Maswali muhimu kuhusu serikali kuhamia Dodoma

Kuna watu kazi yao ni kukosoa kila kitu bila kutathimini vyema kauli za wahusika, Mheshimiwa alisema ndani ya kipindi cha awamu yake ya kwanza ya uongozi lkn mtu analazimisha ahadi itimie ndani ya miezi miwili!!!! kweli tuna safari ndefu ya kujikomboa kifikra kwa aina hii ya watu tuliopo!!!!
Wale waliosema ndani ya wiki watakuwa Dodoma unewasahau?
 
Baada ya Rais magufuli kutangaza serikali kuhamia Dodoma, kuna mawaziri walisema wiki inayofuata watakuwa tayari wameshahamia akiwemo waziri wa kilimo. Lakini nashangaa hadi leo mawaziri hao nakutana nao mitaani hapa jiji.

Hivi walijua kuhama ni kazi rahisi ati eee? Au walizungumza vile ili kunogesha genge.
si mbege tu zinawahangaisha
 
Huu mchezo hauhitaji hasira,Unajua maana ya neno unafiki?
Ok najua tizeba yupo mwanza anashughulikia masuala ya uvuvi,but ofisi yake bado ipo Dar.Yeye alikuwa wa kwanza kupata kiki kwenye vyombo vya habari kuwa atakuwa wa kwanza kuhamia Dodoma. Alijua kuhamisha ni yeye na naibu wake kupanda gari kwenda Dodoma..
Duniani kote hamna serikali iliyohisha makao makuu kwa muda wa mwaka mmoja.
Yangu macho,nione tunakoelekea
Na ndio maana JPM alisema kabla ya 2020 atakuwa amehamia yeye na serikali yake. Haraka ya nini. Subiri 2020 ulete tathmini yako.
 
Natamani kulia lkn machozi nahisi yalishaisha! natamani kupigana lkn sijui nipigane na nani! natamani nimtukane mtu lkn sijui ni nani! we acha tu, dharau sana hii!
 
Hivi leo kumeamkaje huko Darisalamu, isijekua wameshaanza manda wa majengo na mimi sina taarifa, mimi nataka yale majengo pacha pale
 
"There are people in the world so hungry, that God cannot appear to them except in the form of bread." Mahatma Gandhi
 
Juzi waziri mkuu amepokea msaada wa madawati 100 kutoka umoja wa nchi za Kuwait. Hilo mimi nimeona kwa Tanzania ni kama tusi. Kama hadi vitu vidogo kama madawati 100 yenye thamani ya mil 12 tunapewa misaada kutoka nchi za nje halafu unaenda kupokelewa na Waziri Mkuu kwa mbwembwe kibao.

Wakati huo Tanzania ina mpango wa kutumia mabillioni ya shilingi kuhamia Dodoma. Na kwanini serikali isifanye mambo mengine ya msingi halafu hilo swala liwe la mwisho.

Kwa sababu swala la kuhamia Dodoma sio tatizo.
Mkuu hiki kitu ni siriaz au unatania ...... maana kama w/mkuu anaweza kufunga barabara na misafara inayosababisha vifo vya wagonjwa kwa ajili ya kupisha msafara wake kisha yeye anaenda kupokea madawati 100,ambapo gharama za msafara wake mmoja unazidi alichoenda kukipokea nahisi kuna tatizo.
 
hakuna namna lazima tu,mtakubaliana na sisi kina gogo la shamba pale tuliposema kwamba hii miaka mitano ya Makufuli tutasikia na kuona mambo mengi ya ajabu
 
Mkuu hiki kitu ni siriaz au unatania ...... maana kama w/mkuu anaweza kufunga barabara na misafara inayosababisha vifo vya wagonjwa kwa ajili ya kupisha msafara wake kisha yeye anaenda kupokea madawati 100,ambapo gharama za msafara wake mmoja unazidi alichoenda kukipokea nahisi kuna tatizo.
mkuu hii nchi wanako tupeleka ni kubaya.
 
Juzi waziri mkuu amepokea msaada wa madawati 100 kutoka umoja wa nchi za Kuwait. Hilo mimi nimeona kwa Tanzania ni kama tusi. Kama hadi vitu vidogo kama madawati 100 yenye thamani ya mil 12 tunapewa misaada kutoka nchi za nje halafu unaenda kupokelewa na Waziri Mkuu kwa mbwembwe kibao.

Wakati huo Tanzania ina mpango wa kutumia mabillioni ya shilingi kuhamia Dodoma. Na kwanini serikali isifanye mambo mengine ya msingi halafu hilo swala liwe la mwisho.

Kwa sababu swala la kuhamia Dodoma sio tatizo.
Tumerogwa na aliyeturoga kafa na dawa ndo tatizo tulilonalo mkuu
 
Ni kweli tuna matatizo mengi lakini kwa Hulka ya Mkuu wa kaya, hawezi kuendelea kuwa chini ya UKAWA kwa miaka yote mitano ya uongozi wake wa Kaya! Jiulize, unawezaje kufurahia kuwa na pesa na mali nyingi lakini unaishi kwa mdogo wako?
 
Hakuna cha ajabu pale! kilichoshindikana hapa kwa zaidi ya nusu karne! Ni pesa ya walipakodi inataka kubadirishiwa matumizi.

Chonde chonde watanzania wenzangu makao makuu Dodoma ni tego lililotegwa likimsubili yeyote alikanyage!

Kusema kweli hata aliyelitega na yeye alishidwa kulitegua, akawa akilipita kwa tahadhari, hatimae akamaliza zamu yake salama!

Watatu waliomfuatia mtegaji hawakudhubutu hata kwa maneno tu kwa hofu ileile ya mtangulizi wao!

Nadhani waligundua kuwa matatizo ya nchi hii hayapo kwenye wapi yalipo Makao makuu ya chama au serikari.

Ukizingatia katika dunia hii ya fungamano kuu la Mawasiliano; mwanadamu anaweza kuendesha shughuri za kiutawala akiwa mahali popote pale, hata kama mahali hapo ni mwezini.

Ndiyo maana hili limejaa katika fahamu za watu wengi wa leo mithiri ya bahari ilivyojazwa maji.

Pengine nitoe angalizo kwa serikali yetu hii sikivu,

1) Wasione ni unyonge kuupotezea mpango huu kwa sababu ya vipaumbele vingi tulivyonavyo kama taifa kwa sasa,Mkifanya hivyo mtakuwa na uwezo wa kufanya mengi kati ya yale mliyowaahidi wananchi.

2) Kinyume chake, mkipuuza na kwamba eti mkahamia Dodoma ndani ya miaka hii mitano, hapo kubarini kwamba hapo mtakuwa mmeuvaa mtego wa kufanya jambo lenye gharama kubwa ingawa halina matokeo yanayopeleka unafuu wa maisha kwa wananchi!

Sasa basi, naomba pokeeni ushauri wangu au vinginevyo Mimi sijui nani atawanasua katika hili tego la Dodoma!
 
Utakuwa na bahati ikiwa angalau wakikusikia.
Kukuelewa mmmh!!!!
 
Mkuu inaonekana jamaa wamedhairia haswa na sidhani kama watakuelewa
 
Utakuwa na bahati ikiwa angalau wakikusikia.
Kukuelewa mmmh!!!!
Kweli kabla ya kueleweka kuna swala muhimu la kusikika. Sijui kama mpaka sasa wametusikia kweli achilia mbali kutuelewa
 
Back
Top Bottom