kama wewe, nawe litakufaa:

Mlijibu humu kama serikali au chama chetu ?
 
Mkuu unaakili sana big up.Nisaidie tu hili moja.Hivi waziri (mfano mama Tibaijuka) ni Mtumishi wa nani?
Waziri sio Mtumishi kama alivyo Katibu Mkuu. Waziri ni MWANASIASA tena MBUNGE. Uteuzi wa waziri una taratibu zake. Ajira yake inaendelea kuwepo kwa kadri itakavyompendeza Rais. Tibaijuka sasa karudi bungeni. Maswe akiondoka ni jumla.
 
Shangazi FaizaFoxy nami nimekuwa mvivu naomba kufahamu AG amaendika barua ya kujiuzulu akidai ushauri wake haukueleweka na kupelekea kuchafua hali ya hewa, kwa nini asifafanue tena huo ushauri wake ili aeleweke na kwanini bosi wake ambaye ni JK aridhie kujiuzulu kwake?

Tuwekee hiyo barua, au ni ya kusadikika?
 
Hujanijibu mkuu.Mgogoro kati ya wanahisa wa IPTL-watu binafisi serikali imeingiaje hapa?
Hilo limeng'ang'aniwa na akina Kafulila ili Singasinga aonekane sio mmiliki halali wa IPTL! Sikumsikia Rais wetu akiliongelea hilo. Halituhusu sana zaidi ya uwepo wa mitambo ile ndani ya nchi yetu, inazalisha umeme tunaununua, tunautumia.
 
Msilishwe maneno na celebrities wa siasa zetu za Bongo. Serikali ya Moi ilianguka baada ya KANU kugawanyika mapande. Sio kwa ajili ya Singasinga.
Wewe hujaona kama serikali yako imegawanyika vipande vipande?.Waziri mmoja anasema hizi ni pesa za umma mwingine anasema si za umma,sehemu moja ya bunge (Wabunge) wanatoa maazimio kushughulikia wezi wa fedha ya umma,upande wa pili wa Bunge(Rais) anasema si pesa ya Umma,Rais anashindwa kuamini vyombo ambavyo wakuu wake amewateua mwenyewe-Wewe unategemea kuona mgawanyiko wa aina gani ndugu ili uamini ccm inaanguka.
 
My take kwenye hili swala limekwisha pita. Hakuna hata siku moja toka JK ameingia madarakani alikwisha kutoa maamuzi Kwa mujibu wa uchunguzi wa vyombo vilivo chini yake. Hio ilikua ni njia tu ya kutoa majibu ili ionekane Rais kaongea. Tusubiri kashifa zonazokuja kwenye hili msitegemee muujiza mpya ndo limefungwa. Mwisho Kwa ushauri tu akina dada na mama zetu mmekuwa na tatizo la kupiga kura kwa kuangalia mvuto wa mgombea ilhali wengi wenu mmeshaolewa na hata km mngekuwa bado hatowaoa wote. Tutumia akili zetu kuchagua viongozi na sio hisia na mihemko ya kimaumbile. We can make a big change 2015. Changes begin with me.
 
Mlijibu humu kama serikali au chama chetu ?

Kwanini usiwaulize bunge walioleta hilo azimio? analoouliza huyo mleta mada wala si jipya na limo kwenye azimio namba 3 la maazimio ya bunge yaliyopelekwa kwa Kikwete, hili hapa:

Azimio la Tatu: Linasomeka; "Bunge linaazimia kwamba TAKUKURU, Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya ulinzi na usalama vichukue hatua stahili kwa mujibu wa sheria za nchi yetu dhidi ya watu waliotajwa kwenye taarifa maalum ya Kamati husika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya Akaunti ya ESCROW, na watu wengine watakaogundulika kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea kuhusu kuhusika kwao katika vitendo hivyo vya jinai"

Vyombo husika vimekwishaagizwa kufanya hivyo na kazi imeanza na inaendelea. Ikiwa wapo watu wenye makosa hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.
 
Hilo limeng'ang'aniwa na akina Kafulila ili Singasinga aonekane sio mmiliki halali wa IPTL! Sikumsikia Rais wetu akiliongelea hilo. Halituhusu sana zaidi ya uwepo wa mitambo ile ndani ya nchi yetu, inazalisha umeme tunaununua, tunautumia.
Nakupa dawa ya upofu wako naamini itakufanya uone kuanzia sasa ila kama shida in upofu tu na si ubongo.Escrow account ilifunguliwa kwa kuwa kulikuwa na mgogoro kati ya Tanesco (Shirika la umma-hapa ndipo serikali inaingilia) na IPTL huu ndio ukweli si swala la Kafulila wala JK.Zile pesa zilikuwa za Tanesco kwa upande mmoja na upande mwingine zilikuwa za BOT waliokuwa wanazitunza.-Umewahi kusikia SSB akitaka kulipia magari Scania ya kusambazia bidhaa yake AG anaombwa ushauri?
 
Wewe hujaona kama serikali yako imegawanyika vipande vipande?.Waziri mmoja anasema hizi ni pesa za umma mwingine anasema si za umma,sehemu moja ya bunge (Wabunge) wanatoa maazimio kushughulikia wezi wa fedha ya umma,upande wa pili wa Bunge(Rais) anasema si pesa ya Umma,Rais anashindwa kuamini vyombo ambavyo wakuu wake amewateua mwenyewe-Wewe unategemea kuona mgawanyiko wa aina gani ndugu ili uamini ccm inaanguka.
Mtu mwenye akili zake timamu ambaye alifuatilia mjadala ule Bungeni atakuwa alibaini mapungufu mengi sana. Mjadala ule ulikuwa ni void ab initio.

Natarajia mtu kama Prof Mark Mwandosya baada ya kutofautiana na Rais angejiuzulu tu. Vinginevyo kwenye Cabinet ijayo apumzishwe tu kwani amepona. Hana wizara.
 
Tuwekee hiyo barua, au ni ya kusadikika?
Kwani mimi ndio bosi wa Werema mpaka niwe na barua ya yeye kujiuzulu?,taarifa za kuchafua hali ya hewa anakodai AG aliyejiuzu zimenukuliwa na vyombo vya habari.
Labda nikuulize hivi, Kwanini Werema kajiuzulu?, je kujiuzulu na kustaafu ni vitu viwili vinavyo fanana?
Asante
 
Kwanini usiwaulize bunge walioleta hilo azimio? analoouliza huyo mleta mada wala si jipya na limo kwenye azimio namba 3 la maazimio ya bunge yaliyopelekwa kwa Kikwete, hili hapa:

Azimio la Tatu: Linasomeka; “Bunge linaazimia kwamba TAKUKURU, Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya ulinzi na usalama vichukue hatua stahili kwa mujibu wa sheria za nchi yetu dhidi ya watu waliotajwa kwenye taarifa maalum ya Kamati husika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya Akaunti ya ESCROW, na watu wengine watakaogundulika kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea kuhusu kuhusika kwao katika vitendo hivyo vya jinai”

Vyombo husika vimekwishaagizwa kufanya hivyo na kazi imeanza na inaendelea. Ikiwa wapo watu wenye makosa hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.

Shidaaa umekaririshwa, azimio azimo .

Wewe umesema hili swali mlishajibu sasa mlijibu kama nani au wewe FaizaFoxy ni bunge au serikali au wewe ndiyo Rais wa nchi hii?
 
Last edited by a moderator:
Waziri sio Mtumishi kama alivyo Katibu Mkuu. Waziri ni MWANASIASA tena MBUNGE. Uteuzi wa waziri una taratibu zake. Ajira yake inaendelea kuwepo kwa kadri itakavyompendeza Rais. Tibaijuka sasa karudi bungeni. Maswe akiondoka ni jumla.
Kama Waziri si mtumishi wa umma,nani anamlipa mshahara na marupurupu mengine na anafanya kazi ya nani na kwa nn?Je Katibu mkuu anapatikana vipi?
 
Nakupa dawa ya upofu wako naamini itakufanya uone kuanzia sasa ila kama shida in upofu tu na si ubongo.Escrow account ilifunguliwa kwa kuwa kulikuwa na mgogoro kati ya Tanesco (Shirika la umma-hapa ndipo serikali inaingilia) na IPTL huu ndio ukweli si swala la Kafulila wala JK.Zile pesa zilikuwa za Tanesco kwa upande mmoja na upande mwingine zilikuwa za BOT waliokuwa wanazitunza.-Umewahi kusikia SSB akitaka kulipia magari Scania ya kusambazia bidhaa yake AG anaombwa ushauri?
Nimekupatia tafsiri ya escrow account nikidhani ingekusaidia. Naona bado unataka kurukia matusi sasa! Zile pesa sio za TANESCO wala BOT hazimhusu kabisaa. TANESCO walishazilipa kwa IPTL. Kumbuka pia pesa nyingine zilishatangulia kulipwa kabla ya mgogoro huu kuibuka na account hii kufunguliwa.
 
Mtu mwenye akili zake timamu ambaye alifuatilia mjadala ule Bungeni atakuwa alibaini mapungufu mengi sana. Mjadala ule ulikuwa ni void ab initio.

Natarajia mtu kama Prof Mark Mwandosya baada ya kutofautiana na Rais angejiuzulu tu. Vinginevyo kwenye Cabinet ijayo apumzishwe tu kwani amepona. Hana wizara.
Vipi Kuhusu Rais?yeye ni sehemu ya bunge na ametofautiana nalo-katiba inasemaje juu ya hili?
 
Nimekupatia tafsiri ya escrow account nikidhani ingekusaidia. Naona bado unataka kurukia matusi sasa! Zile pesa sio za TANESCO wala BOT hazimhusu kabisaa. TANESCO walishazilipa kwa IPTL. Kumbuka pia pesa nyingine zilishatangulia kulipwa kabla ya mgogoro huu kuibuka na account hii kufunguliwa.
Oooh nimekusoma sasa,Kumbe IPTL wana account BOT-imetulia hii mkuu
 
Back
Top Bottom