Maswali ya kisiasa yenye kuhitaji majawabu yake

ASIWAJU

JF-Expert Member
Nov 18, 2022
1,939
1,625
Karibuni wadau kwa majawabu yenu juu ya maswali yangu haya yafuatayo.

1. Kwa nini wanasiasa wa TANU na vyama baadhi miaka ya 1950s walishinikiza suala la wao kupewa uhuru kutoka kwa Muingereza? Sababu gani ya msingi ili wafanya wao kushinikiza hitaji lao?

2. Kwa nini Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika chini ya Mwalimu Nyerere ili amua kuchukua maamuzi ya kuunganisha nchi huru ya Tanganyika na kisiwa huru cha Zanzibar chini ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Karume 1964?

3. Ni sababu zipi zili lazimisha muungano kuwepo?

4. Baada ya muungano mipaka na serikali ya Jamhuri ya Tanganyika ni ipi ? Na mipaka na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni ipi?

5. Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika ni ipi? Na Katiba ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni ipi?

6. Ni kwa namna gani serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina nufahika na aina hii ya muungano?

7. Pia ni kwa namna gani serikali ya Jamhuri ya Tanganyika ina nufahika na aina hii ya Muungano?

8. Hatua za kuchukua katika kuvunja huu muungano ni zipi?

Karibuni kwa majawabu ya maswali na pia maswali ya nyongeza kwa manufaa ya wote.
 
Muungano unanufaisha zaidi upande mmoja na kuminya upande mwingine.
kibaya zaidi hoja nzito kama hizi za muungano zinaminywa kuwa mijadala huru na ukijaribu unapakwa matope kwa nguvu zote,kumbuka Mtikila(Mtanganyika)alipakwa matope kiasi wananchi wakamuona mbaya anataka kusababisha vita.
 
Nadhani suala la elimu bora ni tatizo katika kundi kubwa la wananchi hapa Tanzania.
 
Muungano unanufaisha zaidi upande mmoja na kuminya upande mwingine.
kibaya zaidi hoja nzito kama hizi za muungano zinaminywa kuwa mijadala huru na ukijaribu unapakwa matope kwa nguvu zote,kumbuka Mtikila(Mtanganyika)alipakwa matope kiasi wananchi wakamuona mbaya anataka kusababisha vita.
Kwahili ni sahihi,kuna vitu vingi wazenji wananufaika zaidi........ kuliko sisi...
 
Karibuni wadau kwa majawabu yenu juu ya maswali yangu haya yafuatayo.

1. Kwa nini wanasiasa wa TANU na vyama baadhi miaka ya 1950s walishinikiza suala la wao kupewa uhuru kutoka kwa Muingereza? Sababu gani ya msingi ili wafanya wao kushinikiza hitaji lao?

2. Kwa nini Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika chini ya Mwalimu Nyerere ili amua kuchukua maamuzi ya kuunganisha nchi huru ya Tanganyika na kisiwa huru cha Zanzibar chini ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Karume 1964?

3. Ni sababu zipi zili lazimisha muungano kuwepo?

4. Baada ya muungano mipaka na serikali ya Jamhuri ya Tanganyika ni ipi ? Na mipaka na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni ipi?

5. Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika ni ipi? Na Katiba ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni ipi?

6. Ni kwa namna gani serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina nufahika na aina hii ya muungano?

7. Pia ni kwa namna gani serikali ya Jamhuri ya Tanganyika ina nufahika na aina hii ya Muungano?

8. Hatua za kuchukua katika kuvunja huu muungano ni zipi?

Karibuni kwa majawabu ya maswali na pia maswali ya nyongeza kwa manufaa ya wote.
Wazee wa Tanu kudai Uhuru kipindi kile ukisoma historia ni utashi baada ya baadhi yao kuwa wamepata Elimu na ufahamu, muungano wa Tanganyika na zenji wengi huwa wanasema ni sababu za kiusalama na kiulinzi Kwa Tanganyika na Tanganyika ikafa baada ya hapo, SMZ wanaKatiba, bendera yao na wimbo wao....wakati sisi watanganyika wa bara hatuna.

Anyway muungano uwepo ila Mtanganyika aruhusiwe kwenda kumiliki ardhi, kugombea, Kuteuliwa kuwa DC, RC,Wizara za SMZ na nafasi zingine tofauti na hivyo itakuwa unafiki tu kuwa na muungano unaonufaisha wachache........
 
Inasemekana sehemu kubwa ya ukanda wa pwani ilikuwa sehemu ya Zanzibar, hivyo hofu iliyopo ni iwapo Zanzibar itatengana na Tanganyika, kuna uwezekano wakosonga mbele kudai mipaka yao. Hapo kuna uwezekano wa kufanya Tanganyika kuwa landloked country.
 
Hakuna namna ya Kuvunja Muungano, si kwa katiba ya Muungano wala Mkataba wa Muungano.

Sababu zilizopelekea kuwepo kwa Muungano ni nyingi baadhi ni kama ifuatavyo:-

Mosi ni Shauku ya Nyerere juu ya Afrika moja,

Pili ni hofu ya Karume juu ya kuatamia mamlaka ya Utawala wa Zanzibar,

Tatu ni nchi za Magharibi kuondoa uwezekano wa Zanzibar kuingia kwenye Ukomnisti.
 
Wazee wa Tanu kudai Uhuru kipindi kile ukisoma historia ni utashi baada ya baadhi yao kuwa wamepata Elimu na ufahamu,muungano wa Tanganyika na zenji wengi huwa wanasema ni sababu za kiusalama na kiulinzi Kwa Tanganyika na Tanganyika ikafa baada ya hapo,SMZ wanaKatiba, bendera yao na wimbo wao....wakati sisi watanganyika wa bara hatuna.

Anyway muungano uwepo ila Mtanganyika aruhusiwe kwenda kumiliki ardhi, kugombea,Kuteuliwa kuwa DC,RC,Wizara za SMZ na nafasi zingine tofauti na hivyo itakuwa unafiki tu kuwa na muungano unaonufaisha wachache........
Wananchi wanapaswa kufahamishwa ni vitu gani walivyo unganisha na ambavyo havija unganishwa ? na utendaji kazi wa hizi serikali za Zanzibar, Tanganyika na Muungano kama zipo huru ?
 
Hapo no 1 tunatofautiana, uhuru wa Tanzania haukutokana na kushinikizwa kwa Uingereza, Tanganyika halikua colon la mwingereza, nchi yetu ilikua chini ya UN, ndio maana Nyerere na wenzake walikwenda New York sio London, binafsi ilikua mapema mno kwa Tanganyika kupata uhuru kutoka UN,na mbaya zaidi ziara ya Nyerere China in mid 60s ndio ilituvuruga kabisa kama nchi. Nitarudia Muungano baadaye, nipo shambani lingusenguse
 
Inasemekana sehemu kubwa ya ukanda wa pwani ilikuwa sehemu ya Zanzibar, hivyo hofu iliyopo ni iwapo Zanzibar itatengana na Tanganyika, kuna uwezekano wakosonga mbele kudai mipaka yao. Hapo kuna uwezekano wa kufanya Tanganyika kuwa landloked country.
Duuuh!, ndio maana una nga'ng'aniwa kwa nguvu sana hasa huku Tanganyika.
Kama ni hivyo basi hii ni shida.

Kwani hilo eneo Zanzibar wameanza kumiliki toka lini ? Maan ramani za kikoloni mbona hazioneshi hivyo ?
 
Back
Top Bottom